Vazi la Taifa ni utapeli wa serikali?!!

kipumbwi

JF-Expert Member
Feb 3, 2015
3,057
8,724
"Hakuna vazi lolote duniani linaloitwa la taifa lililoundiwa tume. Hakuna! Kuwafanya Watanzania watumie muda wao kusaka vazi la taifa ni wild-goose chase (wehu) na diversionary tactic ili wasahau mambo muhimu yaliyowashinda watawala. Tusipotezeane muda wetu," Jenerali Ulimwengu
20240209_163242.jpg
NB- 2004-2005 mwanzoni mwa utawala wa Rais Kikwete kulifanyika huu utapeli, waziri akiwa Emanuel Nchimbi,baadae tena baada ya miaka 2011 ukarudiwa tena huu utapeli Waziri akiwa Dr Hellen Mkangara

Naona mambo yamerejea tena,sio utapeli wa serikali huu?!!
 
Wanatafuta mbinu za kuvuruga mjadala kuhusu umeme, gharama za maisha n.k
 
Ebu kwanza.....
Kwani hili vazi linaundiwa tume ya uchaguzi kwenye nchi gani wakuu...🤔
 
Cha ajabu hata wewe na mimi tungepata nafasi kama ya FA pale mjengoni lazima tungetetea 🤣,,

Pale wote bendera ufata upepo,, wana familia wale🤣,,

Siasa ni biashara nzuri sana hasa kwa nchi zetu hizi,, yaan ni upuuz mtupu vazi la taifa
 
Nimememsikia salma kikwete akichangia bungeni kuwa nguo anazovaa Rais Samia ndiyo ziwe vazi la Taifa. Yaani hata sisi wanaume tuvalishwe madera ,kweli akutukanae hakuchagulii tusi. Na kibaya zaidi hata wabunge wanaume na kengele zao zinaning'inia walimshangilia sana. Dhalim alituweza kweli kutuachia wajinga mjengoni
 
Nimememsikia salma kikwete akichangia bungeni kuwa nguo anazovaa Rais Samia ndiyo ziwe vazi la Taifa. Yaani hata sisi wanaume tuvalishwe madera ,kweli akutukanae hakuchagulii tusi. Na kibaya zaidi hata wabunge wanaume na kengele zao zinaning'inia walimshangilia sana. Dhalim alituweza kweli kutuachia wajinga mjengoni
Sisi tulitakiwa tuendelee kutaliwa
 

Nchi umeme unakatika katika kama mapigo ya moyo halafu watu na vichwa vyao vikubwa wanakaa kujipanga kupata vazi la taifa. Nchi ya ajabu sana.
 
Kuna watu wanatufanya Watanzania "mazuzu' kwa kujiondoa ufahamu...


Rwanda
iu


Nigeria
c2dabfeb18e4859f.png


Ni hivi

Kuna watu wamepofushwa na Ukweli

Ukweli ni UKWELI

Watu waliopofushwa hawajui Ukweli

Kimsingi, Mavazi ya kitaifa ni zaidi ya kitambaa. Vazi la Kitaifa linabeba Ukweli wa Kitamaduni na kuakisi urithi wa pamoja wa Taifa.
 
Back
Top Bottom