Tabia ya mke kusambaza habari kutoka ndani kwake, je ni sahihi?

Pleasepast

JF-Expert Member
May 30, 2023
325
454
Habari za siku wapendwa.

Kwenye maisha watu tunatofautiana sasa wapo watu wengine wana ile tabia ya kusambaza jambo mpaka kwa watu ambao hawahusiki kabisa je.? Ni njia gani itumike kuishi nao au kuwathibiti yani iko hivi tuseme unaishi na mke wako au mume wako lakini ikitokea mmepishana kauli kidogo tu tena mkiwa mbali mbali sasa ile labda unamtumia sms ambayo ni ya ugomvi na wote mnatumiana lakini yeye anachambua zile ambazo zina mgusa kisha ana forward kwa ndugu zake wote unakuta mmekwazana kawaida tu lakini hakujibu io sms uliyotuma kwake lakini baada ya dakika 20 unapokea majibu ya io sms kutoka kwa dada yake mara ghafla kwa kaka yake ghafla tena kutoka kwa mama yake na zote zinatoa jibu la sms ambayo ulimtumia yeye hivi wakuu hii kitaalamu imekaaje na mara nyingi ni wanawake ndio wanakuwa hivi sasa uyu mke utaishi nae vipi.

Naomba kuwasilisha tujadili hii tabia na wengine wajue jinsi ya ku handle hii issue.
 
Ni njia gani itumike kuishi nao au kuwathibiti yani iko hivi tuseme unaishi na mke wako au mume wako lakini ikitokea mmepishana kauli kidogo tu tena mkiwa mbali mbali sasa ile labda unamtumia sms ambayo ni ya ugomvi na wote mnatumiana lakini yeye anachambua zile ambazo zina mgusa kisha ana forward kwa ndugu zake wote
That is how they are
Na madishi yakiyumba zaidi anaweza kuongea na simu kwa sauti kubwa mpaka majirani wasikie kwamba unachongewa kwa ndugu zake
 
Usirushiane maneno na mke wako/mume wako kwenye sms. Sms huwa zinatunza kumbukumbu mbaya sana.
Kama kuna tatizo mpigie simu au subiri urudi nyumbani.
Hata simu asimpigie, akishajua kakosea simu ikipigwa anarecord. Na bahati mbaya sana mdomo husema zaidi ya mikono.

Amsubirie nyumbani wagombane wee, mpaka wamalizane.
 
Hata simu asimpigie, akishajua kakosea simu ikipigwa anarecord. Na bahati mbaya sana mdomo husema zaidi ya mikono.

Amsubirie nyumbani wagombane wee, mpaka wamalizane.
Hapo Umenena vyema ni vizuri mtu asubilie arudi nyumbani iwe ana kwa ana safi kabisa.
 
Kuna baadhi ya makabila haya ni mambo ya kawaida, ni maisha waliyokulia kwenye makuuzi yao na ni jambo la kawaida.

Unapooa kabila tofauti jijenge kisaikolojia kutegemea tabia zao wanazosifika kuwa nazo, ukilipenda boga usichukie maua yake
 
Kuna baadhi ya makabila haya ni mambo ya kawaida ndio maana huwa tunasisitiza unapooa jiandae na tabia kama hizo, ukilipenda boga usichukie maua yake
Hakika mkuu sasa kwa msaada wa wadau unaweza kuweka sample kidogo za ayo makabila watu wawe aware
 
Huyo Mke bado hajatoka kwenye himaya ya familia yao, na inawezekana wewe kwa aina ya matusi na kejeri unazompa ndio zinazomfanya aone bado hajaingia kwenye himaya ya familia yenu, hivyo anatafuta relief kutoka familia yao. mfanye aone nyinyi ni familia moja na mambo yenu yaishie kwenye kuta za nyumba yenu

Btw... punguza kumtukana matusi ya kumdhalilisha kikubwa muheshimu aone wewe ndio ndio kila kitu kwake.
 
Kama ni maratizo ya kawaida ni vizuri kujadiliwa ndani ya ndoa na wanandoa wenyewe, na siyo kushirikisha ndugu au kujibizana kwenye simu....
 
Huyo Mke bado hajatoka kwenye himaya ya familia yao, na inawezekana wewe kwa aina ya matusi na kejeri unazompa ndio zinazomfanya aone bado hajaingia kwenye himaya ya familia yenu, hivyo anatafuta relief kutoka familia yao. mfanye aone nyinyi ni familia moja na mambo yenu yaishie kwenye kuta za nyumba yenu

Btw... punguza kumtukana matusi ya kumdhalilisha kikubwa muheshimu aone wewe ndio ndio kila kitu kwake.
Hakika huu ni ushauri mzuri sana.
 
Back
Top Bottom