Nkuba25
JF-Expert Member
- Nov 18, 2015
- 2,268
- 12,496
Mzee wangu MohammedNkuba25,
Si kama hayo yalifanywa kwa bahati mbaya.
Kuna watu hawakuitaka historia hii.
Historia hii ilikuwa inawatisha sana na ndiyo
kisa cha kuja na historia ya Kuvukoni College.
Naweza kuamini kabisa haya uyasemayo pasipo shaka kabisa.
Sasa hivi nimeanza kufuatilia mihadhara yako mbalimbali kuanzia ile ya TV Stations, Radio Stations na hata Misikitini. Mimi always naangalia arguments za mtu irrespective anazungumzia wapi.
Mzee wangu Mohamed nilikuwa naangalia Clip yako moja ukagusia Habari ya bibi Titi Mohammed alivyofanyiwa, kwa lugha ya sisi vijana tunaita "Figisu-Figisu". Kwa kweli ilinisikitisha sana.
Mwanamama muhimu kama Bibi Titi, Leo hii humsikii kabisa katika historia ya nchi yetu. Yaana kwa ujumla, watu wachache waliibaka historia yetu.
Na kinachoniuma zaidi ni kufundishwa uchafu, uhongo, ujinga na upuuzi katika masomo yangu ya historia tokea niko Primary mpaka Secondary School.