Hivi Mgao umeanza tena kimyakimya?

Nadhani ifike wakati tuachane na hizi semantics, mgawo; hitilafu, wizi, ubadhirifu... (who cares..) all in all wananchi inabidi wapate umeme 24/7 ni aibu taifa lenye miaka 50 bado umeme wa kudunduliza
 
Ninapoandika hapa ni group la pili la wafanyakzi wa juu wako ikulu wanaapishwa kulinda siri za tanesco zisitoke nje, hii ni pamoja na kuhakikisha kuwa taarifa za mgao mkali wa umeme hazitoki nje ya tanesco. Hali ni mbaya mikoa kama kilimanjaro inapata megawati 15 kwa siku, na mikoa mingine ni chini ya hapo.

Wafanyakazi wanakula kiapo hicho tangu jana, group la kwanza limeshinda ikulu hadi jioni, na sasa group lingine lipo huko tangu asubuhi

Source: Aliyeapishwa tayari
 
Niliwahi kuweka hii thread hapa jamvini, lakini ikatoweka na mpaka leo sijui iko wapi, naona mod anaweza kuwa naye yuko kundi hili,

mnamo mwezi Novembea, wafanyakazi wa ngazi za juu wa TANESCO, haswa wakuu wa vitengo na maafisa waandamizi, waliitwa ikulu kwa makundi na kupewa viapo kuwa wasitoe siri za TANESCO haswa mgao.

Hili la kuapishwa liko wazi, walioapishwa wapo.
 
Ndio maana mod walifyeka thread yako haina mashiko.Hapa tunachotaka ni facts, either hoja kujithibitisha yenyewe kutokana na umahiri wa mleta hoja au kuambatanisha vithibitisho vya maandishi,picha au sauti
 
Ushahidi kamhoji mfanyakazi yeyote afisa mwandamizi wa TANESCO, wako wengi sana, kuna unafiki mkubwa sana unafanywa na wizara, mwendelezo ule ule wa kudanganyana kuhusu mgao
 
Ni fedheha kwa serikali kusema uongo!

Ni aibu kwa viongozi wa TANESCO kujidanganya wenyewe!

Ni ufisadi mkubwa kuwasababishia wananchi hasara kutokana na kukosa huduma ya umeme ya uhakika!

Ni serikali isiyojali pekee inayoweza kubaki madarakani kwa ulaghai!
 
CCM imekosa mwelekeo
Ni fedheha kwa serikali kusema uongo!

Ni aibu kwa viongozi wa TANESCO kujidanganya wenyewe!

Ni ufisadi mkubwa kuwasababishia wananchi hasara kutokana na kukosa huduma ya umeme ya uhakika!

Ni serikali isiyojali pekee inayoweza kubaki madarakani kwa ulaghai!
 
Sijui mnaotaka jamaa atoe ushihidi mnaangalia nini, hivi mazingira tu ya upatikanaji wa umeme si ni ushahidi tosha? kuonesha kama haya madai yanaukweli, angalia watendaji wa Tanesco, wote wanakana kwamba hakuna mgao, lakini hata kama kuna Break down, matengenezo n.k, mbona muda wa umeme kukatika hua ni huo huo na hata interval, i mean muda waliokata na kurudisha kila siku hua zinafanana, huo si ni mgao tuo?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom