Hivi vazi la taifa limekwenda wapi?

Business za kina Nchimbi na wale jamaa wa Clouds..kina nani wale!?kaondoka na business yake..aliyepata u-boss hapo nae atakuja na lake!nonsense!
 
Nenda kaulize magamba wenzako kwasababu ndio waliokuwa wanaratibu zoezi zima sio uje na vithread vya ajabu hapa

Kwani wewe umejuaje kama mleta mada ni gamba?.......ameshasema kuuliza sio ujinga so wewe kama huna jibu ungepita kimya kimya!
 
ora eto rabola
Mhulize joseph kusaga sindio
m/kiti lakin mh. nchimbi, ebwana
nakukubali sana kwa kuogoza vizuri kila wizara kama wasiraaaaa.
 
Nakubali kabisa kuwa bila ya watz kupenda tamaduni zetu mbalimbali, hatutalivaa hilo vazi.
Tunalivaa ili iweje?
Mi naona ni ushabiki usiokuwa maana. Tulitakiwa tushikane kama taifa, tuwe na mapenzi na tanzania, tuijue tanzania maana yake nini, ujulikane msingi wa kuwepo tanzania, lengo, mtazamao, ndo labda, LABDA; tunaweza kufikiria swala la vazi.
Kwa sasa tanzania imeshikiliwa kwa plasta,mitazamo na mapenzi nchi kwa sasa ni ya kulazimishia kama kungoa jino, hamu ya vazi inatoka wapi?
Vazi kuonyesha nini?
Hata hao wabunifu, kuvuta hisia ili kubuni hilo vazi, sijui watapataje?
Halafu bajeti ilikuwa ya shughuli gani hasa?
 
Watu na project zao wameisha bana chao saizi wanatafyta ishu nyingine ndani ya serikali ya sisiem nchi yetu ni shamba la bibi tu.:sad:
 
Kuuliza si ujinga anayeuliza anataka kujua..
Ndugu wanajamvi, hoja na mchakato wa vazi la taifa umefikia wapi? What is the status...?

Tuwe wavumilivu. Infact wanafanya upembuzi yakinifu. We ulishaona wapi hadi yafanyike mashindano ndo lipatikane vazi la taifa? Huu ni usanii, miaka kama mitano au sita nyuma, liliwahi kufanyika shindano kama hilo na mshindi akapatikana, akapewa na zawadi, lakini leo tena wanaibuka wazee wa mishe wengine na shindano lile lile.
 
Tz shamba la bibi watu wamebuni jinsi ya kupiga hela tu,washapiga sasa wapo mbezi beach kwenye ghorofa wanapunga upepo tu!
 
Ndugu,

Tafadhali mnisaidie,
Jukwaani nimetinga,
Swali nauliza,

Liwapi vazi la Taifa????

Miezi kadhaa imepita,
Tangu kamati kuundwa,
Na kwa mbwembwe kunadiwa,

Liwapi vazi la taifa???

Nchimbi alizindua,
Kamati vazi la Taifa,
Na wajumbe kuteua,

Liwapi vazi la taifa???


Sugu akamchana,
Washikaji kuwajaza,
Swali nauliza,

Liwapi vazi la taifa?????
 
Teh teh teh!, ngoja wenyewe wakupe feedback, lol, Bongo kuna mengi, things are always not taken seriously
 
Mkuu umenikumbusha mbaaali kweli, aisee.
Hivi hii kitu kweli si ilikula hela yetu.
Yep, this iz Tizii. Kila kila kitu kinajiendesha chenyewe, safi sana!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom