Hivi ni Sahihi Kumpa Mpenzio Shikamoo?

Status
Not open for further replies.
kusema ukweli ukweli sijawahi kumuamkia mme wangu shikamoo,tukiamka asubuhi namuuliza umeamkaje ......
Mie nikiwahi kuamka namuuliza mwandani, hujambo bibie? Si unajua tena ikirudi ndio hivyo = sijambo, shikamoo! (haiwezi kuwa, sijambo, hujambo na wewe)! Kwi kwi kwi! Inaweza kukupa taabu lkn ni vijimbambo tu!
 
acha udaku!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Naam! ndiyo maana yake haswa! ila sijui maana ya marhaba! nafikiri ni jibu lenye dharau au la kudhalilisha pia.
Kusema kweli kwa ufahamu wa historia jinsi kiswahili kilivyo toka kwa mabwana wa utumwa ingestahili hii salamu iwe imeshajadiliwa na kukubaliana kuibadilisha kabisaa. Ingelifaa kumsalimia unayemheshimu kama baba, mama, mjomba nk. kwa kutumia neno Heshima yako Mzee, au Heshima yako Baba. Nadhani "its long overdue"!
 
usiponiamkia nakusaidia kufungasha virago kukurudisha kwenu!! mbona wengine wakiamka wanabusiana? kwa sisi wengine kale kashikamoo kaasubuhi kana utamu kama wa busu hivi!
 
hamna sbb ya kumsalimia mumeo/mpenzi.mie mtu akishakua mpenzi no shikamoo.naona haina ladha kabisa.
 
Kwani zinatoka moyoni basi? kwanza wameshabadili siku hizi sio shikamoo ila 'shikaoo'
 
Wakuu habari zenu!
Hili jambo limekuwa likinitatiza sana tena sana...Utakuta binti au mwanamke aliyeolewa anamwamkia mume wake eti kwakuwa mwaume ni mkubwa kiumri kuliko mkewe,mimi hii sielewi kabisa..What I know mke na mume ni mtu na rafiki yake tena ndio best friends na kwaninavyofahamu maana shikamoo naona haistahili kufanyika kwa wapendanao..mimi kwangu naona haina maana kabisa kumpa shikamoo mumeo hata kama amekuzidi miaka 40! Lakini kila kukicha nasikia watu wakiwaamkia waume zao..Jamani hivi hii imekaaje?je ni sawa?
hii salamu ni noma kwanza mimi siifagilii kabisa hata kwa mtu aliyenizidi umri naona utumwa kumwamkia,mambo haya shkamoo,shkamoo hayafai kipindi hiki ni bora kabisa wataalam wa kiswahili watoe salamu ingine,kina mzee mwnkjj watatusaidia mimi niliacha siku nyingi kutoa shkamoo aisee nisiseme uongo,halafu iweje mtu mnalala kitanda kimoja mnaamka mnachangia mawazo yote ndani ya nyumba then eti akiamka akupe shkamoo kivipi?huu ni utumwa na haiko sawa kabisa na haki za bin adamu, kwa ujumla hiyo salamu imepitwa na wakati.
 
just imagine.... mmeshtuka usingizini 11 alfajiri na mnataka kucheza kale ka mchezo ka baba na mama, utaanza kwanza shikamoo au mtacheza kwanza? maana mkimaliza hilo zoezi la alfajiri ni bafuni na kuwahi kibaruani tena!
 
just imagine.... mmeshtuka usingizini 11 alfajiri na mnataka kucheza kale ka mchezo ka baba na mama, utaanza kwanza shikamoo au mtacheza kwanza? maana mkimaliza hilo zoezi la alfajiri ni bafuni na kuwahi kibaruani tena!

utasema shkamoo huku ukiendelea na mchezo :d hahaha

kusalimiana si lazima shikamoo......kuna wengine wana `umeamkaje mpenzi`, `za kuamka?` `assalaam aleykum`, `bwana asifiwe` n.k

sasa hapa Gender sensitive umekusudia Shikamoo tu au mpaka hizi nyengine zina utata kumpa mumeo?
 
Nyie watu hebu acheni matani loh imagine jibaba lenye kimwana- linakunjwa hadi linalia lia na kamasi tele- kisha asubuhi anaamkiwa ah anaipokeaje hiyo 'niko chini ya miguu yako?' ah wala haipo bwana.
 
mwanajamii.......labda hicho kimwana kilikuwa chini ya miguu yake kwenye usiku wake ....teh teh teh
 
mwanajamii.......labda hicho kimwana kilikuwa chini ya miguu yake kwenye usiku wake ....teh teh teh
Gaijin lol inawezeka na maana mapenzi ni kitu cha ajabu sana.

Haya na kwa wale majimama yenye ving'asti- imagini mmama wa haja anapelekeshwa puta na kiboy chenye umri kama mwanaye- yaani anashughulikiwa hadi yanamtoka ya kumtoka- asubuhi kiboy kinaanza shikamoo ah--- labda kama ni ya utani na mama aitikie marhabaa mpenzi but not serious kwa kweli.

Mie mwenzangu alianzaga hayo ya kudai nimwamkie- sikumbishia wala nini ila kwa kuwa wakati ananitokea hakuwahi kuizungumzia na maisha yakaendelea nilimshangaa alipoanza baada ya ndoa - nilikuwa nashikwa na kigugumizi wala haitoki mdomoni- Hadi akazoea akaona haina dili.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom