Hivi ndivyo viroja vya wanaojiita mashabiki wa Diamond kuhusu KTMA

tindikalikali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,855
1,117
Mara nyingi watu wanaposhindwa kusimama katika hoja huwa wanaanza kuibua viroja wakidhani zinaweza kuwavusha katika jambo husika. Vituko huwa vinaanza pale mtu anaposimama na kutaka kuaminisha watu kwa hivyo viroja kwamba yupo sahihi, watu wa aina hii huweka facts pembeni na kuongozwa na hisia tu!

Mengi yamesemwa na yanaendelea kusemwa baada ya utolewaji wa hizi tuzo usiku wa jana!! Viroja ni vingi ila mi nitavisema vichache..

1. Eti Alikiba hawezi kuwa mtumbuizaji bora zaidi ya Diamond;
Hapa nilijipa muda kidogo wa kujiuliza nini maana ya kutumbuiza, mwisho nikagundua kuwa wengi wanaolalamika wanafikiri utumbuizaji bora ni kukata mauno jukwaani, hata ingekuwa ni kukata mauno basi washindi wangekuwa ni Bella au Nyoshi el sadaat, au kama kigezo ni hicho tu basi tuzo zingeenda kwa shilole kila mwaka!!

2. Eti watu wana chuki dhidi ya Diamond
Hapa ilibidi nicheke kwanza, hivi usipompigia msanii kura maana yake unamchukia si ndiyo? Sasa kama ni hivyo mbona wao hawajampigia kura Kiba, je wanamchukia? Mimi niwaulize kwanini mnamchukia Kiba kwa kiwango hicho je mna malengo gani?

3. Kwamba mtunzi bora alistahili kuwa Barnaba!
Hapa wameenda mbali na kudai eti Barnaba katunga nyimbo nyingi sana kuanzia nyimbo zake, za vannesa mpaka za Rubby!! Swali ni kwamba je hizo ndizo zilizokuwa zinashindanishwa na utunzi uliotukuka wa mashahiri ya wimbo wa Mwana?

4. Kwamba wao wanadeal na tuzo za kimataifa tu, hizi local hawazitaki!!
Huu ni utani wa aina nyingine sasa, mtu unajiuliza international maana yake nini? Je kuimba na Wanaija ndiyo u international wanaousema? Hata kama ni hivyo, hili lina uhusiano gani na tuzo za jana? Kiroja zaidi ni pale hao hao mashabiki wanaoponda tuzo za nyumbani pamoja na mashabiki wa kiba, ndiyo hao hao wanataka tuwapigie kura kwenye tuzo za MTV, yani unaponda watu na kuwatukana then wapige kura ili ushinde na uwatukane zaidi? Kwa mimi siwezi kusupport hili na kura yangu hawawezi kuipata!

5. Kwamba kuna mkakakati wa Clouds wa kumshusha Diamond na kumpandisha Kiba!!
Hapa mwenye kufikiri sawasawa unajiuliza Kiba anapandishwa kwenda wapi? Alikiba wa Cinderela, Run dunia, Dushelele, My everything, Far away na Nakshi nakshi anapandishwa kwa kumshusha Diamond, utani mwingine huu!! Inawezekana kweli anashushwa lakini yeye alipopata tuzo 7 mwaka jana nani alikuwa anashushwa ili yeye apande?

6. Kwamba tuzo za Alikiba alizopata ni 5 ni siyo 6!!
Hapa napo kuna viroja, maana wanaopinga tuzo ya collaboration kuhesabiwa kama tuzo ya Kiba ndiyo hao hao wanaojumuisha tuzo ya "muziki gani" kufanya Diamond awe na tuzo 7 mwaka jana!

7. Eti wimbo mmoja tu unampa tuzo zote hizo?
Sasa hawa sijui walitaka apewe tuzo kwa nyimbo ngapi? Sasa sijui wamezeeka au sijui wamekula maharage ya wapi? Maana wasingekuwa wavivu wangefuatilia tuzo nyingine duniani zinavyoenda, wangejua hata "Some one like you" ya Adele ilimpa tuzo ngapi, na hata Blank space ya Taylor Swift ilimpa tuzo ngapi pia!!

NB; Malalamiko huwa hayakosekani popote, ila tunapolalamika angalau malalamiko yawe na mashiko basi! Lazima tujue kuwa wimbo/msanii akiwa nominated maana yake kuna uwezekano akashinda, sasa hapo hakuna ajabu katika walioshinda jana!!

Kabla ya kuja na maswali ya je alistahili kushinda, tungeuliza kwanza je alistahili kuwa nominated? Kama alistahili kuwa katika category husika basi anastahili kushinda!! Kuna watu walifikiri zile kura ni mchezo wa kuigiza labda, maana kama unaelewa nguvu ya kura huwezi kuja na maneno kama "wamemnyima tuzo", labda useme "nimemnyima/tumemnyima"...mimi kwa upande wangu nimemnyima tuzo Diamond na nimempa Kiba, pia nimemnyima Bella..na si kwamba Bella hakustahili hapana, kuwa category moja na Kiba ndiko kumemnyima kura yangu!!

Mwisho nimpe pongezi kwa mara nyingine Alikiba kwa kushinda katika category 6 kati ya 7 alizokuwa nominated
 
acha ujinga, sasa hapo umetoa hoja gani hizo? umenichekesha sana kwa jinsi ulivyo argue as if unajua sana, kumbe ni pumba tupu, Dai hafananishwi na hao wasanii wenu wadogo wadogo, uyo Ally Kiba nani anamjua nje ya Tanzania..? Dai sio size yenu.
 
Nasema juzi jana na leo.Ali kiba na diamond hawawezi shindana .mshindanishe diamond na watu levo zake hyu kiba labda mumshindanishe na ney wa mitego idadi ya watoto.Diamond ni level zingine ndo mana chuo kikuu wamsmpa tuzo ya heshima.kiba alitoka,akang'aa akafubaaa sasa ndo kashtuka muziki kazi sio mapenzi?kutumbuiza sibishii labda anamtumbuiza madam rita kitandani lakini sio afananishwe na Diamond on stage.na nyie mazafanta ktma hata mpige kura uchaguzi mkuu mkiwa uchi...diamond hatakaa ashuke kwa juhudi za mtu yoyote isipokua yeye
 
Wallah asilani muziki wa bongo hautaendelea, acha mie nijisikilizie nyimbo za Ferre gola na fally ipupa na baba yao koffi
 
Haya msisahau kuwapigia kura wanaopeperusha nchi yetu kimataifa


Kupiga kura
Diamond Platnumz kategori 3 (tatu) - Best MALE, Best COLLABORATION na Best LIVE and Vanessa 1(moja) -- Best FEMALE

ingia kwa link hii chini

http://mama.mtv.com/voting/


Bonyeza bonyeza VOTE usichoke
 
Kwanza wakome kumshindanisha king Kiba wetu na muimba taarab, asubiri mwakani apambane na mzee Yusuph huko.
 
Kituko na kiroja kingine ni account fake ya kilimanjaro.
I salute your analysis...
Wacha tuendelee kumsupport Kiba.
Mie nilimnyima Diamond na wengine wote katika vipengele walivopambanishwa na Kiba.

Dear hii account ina mkanganyiko, natamani kupata tamko kutoka kwa Kill wenyewe.
Ila ninavyojua mimi page yao haikuwa hivyo wakati nilivyoitembelea kipindi cha kupiga kura.
 
Dear hii account ina mkanganyiko, natamani kupata tamko kutoka kwa Kill wenyewe.
Ila ninavyojua mimi page yao haikuwa hivyo wakati nilivyoitembelea kipindi cha kupiga kura.
Watajijuaaaa sie tunafurahia
So hiyo tuzo ilimpasa nan ??
 
Watajijuaaaa sie tunafurahia
So hiyo tuzo ilimpasa nan ??

Nani zaidi ya King Ali Kiba? Kwa miaka hii ya sasa kufanya mziki wa play back ni aibu.
King anapiga live, ndio maana akapewa.Wasiotaka na wajinyonge tu maana aliyestahili keshapewa.....hakuna jinsi nyingine.
 
4. Kwamba wao wanadeal na tuzo za kimataifa tu, hizi local hawazitaki!!
+tuache hizo # zingine naomba kujua hii # 5, ina maana mkuu wewe hadi leo huamini kama Diamond ni msanii wa kimataifa?

+au wewe hili neno intranational linakupa shida mkuu? Maana naona nyinyi mashabiki wa Kiba ikiongelewa Chibu ni wa kimataifa huwa mnataja Nigeria tu pekeake mnasahau kwa juhudi zake kijana wa watu anajulikana Ghana, Congo na kwingineko au hayo sio mataifa?

+mtoa mada ungeonekana ni shabiki wa kweli wa musiki wa bongo ungempa pongezi kijana kupiga hatua kimataifa.
Kiroja zaidi ni pale hao hao mashabiki wanaoponda tuzo za nyumbani pamoja na mashabiki wa kiba, ndiyo hao hao wanataka tuwapigie kura kwenye tuzo za MTV, yani unaponda watu na kuwatukana then wapige kura ili ushinde na uwatukane zaidi? Kwa mimi siwezi kusupport hili na kura yangu hawawezi kuipata!

+Kwa hiyo hapo kwenye mstari anaetukana watu baada ya kupata tuzo ni Diamond au mashabiki?

+kama kweli wamekutukana haya sawa, sasa swali ni je aliyekuomba kura ni Diamond au mashabiki?

+Hapa wewe kama kweli ni shabiki wa kweli wa muziki wa bongo unamsikiliza nani Diamond au mashabi. Au huna msimamo binafsi unaongozwa na mihemko ya mashabiki?

+kama wewe ni mshabiki wa kweli wa muziki bongo ni aibu kubwa kumpigia kura msanii wa nje eti tu upo katika vita na mashabiki wa yule msanii aliyekua nominated. Kweli hii inatokea bongo hata wenzetu watatushangaa.
 
acha ujinga, sasa hapo umetoa hoja gani hizo? umenichekesha sana kwa jinsi ulivyo argue as if unajua sana, kumbe ni pumba tupu, Dai hafananishwi na hao wasanii wenu wadogo wadogo, uyo Ally Kiba nani anamjua nje ya Tanzania..? Dai sio size yenu.

mkuu msisahau vitu haraka jamani hivi bumbum ni nyimbo ambayo ilistahili kuwa nominoted kwenye MTV awards sasa mbona kinacho lalamikiwa kwa kiba mi ckioni ni chuki tu hizo KING KIBA :D:D:D:D:D:D
 
Back
Top Bottom