Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,922
- 30,271
Picha hiyo huyo ni Ilyas Abdulwahid Sykes. Jina la utani udogoni tukimwita "Jaluo."
Kanitembelea nyumbani kwangu na hapa namwonesha Maktaba iliyohifadhi historia ya baba yake marehemu Abdulwahid Sykes.
Baada ya kifo cha baba yake Ilyas na kaka yake marehemu Kleist walikwenda kusoma Canada ambako baba yao mdogo Abbas Sykes alikuwa balozi.
Kleist alirejea nyumbani Tanzania lakini Ilyas yeye hakurudi.
Nimemwonesha katika Maktaba kitabu cha maisha ya Abdulwahid Sykes (1989) na kitabu cha maisha ya Julius Nyerere (2020) vikiwa pamoja; vitabu vya historia ya maisha ya marafiki wawili waliosimama bega kwa bega kupigania uhuru wa Tanganyika hadi ukapatikana 1961.