Hivi Mgao umeanza tena kimyakimya?

Arumeru Mashariki na vijiji vyake hakuna Stima, umeme wala megawatts tokea asubuhi mpaka saa hii...

Wazee wanasema wanangoja Order ya kuwasha au Laa.
 
hivi labda mmesikia taarifa katika vyombo vya habari kuhusu huu umeme zaidi ya masaa 24 sasa???waziri wa nishati vipi kalala ama...!vasco najua yupo mkutano wa uzazi wa mpango UK yani izi shida na sisi tuliojiajiri na biashara haiwezekan adi umeme
 
Moshi hakuna megawats tangia saa 5 asubhi mpaka usiku huu wa manane
 
Hii nchi viongozi wake sijui wamerogwa! Hata kutoa taarifa kwa umma wanashindwa kama umeme hautakuwepo ili watu wasiwe na hali ya sintofahamu! Mazafanta!
 
kweli zimwi la richmond noma leo kutajwa bungeni imekua noma au ndio hizo generator Nazi zimekua dhaifu
 
Kwa kweli tatizo la umeme serikali iliangalie kwa macho mawili. SUA watu wanafanya mitihani halafu umeme unakoseka kwa muda mrefu, mchana kutwa mpaka usiku wa manane, wanaweza kuchangia kufelisha wanachuo.
 
Doctor Ulimboka will be back and soon he is going to speak out about what happened and what is going on.And one of the main channel to capture these informations is through TANESCO! Discuss...................! Why TANESCO wakazima umeme bila taarifa yoyote kwa umma afu kwa muda mrefu wote huo? Nakusanya majibu............. then ntawapeni majibu mengine.
 
sasa wale wapinga kila thread inayoikosoa hii serikali legelege na dhaifa ebu waje hapa waeleze,je katika hili serikali si dhaifu na imeshindwa kabisa kuwa karibu na wanainchi?hizi si chuki wanayojenga ndani yetu?inakuweje nchi inayosema inaingizwa na "watu makini"na wale wakina mwigulu wanaotoka mapovu bungeni haya uwa hawaoni waikosoe serikali ya chama chao? inakuweje umeme unakatika mahali-mahali na mkurugnezi wa tanesco na serikali kupitia wizara husika wako kimya?au bado new waziri-s wako ktk mafunzo bado?hakuna umeme toka asubuhi na mapema waseme tu tushazoe kama ni mgao au TATIZO LA KIFUNDI manina kweli hawa
 
TANESCO is dead.Mbozi(mbeya)hakuna umee.Unawaka midnight tuu.Nadhani bora kuhama nchi.
 
inashangaza sana, meneja wa mkoa wa arusha ameulizwa na waandishi wa habari akawa na kigugumizi, hana taarifa rasmi kutoka makao makuu. lakini hapa mjini mgao kama kazi. vyakula vimeharibika kwenye mafriji,samaki na kuku sokoni vimeharibika. My take, ni vyema wakatoa taarifa na ratiba ya mgao.
 
TANESCO is dead.Mbozi(mbeya)hakuna umee.Unawaka midnight tuu.Nadhani bora kuhama nchi.
Hiyo sio dawa kuhama nchi. Mungu alichagua uwe Tanzania, hakukosea, inachotakiwa fukuza wayu kazi. Leta mabadiliko ya fikra kwa wote wanaokuzunguka na mema ya nchi tutayaona.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom