Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes na Chief Michael Lukumbuzya

Nkuba25,
Si kama hayo yalifanywa kwa bahati mbaya.
Kuna watu hawakuitaka historia hii.

Historia hii ilikuwa inawatisha sana na ndiyo
kisa cha kuja na historia ya Kuvukoni College.
Mzee wangu Mohammed

Naweza kuamini kabisa haya uyasemayo pasipo shaka kabisa.

Sasa hivi nimeanza kufuatilia mihadhara yako mbalimbali kuanzia ile ya TV Stations, Radio Stations na hata Misikitini. Mimi always naangalia arguments za mtu irrespective anazungumzia wapi.

Mzee wangu Mohamed nilikuwa naangalia Clip yako moja ukagusia Habari ya bibi Titi Mohammed alivyofanyiwa, kwa lugha ya sisi vijana tunaita "Figisu-Figisu". Kwa kweli ilinisikitisha sana.

Mwanamama muhimu kama Bibi Titi, Leo hii humsikii kabisa katika historia ya nchi yetu. Yaana kwa ujumla, watu wachache waliibaka historia yetu.

Na kinachoniuma zaidi ni kufundishwa uchafu, uhongo, ujinga na upuuzi katika masomo yangu ya historia tokea niko Primary mpaka Secondary School.
 
Mzee Wangu Mohamed Said asalaam alaykum. Nimekuwa kimya kwa muda ila uzi haujanipita. Nakushukuru nimepata vitabu kwenye duka la ibn hamza. Hakika haya ni madini kama wasemavyo watoto wa mjini. Mungu akupe uhai mrefu uzidi kutupa ilm sisi vijana wako na wengine wengi ambao wanasoma kimyakimya
Kolorama,
Furaha yenu ndiyo furaha yangu.
''Elimu bila khiyana,'' chembelecho Maalim Faiza.
 
Al Habiby Sheikh Mohamed Said, nashukuru sana kwa kutuelimisha, habari hii imenifurahisha zaidi baada ya kumzungumzia Mama Daisy (Sisi tulikua tunamuita , Bi.Dezi), sikujua asili ya jina hilo kabla ya kusoma hapa.
Bibi huyu ametulea sisi pale temeke nyumbani kwake mtaa wa mjimwema mpaka mwisho wa maisha yake (Allahu marhamhu), nakumbuka maziko yake tumeyafanya pale katika nyumba yake mtaa wa Likwati.
Kama utakua na picha nyingine naomba unitumie.

Shukran
 
Marehem Ngariba alikuwa anapenda kutumia aya hii kabla hajaanza mihadhara wakati wa uhai wake allah amsameh makosa yake na amuweke ktk Firdaus.
WAKUL JAA LHAKU WAZAA LHAKKU INNALBAATILA KANA ZAHUKA......
Kolorama,
Haki imefika na batil ni yenye kutoweka.
 
Al Habiby Sheikh Mohamed Said, nashukuru sana kwa kutuelimisha, habari hii imenifurahisha zaidi baada ya kumzungumzia Mama Daisy (Sisi tulikua tunamuita , Bi.Dezi), sikujua asili ya jina hilo kabla ya kusoma hapa.
Bibi huyu ametulea sisi pale temeke nyumbani kwake mtaa wa mjimwema mpaka mwisho wa maisha yake (Allahu marhamhu), nakumbuka maziko yake tumeyafanya pale katika nyumba yake mtaa wa Likwati.
Kama utakua na picha nyingine naomba unitumie.

Shukran
Ammarito,
Mama Daisy ni mama yangu.

Nina picha kubwa sana ya ukutani ya Mama Daisy na Bwana Abdul Sykes
wamepiga Government House (sasa Ikulu) katika 1950s kwenye hafla waliyoalikwa
na Gavana Twinning.

Ikiwa nitaweza kuipiga nitakuwekea hapa In Shaallah.
 
Hongera ni historia nzuri
Mkunyegere,
Hakika historia ya TANU na harakati za kudai uhuru ni kisa khasa.

Bi. Titi Mohamed anaghadithia anasema wako Tabora 1958 wakati
wa Kura Tatu.

Hali ilikuwa tete kupelekea TANU kumeguka pande mbili.

Baadhi ya wanachama wamekataa kata kata kuingia katika uchaguzi
ule wenye masharti ya kibaguzi.

