Hoja ya Mkonge kuimaliza CCM Tanga - Zitto na Mnyika watikisa Korogwe

[h=2]
icon1.png
Re: Hoja ya Mkonge kuimaliza CCM Tanga - Zitto na Mnyika watikisa Korogwe
[/h]
Zitto alivamia ajenda ya Wabunge wa Majimbo ya Korogwe, kwa vyovyote vile alitegemea wangempinga. Angetaka afanikishe ajenda yake, ambayo kimsingi ni nzuri, angewahusisha wenzake wenye dhamana na majimbo hayo. Tatizo lilikuwa ni njia na wala siyo malengo (kama kweli alikuwa nayo, na kama alikuwa na nia ya kizalendo ya kutaka mafanikio kwenye hili). Kama alikuwa anafanya siasa, kama inavyojidhihirisha sasa, matokeo ndiyo hayo - kukumbana na upinzani na ushindani mkali!

Mimi binafsi nimejifunza: Hoja yangu binafsi ya uchimbaji dhahabu Nzega nliyoiwasilisha kwenye zaidi ya mikutano 5 ya Bunge haijawahi kupatiwa nafasi kwa visingizio visivyo na maana kwa vile tu ni ya kipambanaji na mimi niliifanya ni yangu binafsi, sasa nimeamua kuunganisha wadau wengi zaidi ili tushirikiane kuiweka sawa na kuiwasilisha tena. Na sasa nimeamua kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusiana na ajenda ya 'ajira kwa vijana' lakini nitawashirikisha wabunge wenzangu vijana kabla ya kufanya hivyo ili tufanikishe upatikanaji wa ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili...​

Sikonge, Saint Ivuga, Ng'wanza Madaso and 4 others like this.

Dr. Hamisi Kigwangalla, MD, MPH, MBA
Mabadiliko ya kweli yataletwa na sisi...!

Ndugu yangu Kigwangala.
Maneno yako yanaweza kuwaponza Wahs Wabunge wenzako aw Tanga.
Zito na hiyo Mnyika unajua wamekwenda huko kwa Ustashi wa akina nani ?
Hivyo kwenda kwao huko ni SIASA au RUSHWA ?
Tafakari kwanza kabla ya kujiingiza ktk jambo usilolijua ki undani...!!!!!
Unamjua Shamte ?
Unamjua M/kt wa Bodi ya Mkonge ?
Unajua kwa nini mwaka 2012 Zito anautaka uwe mwaka wa MKONGE ?
Unaujua mkopo wa 10bl Uliokopwa kutoka Mfuko mmoja wa Pensheni ?
Unajua Bodi ya Mkonge ilivyotumia Hati zisizokuwa za kwao kujipatia mkopo huo ?
Ushawahi kumsikia Zito japo kwa dakika 3 kulisema shirika lililotoa mkopo huo kulinanga ?
Unajua jinsi pesa hizo zilivyotumika ?
Unajua Kwamba Mnyika kwa kwenda huko AMETOSWA ? (maskini hakujua kama alikuwa msindikizaji tu).
Na meeeeeengi mengine !!
Naomba uwasiliane na Mhe Nassir, Mhe Mtangi, Mhe Pamba, Mhe Maji marefu na Mhe Kitandula.
Bila ya kumsahau Mhe Maghembe (WZR Kilimo).
Nafikiri hao watakupa Majibu sahihi na kwa nini waliipinga hoja ya Zito.




 
Ukweli na kuheshimu ndugu yangu Hamisi K. But fikiri kama akitoke mtu ambaye anaweza kutetea hoja ya dhahabu bila kukushirikisha wewe, kisha useme amerukia hoja isiyo muhusu ndani ya nchi hii ya tanzania ambayo ni haki kwa kila mmoja kutetea maendeleo ya nchi yake kwa nguvu na akili, ukweli ndugu yangu umeniangusha sana na fikira zako, ambazo nimeona zimekaa ki chama na pia kiubaguzi.Na hili ndilo linaangusha uwezo wa wabunge wa CCM, pale mnapo taka hoja zote nzuri ziwe zinu na zikitoka pengine ni mbaya, well ikiwa watu wa ccm mnajulikana kwa kusema ndio so if time itakuja muweze kusema hapana hope mtakuwa mnaitakia nchii hii maendeleo ya dhati na si maelezo mengi bila vitendo nawakilishaaaaa
 
Muitikio katika picha wa watu wa Tanga unatia moyo... kama watatumia haki yao ya msingi kurekebisha makosa ifikapo 2015 ile Tanga ya zamani inaweza kufufuka upya.
 
Sasa mwishimiwa H.Kigwangalla, kwa vile unadiriki kusema kwamba Mheshimiwa Kabwe Zitto ALIVAMIA ajenda ya Wabunge wa majimbo ya Korogwe ambao ni wachache sana bungeni inaonyesha mliamua kwa makusudi kuikwamisha hoja yake kwa kutumia wingi wenu wa rangi ya kijani kwa maana ya itikadi ili hoja hiyo isimjenge Zitto kisiasa! yaani itikadi za vyama mbele bali utaifa nyuma... tutafika kweli? huoni umechangia katika kudumaza na kukatisha tamaa wananchi na vijana wa Tanga ambao hivi sasa maisha yao yamezidi kudidimia kutokana na ugumu wa maisha wakati hoja ya Mh. Zitto ilikuwa mkombozi kwao? Sasa wewe unatarajia kuwasilisha yako, unatarajia nini?
 
Back
Top Bottom