Hivi kwanini Wahindi na Waarabu hawajiungi vyama vya Upinzani?

wanahogopa kubanwa kwenye kodi na kurudishwa makwao

Kwao wapi Mumbai,Pakistan au Bangladesh?hv unajua majengo karbia yote unayoyaona mjini walijenga wao,serikali wakaja kuyataifisha harafu leo unasema warudi kwao,hakuna mtanzania harisi tukianza kuchunguzana tuache mambo ya ubagauzi kisa mtu ana ngozi nyeusi wakati ndio wamegeuka kuwa mafisadi wakubwa na wakoloni weusi.
 
wanahogopa kubanwa kwenye kodi na kurudishwa makwao

Acha ubaguzi wa rangi. Wao Watanzania kama wewe na wengi ni kizazi cha tatu.

Pili, ukiwafukuza, Tanzania ina uchumi wa kuwapa kazi wazawa watakaokosa kazi au utawapa wewe?

Unafikiri Mseveni mjinga alivyowakaribisha tena na kuwapa viwanda vyao? Au yeye sio Mzalendo kama Iddi Amin?

Fikiri kwa kichwa sio kwa chuki. Hatuna ubavu wa kustahamili kukosa kodi zao. Kuna ufisadi wa baadhi ya wafanyabiashara wa kila rangi wanaokula pamoja na viongozi wetu wabovu. Uzalendo hauna rangi.
 
kuna mwarabu mmoja hivi kama sio mzungu aligombea ubunge jimbo la kigoma ya kusini mwaka 2010 kupitia chadema
hutaki unaacha
 
Upinzani ukishinda, watahamia huko, maana wenyewe wanadai chama chochote kikikamata dola, wao wako huko, kwa sababu ya maslai yao.
 
LAT rosemarie wambagusta Wakuu nilienda kuwauliza mmmh wakajibu kuwa Wanatishiwa tishwa!! Ila wansema wakiungana wao watachukua nchi tena..... maana waafrika hawawezi kutawala kiuadilifu !!
 
Last edited by a moderator:
Upinzani ukishinda, watahamia huko, maana wenyewe wanadai chama chochote kikikamata dola, wao wako huko, kwa sababu ya maslai yao.
Masilahi gani Mkuu.... Miaka mia nane {800} wapo humu nchini.... toeeni nafasi uone watakavo badilisha nchi hii !!! Funguamacho uone miji waliojenga kwa mda mfupi tuu!! Au soma historiya au uliza wazee walikuwa ktk serekali ya mkoloni !! Wewe nenda kakaae foleni Hospitali.......
 
Miaka 800 ninini ndugu yangu, suala ni kwamba uwepo wao umesaidia nini maana naona unachanganya faida za kutawaliwa na gharama za uhuru.
 
Miaka 800 ninini ndugu yangu, suala ni kwamba uwepo wao umesaidia nini maana naona unachanganya faida za kutawaliwa na gharama za uhuru.
Wewe umelala au unasuasua hujui ulisemaloooo !!
Eeeh, hiyo lugha unayoongea ni kwenu ? Hiyo lafudhi unayoitumia uliileta wewe? Hiyo Amani unayo jivunia ulitunga kwa mantiki gani? Huo umoja wa nchi hii uliufunamanisha na katiba gani? Mwambao hadi kigoma na kaskazini hadi kusini mwa nchi wote kuwa na lugha moja ilikuwa kazi ya chifu gani au mtemi gani ???
Biashara na mashule yaliyosomesha wataalamu na viongozi wa nchi hii, jee ni shule za msingi na za kata?? Aamka wewe!!
Viwanda na majengo yaliyotaifishwa yalikuwa ya akina nani? bado kuna mengi sina wasaa wakupoteza hapa!!! Jioni njema alamsiki,,
 
nchi si yao

hawana uzalendo
Kwanini nini nchi si yao wakati ni watanzania wewe ni mbaguzi huna lolote tembea ulimwengu uone watu wanavyoishi, hakuna mambo hayo sasa ulimwenguni, Dunia imekua kama kisiwa kidogo, kila aina ya watu wanaishi pamoja na watu wanajulikana kwa uraia wao katika nchi wanayo ishi, watu wamevuka hiyo akili yako ya kutizama watu kwa rangi au kabila, kinachotizamwa ni uraia wa mtu ikiwemo hapa kwetu Tanzania.

Kwanini sifa ya kuwa mzalendo lazima uwe mpinzani,na kama itakua tafsiri ya uzalendo, mwenye akili kama zako hata mimi ntakuwa siyo mzalendo. Kila mwananchi ana haki ya kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasi anachotaka ilimradi kimesajiliwa kisheria na anakubaliana na sera zake.
 
Upinzani ukishinda, watahamia huko, maana wenyewe wanadai chama chochote kikikamata dola, wao wako huko, kwa sababu ya maslai yao.

Unaweza kuthibitisha maneno yako?

Kila Mtanzania ana haki ya kuchagua Chama anachopikenda. Kila mtu anachagua Chama kitakacholinda maslahi yake, hii ndio demokrasia!
 
Wewe umelala au unasuasua hujui ulisemaloooo !!
Eeeh, hiyo lugha unayoongea ni kwenu ? Hiyo lafudhi unayoitumia uliileta wewe? Hiyo Amani unayo jivunia ulitunga kwa mantiki gani? Huo umoja wa nchi hii uliufunamanisha na katiba gani? Mwambao hadi kigoma na kaskazini hadi kusini mwa nchi wote kuwa na lugha moja ilikuwa kazi ya chifu gani au mtemi gani ???
Biashara na mashule yaliyosomesha wataalamu na viongozi wa nchi hii, jee ni shule za msingi na za kata?? Aamka wewe!!
Viwanda na majengo yaliyotaifishwa yalikuwa ya akina nani? bado kuna mengi sina wasaa wakupoteza hapa!!! Jioni njema alamsiki,,

Halafu, bila hata chembe cha haya, anaomba viza Mtu kama huyu kwenda India kutibiwa au kumpeleka mwanawe kusoma. Bado kuomba na kupokea misaada.
 
Unaweza kuthibitisha maneno yako?

Kila Mtanzania ana haki ya kuchagua Chama anachopikenda. Kila mtu anachagua Chama kitakacholinda maslahi yake, hii ndio demokrasia!

Hah hah hah......., demokrasia ipi kaka? kwamba wao tangu nchi hii ipate uhuru, kweli hawaoni jambo linaloenda visivyo wakalipinga?

Nilisema pale mwanzo kwamba utumwa una gharama zake, moja za hizo ni huo mtizamo wenu wa kuabudu hao watu, bila nyie kuwa na imani na nyie wenyewe, na kujiona kwamba hamuwezi kitu mpaka hao jamaa kama ndugu yako 'Zamiluni' anavyoamini.

Wachina hawakuwahitaji wao, na wakaendelea....!
 
Back
Top Bottom