Wasanii kutohudhuria tuzo za TMA ni kuzidharau?

black abdu

Senior Member
Dec 2, 2022
152
208
Usiku wa Jumamosi ya tarehe 29 mwezi Aprili ulikuwa usiku wa kutolewa tuzo za Muziki Tanzania zilizoandaliwa na kuratibiwa na Wizara inayohusika na Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa.

Kwa heshima ya Tuzo hizi waziri wa wizara hii na viongozi wa baraza la Sanaa walikuwepo ukumbini. Hata hivyo wengi wa wasanii wenye majina makubwa nchini hawakuhudhuria shughuli za utoaji wa tuzo hizo. Ilisemwa kuwa Diamond na Zuchu walikuwa nje ya nchi kikazi, Nandy na Bill Nas walikuwa na shughuli ya ubatizo wa mtoto wao na Barnaba (kama nilisikia vema) alikuwa hospitali. Kama sikosei pia, Kiba alikuwa na show Arusha.

Hata hivyo bado kuna wakina Harmonize, Ben Pol, Jux, Darasa n.k, hata wakongwe wa bongo flava kama Jide, AY, Dully, Banana, TID na wengineo, orodha ni ndefu. Kwa wale walioshonda walipokelewa na wawakilishi.

Kala alikuwepo ukimbini pamoja na wasanii wa Singeli ambao walionekana kuufurahia ule wakati, na wengine waliokuwepo ninwasanii wapya, waliokuwa kwenye orodha ya wateuliwa kupokea tuzo.

Swali langu ni, je, wasanii wote hawa walikuwa na dharura zilizowakosesha kuhudhuria? Wote? Labda inawezekana, ila ninahisi kuna dharau na kujiona wao ni bora kuliko tuzo hizi.

Nasema ni dharau kwa sababu wasanii hawa huhudhuria tuzo zinzotolewa nchi zingine wanapokuwa kwenye orodha ya wateuliwa wa kupokea tuzo.

Inawezekana tuzo zetu hazina hadhi kama za Kenya, Nigeria na Marekani lakini hizi ni zetu na hatupaswi kudharau chetu! Nawaza ile shughuli ingependeza namna gani kama pale ukumbini wangekuwepo wote hao na wakakaa pamoja kama tunavyoona kwa wasanii wa nchi zingine.

Tulichukulia mfano wa tuzo kama za Grammy, wanasanii husitisha hata ziara zao za kimuziki ili kuhudhuria na hufika ukumbini hata kama hawapo kwenye orodha ya wanaogombeq tuzo. Lakini huku kwetu mtu asipokuwepo kwenye orodha hiyo basi anakuwa kama adui wa hizo tuzo! Kwani tuna shida gani?

Binafsi nilifurahi kusikia Muheshimiwa Rais akisema tuzo hizi zingerejea na Wizara husika kubeba jukumu kuziandaa, sasa kwa nini wasanii wetu wasijali na kuheshimu angalao jitihada hizi na kuthamini chetu cha nyumbani?
 
Zile sio tuzo.

Kwanza kuna malalamiko mengi tunayasikia kwa watu waliopata tuzo kudhulumiwa pesa zao.
 
Ili mambo yako yaende, kwenye zamu hii lazima uwe mnafiq.....
Leo nimemsikiliza Kitilya, nikajikuta nawaza sana aiseeee....
 
Back
Top Bottom