Hivi ni Sahihi Kumpa Mpenzio Shikamoo?

Status
Not open for further replies.
Babra samahani natoka nje ya mada!
Unajua nakupenda hadi shetani anachukia? niko chini ya miguu yako (na macho nimeyafumba) naomba urudie lile jina lako la zamani, mwenzio napata shida kweli kukuzoea!!
(Ni ombi tu dada.....au ndo mambo ya mr anapendad lol kaizer vibaya hivyo-unadictate hadi jina!)

Ehee haya twambieni kwa nini hampeani shkamoo wewe na mwenzio?


kwa heshima yako nitalirudia dearest.....
mie bwana MJ1 nampaga tu "mambo baba mtoto"...au vipi nawamambia "mambo fulani"........nahic inamtosha bwana..
 
Wakuu habari zenu!
Hili jambo limekuwa likinitatiza sana tena sana...Utakuta binti au mwanamke aliyeolewa anamwamkia mume wake eti kwakuwa mwaume ni mkubwa kiumri kuliko mkewe,mimi hii sielewi kabisa..What I know mke na mume ni mtu na rafiki yake tena ndio best friends na kwaninavyofahamu maana shikamoo naona haistahili kufanyika kwa wapendanao..mimi kwangu naona haina maana kabisa kumpa shikamoo mumeo hata kama amekuzidi miaka 40! Lakini kila kukicha nasikia watu wakiwaamkia waume zao..Jamani hivi hii imekaaje?je ni sawa?

Mmmmh makubwa kumpa mumeo shikamoosijaolewa bado lakini hata kama nikipata mume ana miaka kumi kunizidia bado sijampa shikamoo. haisound poa saaana kwa kweli
 
shikamoo [nashika miguu yako] Inasemekana asili ya neno hili heshima aliyopewa mwenye [mwinyi] katika maeneo mbalimbali katika ukanda wa pwani. Lakini pia neno hili lilikuwa likitumiwa kwa watumwa kumuamkia bwana [mmiliki] Ingawa mimi ni mswahili lakini neno hili siku zote limekuwa likinipa kigugumizi kulitumia ingawa hupokea kwa kusema marhaba [ahsante] Pengine wataalamu wa kiswahili wanaweza kutuelimisha zaidi kuhusu hili
 
Waacheni wenzi watumia salamu wapendayo, ikiwa wanaifurahia.....iwe shikamoo, mambo switi, vipi dia, laazizi hujambo, za asubuhi baba toni, umeamaje mpenzi, sema mahabuba n.k.
 
Kwa mtazamo wangu kwa wapenzi si lazima kupeana shikamoo.
Lakini mara nyingi hii hutumiwa kama namna ya kumwonyesha anayeamkiwa kuwa mimi bado ni mdogo au dogo dogo. Na haswa mara nyingi hutumika ki biashara sana.
 
aaa jamani mie mwenzenu sikubali mpaka mr anisalimie yeye akiamka ........na asiponisalimia lazima nimuulize kulikoni kukurupuka bila salaam

kweli haina formula na sikumbuki kutumia shikamoo bado ............but ikiwa mpenzi wako atafurahia y not? afterall tunasalimia kuonyesha heshima tu ....so hata shikamoo poa tu
 
Yaani kila siku mnaanikiana vidudu vyenu kweupee na kila mmoja anaona cha mwenzie na kubingirika misarakasi ya kila aina ! Halafu asubuhi usikie kashikamooo mie ntamjibu shikameee
 
Do! sio heshima kumpa shikamoo!! na je wale waliooa wanawake waliowazidi umri watatoa shikamoo wa wake zao? au mke/mume tu ndio shikamoo hebu tulijadili kwa undani hili mume/mke shikamoo inakuja...
 
du siwezi kuamka asubuhi na kumpa mme wangu shikamoo ..
eeeh hapana haiji moyoni mwangu
nitasema tu sweet/or mme wangu umeamkaje
niliona dada mmoja, mmewe wanakaribiana kabisa kiumri eti kila siku anamwamkia shikamoo baba /shikamoo mme wangu
 

niliona dada mmoja, mmewe wanakaribiana kabisa kiumri eti kila siku anamwamkia shikamoo baba /shikamoo mme wangu
Si wanaifurahia? Hakuna kosa kusalimiana salamu ya aina yoyote. Hakuna fomula ya jinsi ya kuishi na mwenzi wako. Kila couple inaishi kivyakevyake.
 
Yaani kila siku mnaanikiana vidudu vyenu kweupee na kila mmoja anaona cha mwenzie na kubingirika misarakasi ya kila aina ! Halafu asubuhi usikie kashikamooo mie ntamjibu shikameee
duh!!!! Kimbweka wewe, unalilia ban eeh
 
du siwezi kuamka asubuhi na kumpa mme wangu shikamoo ..
eeeh hapana haiji moyoni mwangu
nitasema tu sweet/or mme wangu umeamkaje
niliona dada mmoja, mmewe wanakaribiana kabisa kiumri eti kila siku anamwamkia shikamoo baba /shikamoo mme wangu

yani humu tutajua wote wenye tabia njema na mbaya
ukisema sweet umeamkaje shaikamoo unapungukiwa nn?
 
usiponiamkia nakusaidia kufungasha virago kukurudisha kwenu!! mbona wengine wakiamka wanabusiana? kwa sisi wengine kale kashikamoo kaasubuhi kana utamu kama wa busu hivi!

Mmh basi kazi ipo!lakini wewe sikushangai ni Mzee wa Kijiji hivyo ni muhimu kudumisha mila hata hivyo nakupongeza kwa ukarimu wa kusaidia kupaki virago.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom