Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes na Chief Michael Lukumbuzya

Degree ya nini, hebu tukumbushe, na uiweke hapa
His intelligence was quickly recognized by the Roman Catholic fathers who taught him. He went on, with their help, to train as a teacher at Makerere University in Kampala (Uganda). On gaining his Certificate, he taught for three years and then went on a government scholarship to study history and political economy for his Master of Arts at the University of Edinburgh
 
Iweke hapa hiyo degree, unaweka masters. Mi nimekuomba degree
 
His intelligence was quickly recognized by the Roman Catholic fathers who taught him. He went on, with their help, to train as a teacher at Makerere University in Kampala (Uganda). On gaining his Certificate, he taught for three years and then went on a government scholarship to study history and political economy for his Master of Arts at the University of Edinburgh
Ndakilawe,
Kichwa cha Mwalimu Nyerere si cha kufanyia maskhara.

Mimi nimetafiti na katika utafiti nimekutana na mengi kuhusu Nyerere na
vipi aliweza kupangua na kuzishinda njama za Waingereza hadi uhuru wa
Tanganyika ukapatikana.

Jiulize iweje ''the brains,'' za wakati ule, Hamza Mwapachu, Abdul Sykes,
na wengineo wote wamuamini kuwa anaweza kulivusha jahazi katika hali
ile ya dhoruba kali.

Haya acha wakati akipigania uhuru wa Tanganyika alikuwa vilevile akifanya
mipango vipi ataitia mkononi Zanzibar na akifanya mazungumzo na watu hodari
wa wakati ule katika siasa za visiwani mtu kama Ali Muhsin akikaanae tena
nyumbanii kwake Ali Muhsin kufanya vikao vya siri.

Ali Muhsin alikuwa ndiyo nguzo ya siasa za kizalendo Zanzibar na akapewa jina
anaitwa, ''Zaim,'' yaani ''Kiongozi,'' msomi wa Makerere na tayari Hizbu ishaundwa.

Nyerere akalivuta zulia chini ya miguu ya Ali Muhsin.
Nina mengi ya Mwalimu Nyerere.

IMG-20150527-WA0049.jpg

Chini Kwenye Ngazi ya Ndege Ali Muhsin Barwani, Mohamed Shamte,
Hasnu Makame na Abeid Amani Karume wakati wa kupigania uhuru
wa Zanzibar Ali Muhsin kaandika kitabu, ''Conflict and Harmony in
Zanzibar,'' kamueleza Mwalimu Nyerere vizuri sana. Kitabu hiki
kinapatikana Tanzania Publishing House, Samora Avenue Dar es Salaam
 
Mkuu Mohamed Said, umenijuza kitu, kumbe kulikuwa na combination ya hawa watu. Nilikuwa sijui kabisa, sasa Shamte alipotea vipi baada ya uhuru wa Zanzibar
 
Ndakilawe,
Kichwa cha Mwalimu Nyerere si cha kufanyia maskhara.

Mimi nimetafiti na katika utafiti nimekutana na mengi kuhusu Nyerere na
vipi aliweza kupangua na kuzishinda njama za Waingereza hadi uhuru wa
Tanganyika ukapatikana.

Jiulize iweje ''the brains,'' za wakati ule, Hamza Mwapachu, Abdul Sykes,
na wengineo wote wamuamini kuwa anaweza kulivusha jahazi katika hali
ile ya dhoruba kali.

Haya acha wakati akipigania uhuru wa Tanganyika alikuwa vilevile akifanya
mipango vipi ataitia mkononi Zanzibar na akifanya mazungumzo na watu hodari
wa wakati ule katika siasa za visiwani mtu kama Ali Muhsin akikaanae tena
nyumabi kwa Ali Muhsin kufanya vikao vya siri.

Ali Muhsin alikuwa ndiyo nguzo ya siasa za kizalendo Zanzibar na akapewa jina
anaitwa, ''Zaim,'' yaani ''Kiongozi,'' msomi wa Makerere na tayari Hizbu ishaundwa.

Nyerere akalivuta zulia chini ya miguu ya Ali Muhsin.
Nina mengi ya Mwalimu Nyerere.

IMG-20150527-WA0049.jpg

Chini Kwenye Ngazi ya Ndege Ali Muhsin Barwani, Mohamed Shamte,
Hasnu Makame na Abeid Amani Karume wakati wa kupigania uhuru
wa Zanzibar
Ilikuwaje Ali Muhsin akakubali kuongozwa na Karume, ambaye wakati huo inasemwa hakuwa na elimu yoyote
 
Ilikuwaje Ali Muhsin akakubali kuongozwa na Karume, ambaye wakati huo inasemwa hakuwa na elimu yoyote
Ndakilawe,
Ali Muhsin
hakupatapo kuongozwa na Karume ila baada ya serikali
ya Hizbu kupinduliwa.

Ali Muhsin na serikali ya ZNP/ZPPP viongozi wote wakaletwa Bara na
wakawekwa kifungoni na Ali Muhsin akafungwa kwa miaka 10.

Nakuomba usome kitabu cha Ali Muhsin uijue historia ya Zanzibar.

Kitabu kinapatikana pia Ibn Hazm Bookshop Msikiti wa Manyema
na Mtoro, Elite Bookshop Mbezi Samaki na Soma Bookshop Mikocheni.
 
Ndakilawe,
Ali Muhsin
hakupatapo kuongozwa na Karume ila baada ya serikali
ya Hizbu kupinduliwa.

Ali Muhsin na serikali ya ZNP/ZPPP viongozi wote wakaletwa Bara na
wakwekwa kifungoni na Ali Muhsin akafungwa kwa miaka 10.

Nakuomba usome kitabu cha Ali Muhsin uijue historia ya Zanzibar.

Kitabu kinapatikana pia Ibn Hazm Bookshop Msikiti wa Manyema
na Mtoro, Elite Bookshop Mbezi Samaki na Soma Bookschenihop Mikocheni.
Tanganyika library havipatikani
 
Mkuu Mohamed Said, umenijuza kitu, kumbe kulikuwa na combination ya hawa watu. Nilikuwa sijui kabisa, sasa Shamte alipotea vipi baada ya uhuru wa Zanzibar
Onyx,
Nakushauri usome kitabu cha Ali Muhsin, ''Conflict and Harmony in Zanzibar,''
yote yamo ndani.

Mohamed Shamte serikali yake ilipinduliwa na akafungwa Bara.

Nakuwekea picha hapo chini nikifanya mahojiano ya televisheni na
mtoto wa Sheikh Mohamed Shamte, Baraka Shamte kada mkubwa
wa CCM Zanzibar.

Baraka alinieleza mengi kuhusu baba yake wakati akiwa kifungoni hadi
kufikia umauti wake akiwa uhamishoni Arabuni:

20121124_144923.jpg
 
Naona unafyonza Ilm tu pamoja na ujeuri wako tulizana piga goti usomeshwe history.
Carlos...
Mijadala hii inahitaji ustahamilivu sana kwa kuwa wengi wanaokuja
kuchangia huwa wanakuja wakiwa tayari wameshaathirika sana na
historia ya aina ya Chuo Cha Kivukoni.

Anapoelezwa historia ambayo inapingana na ile na khasa anaposoma
majina ya Waislam hamaki zinampanda na kuanza kwa kweli wakati
mwingine kutoa hata matusi.

Lakni mimi najua kuwa hayo ninayomueleza ndiyo kweli yenyewe hata
kama kwake ndiyo mara ya kwanza kaisikia.

Hapo inataka utaratibu na jambo lolote likitanguliwa na upole jambo
hupendeza.

Kuna mtu kaja hapa barzani ananidai mimi nimpe data za shule ngapi
Waislam wanazo.

Yeye anataka hizo data ili afananishe na takwimu za vyuo ambavyo
Kanisa limejenga.

Yeye anajuna wazi na fika kuwa Waislam mayatima hawana lolote la
kuonyesha.

Nikamwambia ukitaka kujua tatizo hili tusianze na data kutoka kwa
Waislam tuanze na data kutoka vyanzo vya kanisa vipi limeweza kuwa
kama lilivyo Tanzania.

Nikawa nampa rejea za kusoma.

Akawa anajibu kwa kejeli na kibri na kusoma hizo rejea hataki na hapo
nilimtahadharisha uzito wa hilo somo.

Lakini mimi sikuwa na haraka na yeye kwani najua wapi utakuwa ukomo
wake.

Katika kujibu maswali ya wachangiaji wengine waliotaka kujua kulikoni na
mimi nikawa najibu sasa yeye akaanza kuelewa kuwa lipo jambo kwani
serikali yenyewe ilipiga marufuku kitabu cha Hamza Njozi, ''Mwembechai
Killings...'' baada ya kuja na ushahidi ambao Mkapa aliudai kutoka kwa
Waislam kuwa ipo dhulma.

Mkapa alipoingia madarakani aliomba apewe ''ushahidi wa kisayansi,''
kutoka kwa Waislam kuwa katika serikali kuna watu wanatumia nafasi
zao kuwakandamiza Waislam.

Hii ilikuwa Ukumbi wa Diamond akijibu hotuba ya Islamic Club iliyosomwa na
Ramadhani Madabida.

Usia wangu kwenu nyote ni kuwa tusiache kueleza ukweli taratibu hili jambo
litaeleweka.

Katika kueleweka hili tatizo dawa yake In Shaallah itapatikana.

DZs1DuWhU3MzUEEfK4leyMy9axjhYxnOOMeV0V0kbcpyWrbq7QrExA90LQqt5G1WlDV7vHK21AmehJ6ALF1MYy88yk0LgQsl04vyMfMIzVBwnTQkSVWDSp69K7kD89r_SsczV1YVeIrw5zZwCrB_gwH5bQeWqNo5jUbS081XpaZUnmFCQjNJXyOUXF0D6RVyPxp7vCVZ0sRe4_uDa0cELuLe0elWVedTpdG9AgPzx5XhYUpwT5uXl6QmGoxdbaL-Jih6TfOimmxlUyb9Lo3w9KoJkvyZC_7APVKb6_quZkjeKO5tvnWj_c2Cnr-5w0aA8s54xiDWTVZNqpZiYE7f8A0eLJK9fVZTTSA1BMbf4TJgDrmsNGnM496pNwfiDawyqfLlXmXyUuXsF3GGUKKBGASeCSC2FcPCOqA3J-042t_ddQH4kMrscf_OQAaphW6UgHno_6Ah4pCBcXzvusnt1Vttxb2o0YmNeewP1AqMuAr_wAmlgK08r9CfL452QbSJG3BSECwQKrBiYB_PnGCAcdPjTGPZEre0DceHSFiCT8_CudnfzWKKRe_EMijlKVgyGH5TmY_Liab_hCm-zZfsKvODqrWv6ro=w384-h288-no

Prof. Njozi na Mwandishi Johannesburg 2006
 
Salaam Aleykum Mudir/Maalim wangu Mohamed Said, usia wako tumeupokea kuwa “tusiache kueleza ukweli taratibu hili jambo litaeleweka”
In Shaa Allah tunaowaeleza watatuelewa na Mwenyezi Mungu azidi kukupa maarifa ya kutuelimisha wote kwa pamoja
 
Back
Top Bottom