Hivi ndivyo viroja vya wanaojiita mashabiki wa Diamond kuhusu KTMA

Baada ya KTMA kutoa tamko hao

Mie nikizani mtakua mnamuongelea mnaemoenda zaidi ya Diamond

Ila nazidi kuamini mnamzimia Diamond hadi chuki zinawajaa na nyimbo zake mbacheza na kusikiliza...lol
 
Kwanza wakome kumshindanisha king Kiba wetu na muimba taarab, asubiri mwakani apambane na mzee Yusuph huko.

et bumbum nayo ipo kwenye MTV awards wametumia kigezo gani? au kwasababu kamshirikisha iyanyaa haki ya wallah bora hata nasema nawe mara 10000k kuliko "bumbum":eek::eek::eek::eek::eek:
 
et bumbum nayo ipo kwenye MTV awards wametumia kigezo gani? au kwasababu kamshirikisha iyanyaa haki ya wallah bora hata nasema nawe mara 10000k kuliko "bumbum":eek::eek::eek::eek::eek:

Mkuu yule kinachombeba ni collabo tu, ndio maana anawang'ang'ania watu wa magharibi maana anajua asipofanya nao kazi ATAPIGWA TU, hana jinsi kwakweli.
 
jamani hakuna tuzo ambazo hazina lawama duniani hata ronado na messi mmoja wapo anapopewa tuzo lazma kuwe na lawama hiyo yote inasababishwa na mashabiki KING KIBAAAAAAAA miaka 10000k
 
hata domo na 20% walivyochukua malalamishi yalikuwepo pia msanii kama belle9 alilamika sana xo is normal KING KIBAAA
 
+tuache hizo # zingine naomba kujua hii # 5, ina maana mkuu wewe hadi leo huamini kama Diamond ni msanii wa kimataifa?

+au wewe hili neno intranational linakupa shida mkuu? Maana naona nyinyi mashabiki wa Kiba ikiongelewa Chibu ni wa kimataifa huwa mnataja Nigeria tu pekeake mnasahau kwa juhudi zake kijana wa watu anajulikana Ghana, Congo na kwingineko au hayo sio mataifa?









+mtoa mada ungeonekana ni shabiki wa kweli wa musiki wa bongo ungempa pongezi kijana kupiga hatua kimataifa.


+Kwa hiyo hapo kwenye mstari anaetukana watu baada ya kupata tuzo ni Diamond au mashabiki?

+kama kweli wamekutukana haya sawa, sasa swali ni je aliyekuomba kura ni Diamond au mashabiki?

+Hapa wewe kama kweli ni shabiki wa kweli wa muziki wa bongo unamsikiliza nani Diamond au mashabi. Au huna msimamo binafsi unaongozwa na mihemko ya mashabiki?

+kama wewe ni mshabiki wa kweli wa muziki bongo ni aibu kubwa kumpigia kura msanii wa nje eti tu upo katika vita na mashabiki wa yule msanii aliyekua nominated. Kweli hii inatokea bongo hata wenzetu watatushangaa.

Well said. By the way nashangaa sana watu wamekazana eti kura zao ndio zimemshindisha Kiba. No one seems to mention that votes from the public only account for 40% of the winning, judges have 60% of the decision.

So you all thinking your votes were the 100%, now think again. You now understand why KTMA wametoa hilo tamko kuhusu makosa yaliyo tokea. Kama ingekuwa 100% your votes then how come kuwe na makosa?
 
Well said. By the way nashangaa sana watu wamekazana eti kura zao ndio zimemshindisha Kiba. No one seems to mention that votes from the public only account for 40% of the winning, judges have 60% of the decision.

So you all thinking your votes were the 100%, now think again. You now understand why KTMA wametoa hilo tamko kuhusu makosa yaliyo tokea. Kama ingekuwa 100% your votes then how come kuwe na makosa?

makosa gani?
 
Nipo na kiba hapa pembeni ananiuliza hivi mbona ninazosifa ambazo mimi mwenyewe sizijui ????? ( mi namjibu ngoja miaka 30 utakayokuwa umempita "ambaye kwa wakati huo DIAMOND atakuwa kastaafu" ndo utawajua kama walikuwa wanamaanisha au )
 
Nipo na kiba hapa pembeni ananiuliza hivi mbona ninazosifa ambazo mimi mwenyewe sizijui ????? ( mi namjibu ngoja miaka 30 utakayokuwa umempita "ambaye kwa wakati huo DIAMOND atakuwa kastaafu" ndo utawajua kama walikuwa wanamaanisha au )

umeandika nini sasa? Kiroja kingine hiki!!
 
diamond and ali kiba must dual imediately for the sake of music fans
 
thread nyingi sana zitafunguliwa kipindi hiki na wengine sijui mlikua wapi au ndio ushabiki wa msimu kwenye raha tu? au pengine ni hizi id mpya? teh teh teh

Platnumz sio wa kushindanishwa na huyo mzigo sasa ifike wakati diamond atoe tamko ili wazembe waache kula nyuma ya mgongo wake am sure kama sio hili bifu kiba asingepata hata tuzo moja. Am out!!!!
 
Mara nyingi watu wanaposhindwa kusimama katika hoja huwa wanaanza kuibua viroja wakidhani zinaweza kuwavusha katika jambo husika. Vituko huwa vinaanza pale mtu anaposimama na kutaka kuaminisha watu kwa hivyo viroja kwamba yupo sahihi, watu wa aina hii huweka facts pembeni na kuongozwa na hisia tu!!

Mengi yamesemwa na yanaendelea kusemwa baada ya utolewaji wa hizi tuzo usiku wa jana!! Viroja ni vingi ila mi nitavisema vichache..

1. Eti Alikiba hawezi kuwa mtumbuizaji bora zaidi ya Diamond.
Hapa nilijipa muda kidogo wa kujiuliza nini maana ya kutumbuiza, mwisho nikagundua kuwa wengi wanaolalamika wanafikiri utumbuizaji bora ni kukata mauno jukwaani, hata ingekuwa ni kukata mauno basi washindi wangekuwa ni Bella au Nyoshi el sadaat, au kama kigezo ni hicho tu basi tuzo zingeenda kwa shilole kila mwaka!!

2. Eti watu wana chuki dhidi ya Diamond!!
Hapa ilibidi nicheke kwanza, hivi usipompigia msanii kura maana yake unamchukia si ndiyo? Sasa kama ni hivyo mbona wao hawajampigia kura Kiba, je wanamchukia? Mimi niwaulize kwanini mnamchukia Kiba kwa kiwango hicho je mna malengo gani?

3. Kwamba mtunzi bora alistahili kuwa Barnaba!!
Hapa wameenda mbali na kudai eti Barnaba katunga nyimbo nyingi sana kuanzia nyimbo zake, za vannesa mpaka za Rubby!! Swali ni kwamba je hizo ndizo zilizokuwa zinashindanishwa na utunzi uliotukuka wa mashahiri ya wimbo wa Mwana?

4. Kwamba wao wanadeal na tuzo za kimataifa tu, hizi local hawazitaki!!
Huu ni utani wa aina nyingine sasa, mtu unajiuliza international maana yake nini? Je kuimba na Wanaija ndiyo u international wanaousema? Hata kama ni hivyo, hili lina uhusiano gani na tuzo za jana? Kiroja zaidi ni pale hao hao mashabiki wanaoponda tuzo za nyumbani pamoja na mashabiki wa kiba, ndiyo hao hao wanataka tuwapigie kura kwenye tuzo za MTV, yani unaponda watu na kuwatukana then wapige kura ili ushinde na uwatukane zaidi? Kwa mimi siwezi kusupport hili na kura yangu hawawezi kuipata!

5. Kwamba kuna mkakakati wa Clouds wa kumshusha Diamond na kumpandisha Kiba!!
Hapa mwenye kufikiri sawasawa unajiuliza Kiba anapandishwa kwenda wapi? Alikiba wa Cinderela, Run dunia, Dushelele, My everything, Far away na Nakshi nakshi anapandishwa kwa kumshusha Diamond, utani mwingine huu!! Inawezekana kweli anashushwa lakini yeye alipopata tuzo 7 mwaka jana nani alikuwa anashushwa ili yeye apande?