Mwalimu Nyerere ameingiwa na hofu ana wasiwasi chama kitavunjika.

Wapinzani wa Kura tatu ni watu wenye nguvu katika chama wakiongozwa
na watu kama Jumanne Abdallah, Bhoke Munanka, Sheikh Suleiman
Takadir
na wengineo.

Mwalimu Nyerere akawa hana hata hamu ya kula chakula anashindia maziwa.

Bi. Titi
akimmudu sana Mwalimu Nyerere na watu wengi hawajui hili jina la
Mwalimu Nyerere alipewa na Bi. Titi.

Bi. Titi kamfuata Nyerere anamwabia,'' Nini wewe nasikia hutaki kula. Unaogopa
kufungwa? Mwenzako Kenyatta yuko jela nini wewe unaogopa kufungwa?''

''Sikiliza Titi si lazima nende jela...''
Mwalimu alijibu kwa unyonge kabisa.

Ukipenda kukijua kisa cha Kura Tatu ingia hapo chini:
Mohamed Said: UCHAGUZI WA KWANZA TANGANYIKA ''UCHAGUZI WA KURA TATU'' 1958 KUTOKA KUMBUKUMBU ZAKE SHEIKH SEMBE
 
UKIPUNGUZA UDINI UTAKUWA MWANDISHI MZURI SANA KAKA!
 
Ndugu Mohamed Said, napenda kusikia japo kidogo tu historia iliobeba jina la hii thread, Historia ya Chief Lukumbuzya! Bibi yangu alikua akiutaja sana huu ukoo wa kichifu!
 
UKIPUNGUZA UDINI UTAKUWA MWANDISHI MZURI SANA KAKA!
Mkuu mzee Muhamed hana udini hata chembe.
Bahati mbaya watu wengi hawapendi tu kuona au kusikia lolote kuhusu uislam au muislam.
Na bahati mbaya sana wengi wa wagombea uhuru ni kutoka ktk jamii ya kiislam hasasa kwa mwambao huu wa tanganyika.
Na bahati mbaya sana hiyo jamii ndio iliyopata zaidi madhila ya wakoloni wareno wajerumani mpaka muengereza.
Na mbaya zaidi ni maumbile tuliyo umbiwa maana ktk maumbile yetu kuna tafsiri mbili ya kila kitu.
Ukitaka kumtafsiri au kumuelewa mzee muhamed said kuwa anaudini inawezekana na ukitaka kumtafsiri kuwa hana udini na anania kutujuza yale yaliowakuta wagombania uhuru wa tanganyika pia inawzekana.
 
UKIPUNGUZA UDINI UTAKUWA MWANDISHI MZURI SANA KAKA!
Gangogine,
Mimi naandika historia ya uhuru wa Tanganyika ambayo kwa
bahati mbaya kwako imetawaliwa na Waislam na hivyo ndivyo
ilivyokuwa

Ikiwa wewe unaona kuwa huo ni ''udini,'' hii ni bahati mbaya
sana kwako.

Nimeandika kitabu cha Abdul Sykes naamini unakifahamu na
kilifanyiwa mapitio na mabingwa wa historia ya Afrika.

Hakuna hata mmoja kati yao aliyenishutumu kwa udini.
 
Ndugu Mohamed Said, napenda kusikia japo kidogo tu historia iliobeba jina la hii thread, Historia ya Chief Lukumbuzya! Bibi yangu alikua akiutaja sana huu ukoo wa kichifu!
Disguise,
Google utapata habari nyingi sana za maisha ya Chief Lukumbuzya.
 
Gangogine,
Mimi naandika historia ya uhuru wa Tanganyika ambayo kwa
bahati mbaya kwako imetawaliwa na Waislam na hivyo ndivyo
ilivyokuwa

Ikiwa wewe unaona kuwa huo ni ''udini,'' hii ni bahati mbaya
sana kwako.

Nimeandika kitabu cha Abdul Sykes naamini unakifahamu na
kilifanyiwa mapitio na mabingwa wa historia ya Afrika.

Hakuna hata mmoja kati yao aliyenishutumu kwa udini.
Unachoambiwa una udini ni kuona kwamba Waislam wanaonewa japo walipigania uhuru wa Tanganyika pengine kuliko dini zingine. Hutaki kuona sababu za ndani zinazorudisha nyuma harakati za Waislam kupiga hatua ambazo zinatokana na wao wenyewe!
 
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom