tindikalikali
JF-Expert Member
- Jan 14, 2011
- 4,855
- 1,117
Mara nyingi watu wanaposhindwa kusimama katika hoja huwa wanaanza kuibua viroja wakidhani zinaweza kuwavusha katika jambo husika. Vituko huwa vinaanza pale mtu anaposimama na kutaka kuaminisha watu kwa hivyo viroja kwamba yupo sahihi, watu wa aina hii huweka facts pembeni na kuongozwa na hisia tu!
Mengi yamesemwa na yanaendelea kusemwa baada ya utolewaji wa hizi tuzo usiku wa jana!! Viroja ni vingi ila mi nitavisema vichache..
1. Eti Alikiba hawezi kuwa mtumbuizaji bora zaidi ya Diamond;
Hapa nilijipa muda kidogo wa kujiuliza nini maana ya kutumbuiza, mwisho nikagundua kuwa wengi wanaolalamika wanafikiri utumbuizaji bora ni kukata mauno jukwaani, hata ingekuwa ni kukata mauno basi washindi wangekuwa ni Bella au Nyoshi el sadaat, au kama kigezo ni hicho tu basi tuzo zingeenda kwa shilole kila mwaka!!
2. Eti watu wana chuki dhidi ya Diamond
Hapa ilibidi nicheke kwanza, hivi usipompigia msanii kura maana yake unamchukia si ndiyo? Sasa kama ni hivyo mbona wao hawajampigia kura Kiba, je wanamchukia? Mimi niwaulize kwanini mnamchukia Kiba kwa kiwango hicho je mna malengo gani?
3. Kwamba mtunzi bora alistahili kuwa Barnaba!
Hapa wameenda mbali na kudai eti Barnaba katunga nyimbo nyingi sana kuanzia nyimbo zake, za vannesa mpaka za Rubby!! Swali ni kwamba je hizo ndizo zilizokuwa zinashindanishwa na utunzi uliotukuka wa mashahiri ya wimbo wa Mwana?
4. Kwamba wao wanadeal na tuzo za kimataifa tu, hizi local hawazitaki!!
Huu ni utani wa aina nyingine sasa, mtu unajiuliza international maana yake nini? Je kuimba na Wanaija ndiyo u international wanaousema? Hata kama ni hivyo, hili lina uhusiano gani na tuzo za jana? Kiroja zaidi ni pale hao hao mashabiki wanaoponda tuzo za nyumbani pamoja na mashabiki wa kiba, ndiyo hao hao wanataka tuwapigie kura kwenye tuzo za MTV, yani unaponda watu na kuwatukana then wapige kura ili ushinde na uwatukane zaidi? Kwa mimi siwezi kusupport hili na kura yangu hawawezi kuipata!
5. Kwamba kuna mkakakati wa Clouds wa kumshusha Diamond na kumpandisha Kiba!!
Hapa mwenye kufikiri sawasawa unajiuliza Kiba anapandishwa kwenda wapi? Alikiba wa Cinderela, Run dunia, Dushelele, My everything, Far away na Nakshi nakshi anapandishwa kwa kumshusha Diamond, utani mwingine huu!! Inawezekana kweli anashushwa lakini yeye alipopata tuzo 7 mwaka jana nani alikuwa anashushwa ili yeye apande?
6. Kwamba tuzo za Alikiba alizopata ni 5 ni siyo 6!!
Hapa napo kuna viroja, maana wanaopinga tuzo ya collaboration kuhesabiwa kama tuzo ya Kiba ndiyo hao hao wanaojumuisha tuzo ya "muziki gani" kufanya Diamond awe na tuzo 7 mwaka jana!
7. Eti wimbo mmoja tu unampa tuzo zote hizo?
Sasa hawa sijui walitaka apewe tuzo kwa nyimbo ngapi? Sasa sijui wamezeeka au sijui wamekula maharage ya wapi? Maana wasingekuwa wavivu wangefuatilia tuzo nyingine duniani zinavyoenda, wangejua hata "Some one like you" ya Adele ilimpa tuzo ngapi, na hata Blank space ya Taylor Swift ilimpa tuzo ngapi pia!!
NB; Malalamiko huwa hayakosekani popote, ila tunapolalamika angalau malalamiko yawe na mashiko basi! Lazima tujue kuwa wimbo/msanii akiwa nominated maana yake kuna uwezekano akashinda, sasa hapo hakuna ajabu katika walioshinda jana!!
Kabla ya kuja na maswali ya je alistahili kushinda, tungeuliza kwanza je alistahili kuwa nominated? Kama alistahili kuwa katika category husika basi anastahili kushinda!! Kuna watu walifikiri zile kura ni mchezo wa kuigiza labda, maana kama unaelewa nguvu ya kura huwezi kuja na maneno kama "wamemnyima tuzo", labda useme "nimemnyima/tumemnyima"...mimi kwa upande wangu nimemnyima tuzo Diamond na nimempa Kiba, pia nimemnyima Bella..na si kwamba Bella hakustahili hapana, kuwa category moja na Kiba ndiko kumemnyima kura yangu!!
Mwisho nimpe pongezi kwa mara nyingine Alikiba kwa kushinda katika category 6 kati ya 7 alizokuwa nominated