6. Kwamba tuzo za Alikiba alizopata ni 5 ni siyo 6!!
Hapa napo kuna viroja, maana wanaopinga tuzo ya collaboration kuhesabiwa kama tuzo ya Kiba ndiyo hao hao wanaojumuisha tuzo ya "muziki gani" kufanya Diamond awe na tuzo 7 mwaka jana!

7. Eti wimbo mmoja tu unampa tuzo zote hizo?
Sasa hawa sijui walitaka apewe tuzo kwa nyimbo ngapi? Sasa sijui wamezeeka au sijui wamekula maharage ya wapi? Maana wasingekuwa wavivu wangefuatilia tuzo nyingine duniani zinavyoenda, wangejua hata "Some one like you" ya Adele ilimpa tuzo ngapi, na hata Blank space ya Taylor Swift ilimpa tuzo ngapi pia!!

NB; Malalamiko huwa hayakosekani popote, ila tunapolalamika angalau malalamiko yawe na mashiko basi! Lazima tujue kuwa wimbo/msanii akiwa nominated maana yake kuna uwezekano akashinda, sasa hapo hakuna ajabu katika walioshinda jana!! Kabla ya kuja na maswali ya je alistahili kushinda, tungeuliza kwanza je alistahili kuwa nominated? Kama alistahili kuwa katika category husika basi anastahili kushinda!! Kuna watu walifikiri zile kura ni mchezo wa kuigiza labda, maana kama unaelewa nguvu ya kura huwezi kuja na maneno kama "wamemnyima tuzo", labda useme "nimemnyima/tumemnyima"...mimi kwa upande wangu nimemnyima tuzo Diamond na nimempa Kiba, pia nimemnyima Bella..na si kwamba Bella hakustahili hapana, kuwa category moja na Kiba ndiko kumemnyima kura yangu!!

Mwisho nimpe pongezi kwa mara nyingine Alikiba kwa kushinda katika category 6 kati ya 7 alizokuwa nominated
Hoja kwa hoja.
Asante TEAM KIBA 4 REAL.
 
acha ujinga, sasa hapo umetoa hoja gani hizo? umenichekesha sana kwa jinsi ulivyo argue as if unajua sana, kumbe ni pumba tupu, Dai hafananishwi na hao wasanii wenu wadogo wadogo, uyo Ally Kiba nani anamjua nje ya Tanzania..? Dai sio size yenu.

Kama Ally Kiba hajulikani nje ya Tanzania ule wimbo wa ONE 8 ambao walishiriki wanamziki nguri kama R.KELLY, FALLY IPUPA, 2FACE ilikuwaje KIBA akawemo umo? kwa Tanzania msanii anae heshimika na kujulikana nchi nyingi na kufanya korabo nchi nyiingi ni AY kitu ambacho huyo DOMO hamfikii AY hata robo.
 
thread nyingi sana zitafunguliwa kipindi hiki na wengine sijui mlikua wapi au ndio ushabiki wa msimu kwenye raha tu? au pengine ni hizi id mpya? teh teh teh

Platnumz sio wa kushindanishwa na huyo mzigo sasa ifike wakati diamond atoe tamko ili wazembe waache kula nyuma ya mgongo wake am sure kama sio hili bifu kiba asingepata hata tuzo moja. Am out!!!!

Bifu lipi liilomshusha Diamond likampandisha KIBA?? yaani bado unaendelea na hoja za kitoto. tambua kuwa hiki mnachokifanya ndio kwanza kinazidi kumdidimiza huyo Diamond na ninakuhakikishia kama mtaendelea hivi huyo DOMO atapotea kabisa kwani msanii ujengwa na washabiki.
 
acha ujinga, sasa hapo umetoa hoja gani hizo? umenichekesha sana kwa jinsi ulivyo argue as if unajua sana, kumbe ni pumba tupu, Dai hafananishwi na hao wasanii wenu wadogo wadogo, uyo Ally Kiba nani anamjua nje ya Tanzania..? Dai sio size yenu.

Dimond ana ukubwagani katika game ya bongo au ndo mahaba niue yakwenu,mkiambiwa mashabiki wa bwana mdogo hamjui muziki na hamjitambui mshabikia nini mnarusha matusi
 
Back
Top Bottom