Hivi vazi la taifa limekwenda wapi?

kasyabone tall

JF-Expert Member
Sep 13, 2009
254
59
Hivi vazi la taifa limekwenda wapi?
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, juzi alikaririwa na vyombo vya habari kukemea matumizi ya suti kwa watumishi wa serikali kwa maelezo kuwa, zina gharama kubwa huku Watanzania wengi wakiwa maskini wa kutupwa.
Kauli hiyo ya mheshimiwa Pinda, imekuja wakati akiwa katika mkakati wa kupunguza matumizi ya serikali kwa kuanzia na ununuzi wa magari ya kifahari na kisha kushukia kwenye suti zinazovaliwa na watumishi wa serikali bila kujali mazingira husika.

Kutolewa kwa wazo hilo la Waziri Mkuu kumetukumbusha wazo la vazi la kitaifa ambalo lilipewa kipaumbele na serikali ya awamu ya tatu hata kukaundwa tume ya kufuatilia suala hilo ambalo mpaka sasa halijatiliwa umuhimu unaostahili.

Suala la vazi la kitaifa ni muhimu sana kujenga utaifa na kutambulika kwa haraka kwa raia wa Tanzania hata wanapokuwa nje ya nchi na pia kutangaza utamaduni wetu nje ya mipaka yetu.

Tunapokosa vazi la taifa pia tunakosa utambulisho wa taifa letu na raia wake na linapokosekana kama ilivyo sasa, kila mtu anajitumbukiza kwenye mavazi yanayompendezesha yeye na mengine kama yanayomkera waziri mkuu.

Tunashauri wahusika wa suala la vazi la kitaifa kuliangalia upya suala hilo, ili nguvu za viongozi wetu zinazotumika katika kukemea masuala kama ya suti zielekezwe kwenye masuala ya msingi ya maendeleo ya taifa letu.
 
suti sioni kama ni tatizo, tatizo ni kwa nini hazishonwi hapa hapa bongo? mpaka zinunuliwe ulaya na marekani?
 
Tume tena ? watakula wapi bila tume kuwepo na sasa watakuja na nyingine ?
 
Mkuu kuwa na vazi la taifa ni vigumu sana. Hauwezi ukadesign tu kitu halafu muamue kuwa ni vazi la taifa. Kitu kuwa vazi la taifa lazima liwe na historical na cultural background na lazima jamii ijivunie kitu hicho. Kwa sababu hiyo ni vigumu sana kuwa na vazi la kitaifa.
 
mkuu kuwa na vazi la taifa ni vigumu sana. Hauwezi ukadesign tu kitu halafu muamue kuwa ni vazi la taifa. Kitu kuwa vazi la taifa lazima liwe na historical na cultural background na lazima jamii ijivunie kitu hicho. Kwa sababu hiyo ni vigumu sana kuwa na vazi la kitaifa.

.....kwamba hatuna historia au utamaduni tunaoweza kujivunia hadi kuwa na vazi la kitaifa kama zilivyo nchi za afrika magharibi?kama hatuna basi tuangalie hata mazingira yetu.
 
.....kwamba hatuna historia au utamaduni tunaoweza kujivunia hadi kuwa na vazi la kitaifa kama zilivyo nchi za afrika magharibi?kama hatuna basi tuangalie hata mazingira yetu.

No mkuu ninacho sema mimi ni kuwa vazi la taifa ni kitu gradual. Hauwezi leo hii wewe kama Shaycas ukabuni nguo useme ni ya taifa halafu utegemee moja kwa moja watu watalipokea na kulichukulia kama vazi la taifa. Historically tulikuwa na mavazi ya kikabila lakini hatukua na vazi moja ambalo kila kabila lilitambua kama vazi "letu". Hapo sijui umenipata mkuu?
 
Kuuliza si ujinga anayeuliza anataka kujua...

Ndugu wanajamvi, hoja na mchakato wa vazi la taifa umefikia wapi? What is the status...?
 
watu walishachukua chao mapema,maana ile kasi duh!!!sikutegemea ingekuwa hivi mpaka sasa.
 
Kuuliza si ujinga anayeuliza anataka kujua..
Ndugu wanajamvi, hoja na mchakato wa vazi la taifa umefikia wapi? What is the status...?
Nenda kaulize magamba wenzako kwasababu ndio waliokuwa wanaratibu zoezi zima sio uje na vithread vya ajabu hapa
 
Ungeuliza fungu la vazi la Taifa liliishia lini ungeeleweka. Huyu mwenye wizara ya Utamaduni na Michezo hakukuta kitu kama hicho mezani. Labda kama atabuni kitu hicho na yeye katika bajeti hii iliyopita mia kwa mia.
 
wamependekeza gwanda ndio rasmi la taifa , sasa wanasubuli kamati kuu ya magamba waidhinishe , wamekubali rangi 3
nyeusi, blue na kijani
 
wajiulize hayo mataifa yenye vazi la taifa waliyapataje?Kama uhuthamini utamaduni wako utategemea vipi kupata vazi la taifa,angalia magazeti ya sasa hivi yanajiita magazeti pendwa,na baadhi ya redio zinavyokazana kuua utamaduni wetu kumbuka taifa bila utamaduni ni sawa na kutembea uchi uliza sasa hivi kama tunao maofisa utamaduni na kama tunao je wanatumika kikamilifu
 
Najiuliza hivi mpaka tunafikiria/serikali inafikiria vazi la taifa kwa manufaaa ya nani? Je tumejiandaa? hebu angalia viongozi wetu wakuu wana nia ya kweli na vazi la Taifa? nenda Bungeni/Kwenye sherehe za kitaifa viongozi wanavaa vazi lolote toka Tanzania?(Batik/Khanga/Kitenge/Kaniki? Je bitambaa na mapambo yanayotumika kwenye mikutano ya kitaifa na kimataifa inayofanyika nchini (eg. AU/SADC/EAC Summits, Sullivan, WEF) tunatumia mali zilizotengenezwa Tanzania? Samani/furnitures maofisini husuani ofisi za serikali, Mikoba Delegates wanayopewaga kwenye mikutano je? So kabla Waziri (by then Dr. Nchimbi) hajaunda ile kamati uchwara ya kina Merinyo angefanya ka-utafiti kimya kimya ili akijiridhisha ndo atoke na kauli. Huyu waziri wa sasa sina imani nae maana sijui hata anafanya nini pale wizarani, ni msomi sana but ni kama amewekwa pale kupitisha muda tu.

2. Je tuna viwanda vya kutosha kuzalisha Vazi la Taifa (hapa serikali pia inapaswa kuwapa incentives wenye viwanda ili bei ya vitambaa/vazi ziwe affordable. Nawahakikishia waTZ kama tunawekeza kwenye sekta ya Viwanda ipasavyo TZ itatambulika duniani kwa vazi lake na tutauza nje sana bidhaa zetu ndani ya Afrika hata duniani.

NB: VAZI LA TAIFA KWENYE NCHI YA WAVAA MITUMBA "Malonya" ITABAKI KUWA HADITHI MILELE
 
Back
Top Bottom