Mkuu wa Wilaya Jokate azuru Afrika Kusini kutangaza zao la mkonge na bidhaa zake pamoja na masuala ya uhifadhi wa wanyamapori na mazingira

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
DC JOKATE AZURU AFRIKA YA KUSINI KUTANGAZA ZAO LA MKONGE NA BIDHAA ZAKE PAMOJA NA MASUALA YA UHIFADHI WA WANYAMAPORI NA MAZINGIRA - 28-03-2023

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe Jokate Mwegelo amezuru Afrika Kusini wiki hii kutangaza umuhimu wa Vijana wa Afrika kushiriki katika Ujenzi wa Afrika.

Lengo kuu la Ziara hiyo ni kutangaza zao la Mkonge na bidhaa zinazotokana na Mkonge, Masuala ya uhifadhi wa wanyamapori na Mazingira pamoja na Fursa za mazao Mengine yanayolimwa Wilayani Korogwe Mkoani Tanga. Hata hivyo atatumia fursa hiyo kutangaza Chapa ya 'MADE IN KOROGWE' ikiwa ni sehemu ya kutangaza bidhaa zinazalishwa Wilayani Korogwe Mkoani Tanga

Katika Ziara hiyo, Mhe. Jokate atapata fursa ya kutangaza shughuli Mbalimbali zinazofanywa na wajasiriamali Wanawake na Vijana wa Kitanzania.

"Nina Furaha kutembelea Afrika kusini na kuungana na wafanyabiashara wengine na Viongozi ambao wanashiriki maono ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kujenga Bara Bora la Afrika. Natarajia kushiriki Uzoefu wangu na Kujifunza Kwa wengine" - Mhe Jokate Mwegelo

Pia watajadili jinsi wajasiriamali wa Afrika kusini na Tanzania wanaweza kufanyakazi pamoja ili kukuza ukuaji na Maendeleo katika Bara la Afrika.

"Kuna Watanzania wengi sana Nchini Afrika kusini na Waafrika kusini ambao wanataka kuwekeza katika Nchi yetu hii imekuwa fursa nzuri sana ya Kujadili njia za USHIRIKIANO" - Mhe. Jokate Mwegelo.

Pia Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe Jokate Mwegelo amesema Kuna fursa nyingi sana Korogwe kutoka katika bidhaa rafiki Kwa mazingira zinazotengemezwa na Wanawake wa Korogwe Mkoani Tanga" - Mhe. Jokate Mwegelo Mkuu wa Wilaya ya Korogwe

IMG-20230328-WA0317.jpg

IMG-20230328-WA0320.jpg
IMG-20230328-WA0319.jpg
IMG-20230328-WA0321.jpg
 
Hongera sana, kamaliza uzazi?

Kamuachia baba watoto huyo mtoto?

Mtoto ameanza kulishwa vyakula huku hajatimiza mwaka?

Ba-watoto wake [imarisha-bei] kama ndio yeye anaishi naye ama Jo-ako mwenyewe?

WAnaume tusikimbie majukumu, mtoto kulelewa upande mmoja inaumiza sana, anakosa ujasiri.

HONGERA JOKATE.
 
Usiingize Raisi huku kwenye vitu vidogo vidogo wanavyoweza kufanya hata wajasiriamali.
Kwa hiyo kutangaza Vikapu na mazulia ya Mkonge ni kazi ya Rais?
kaongelea mipaka ya kazi pamoja na majukumu ya kila kazi. Rais katolea mfano.
 
Samahani mimi sipo huko serikalini
Huku kwetu kinachotakiwa ni kuhakikisha kazi inafanyika (na mtu anaruhusiwa kujiongeza) muhimu zaidi, matokeo yaonekane/Ilete faida (result oriented) mengine yote sio kipaumbele
acha uongo mtu huwezi kujiongeza nje ya mipaka yako ya kazi hata kwenye kampuni binafsi.
 
Usiingize Raisi huku kwenye vitu vidogo vidogo wanavyoweza kufanya hata wajasiriamali.
Kwa hiyo kutangaza Vikapu na mazulia ya Mkonge ni kazi ya Rais?
Ni kazi ya DC?
Anapewa Bajeti hiyo?

Acheni kukurupuka ndio maana akiwa WASIRRA kila siku wanateuliwa na akina Happi, Makonda , na wengine kama yule DC wa Sumbawanga wanatumbuliwa, hamna mipaka ya kazi, hamjui halafu hamjui kama hamjui.
 
Nchi ngumu sana hii
Jokate anatangaza mkongwe Made in Korogwe,

Atakuja mwingine ndizi Made in Rombo,

Korosho Made in Tandahimba,

Ulanzi Made in Iringa,

Kwa utaratibu huu tutafika bwashee?

Hivi mkuu wa Wilaya ya Kishapu anaweza kusafiri kwenda sauzi kutangaza zao pamba?

Je huyu ni miongoni mwa watoto pendwa wa awamu hii ya kulamba asali?

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Jokate anatangaza mkongwe Made in Korogwe,

Atakuja mwingine ndizi Made in Rombo,

Korosho Made in Tandahimba,

Ulanzi Made in Iringa,

Kwa utaratibu huu tutafika bwashee?

Hivi mkuu wa Wilaya ya Kishapu anaweza kusafiri kwenda sauzi kutangaza zao pamba?

Je huyu ni miongoni mwa watoto pendwa wa awamu hii ya kulamba asali?

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
Bamboo juice
 
Back
Top Bottom