Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes na Chief Michael Lukumbuzya

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,915
30,259
CtOKRwRzrB5mBzQ5Cb9hS_jD8pN0sOFV1B9UckVYU8i70_Q_XEgdcQvlLqtXwNIGW3VWYaLF4a3otlgbC7K9Em0h3Ei39ed7tspSVQ5gtgrZL5rX2su_TqGlyreZorkWRdRYWBJm9Hn-QodC4i5vw06b46UkgySmTNjczP8cj6bmXb4RA6T3qSC_BRU6IEc8Uk75bpciUYbt_YdFaT-dh7hXKdN7cAdD9DHdB4xKJnFGYL4kk1Re5KOjQb6dQbt6-W2QvuYpX7q_3wE2ayyasqEFYWkowgSSkAVFoSq7jL6StW7uicmeAbddSAD_lW0f1GKpvu4xqI9a4PI-bYpm_24kxvl6H8PB1jGH53J9kAbmKXXFPW9YH4qAATIs8DSUScqrg8cJFiy35i4w8jl_JY9uTugl2Aw44difR64FY7bDSEaxEnvJoAwt7M-fxGIG15Umq6XOPqn2rzgSW-lp0fZFNQw9Psx1PGIaIrPRkMAm9PszJcCMiwBkZ9tPSxmQbYeMWxj0yL1lzzPXdNCcTFcoGpAmatJ1uOku2ZCcVz5Si6WIiO58WJjxk8cC3pX-kibj3Y1fBK5co9QGLfLHjSh0zHTOmAOH=w579-h657-no

Chief Michael Lukumbuzya wa Ukerewe​

Nilikuwa naitafuta picha ya hayati Chief Michael Lukumbuzya kwa miaka mingi bila mafanikio. Sababu ya kuitafuta picha ya Chief Lukumbuzya ni kisa alichonihadithia Bi. Mwamvua biti Masha mke wa marehemu Abdulwahid Sykes maarufu akijuikana kwa jina la mwanae wa kwanza Daisy hivyo tukimuita Mama Daisy.

Nilikuwa kila nikipata fursa ya kuwa na mama yangu Bi. Mwamvua, yaani Mama Daisy nikipenda kumdodosa mambo yalivyokuwa wakati wa ukoloni walipokuwa wanapambana na Muingereza, kwanza kichinichini katika miaka ya mwanzo ya 1950 wakati wa TAA kisha wakipambana na mkoloni dhahiri baada ya kuunda TANU mwaka wa 1954.

Bi. Mwamvua
alikuwa wakati mwingine bila kutegemea akiniangushia habari muhimu kupita kiasi. Mfano siku aliponiambia kuwa nafasi ya president wa TANU nafasi ile ilikuwa ya Chief Kidaha Makwaia lakini alikataa ndipo bahati ikamuangukia Julius Nyerere.

IMG-20160406-WA0111%2B%25281%2529.jpg

Chief David Kidaha Makwaia​

Iko siku akanieleza taharuki iliyotokea nyumbani kwa Abdul Sykes baada ya Nyerere kula chakuka kilichomfanya tumbo limkate na ikadhaniwa kuwa amelishwa sumu.

Mkasa huu ulitokea wakati mama yake Nyerere, Bi. Mugaya Nyangombe yuko na Mama Maria Nyerere vilevile wamekaa uani na akina mama wengine na Abdul Sykes, Nyerere na viongozi wengine wako nyumba kubwa wanapanga mipango ya kupeleka harakati mbele.

Mama yake Nyerere alianza kulia akiamini kabisa kuwa mwanae katiliwa sumu katika chakula. Mama Daisy alikuwa na habari nyingi sana za nyakati zile. Historia ya TANU kama zilivyo nyaraka na picha zake nyingi zimo mikononi mwa watu.

Mfano mwingine ni wa mkutano wa kwanza wa Wanawake wa TANU uliokuwa ukifanyika Arnautoglo Hall na yeye alikuwa yuko nyumbani anafanya shughuli zake. Anasema, ‘’Aliporudi nyumbani Bwana Abdul kanikuta nimekaa, akaniuliza wewe hukwenda mkutanoni? Wenzako wote wako Arnautoglo…’’ Bi. Mwamvua anasema hapo hapo akachukua baibui lake na kuelekea mkutanoni.

Wasemaji wakuu walikuwa Bi. Titi Mohamed na Bi. Tatu biti Mzee. Huu ndiyo mkutano wa kwanza wa wanawake wa TANU.

toW0HLKw0_eZRKHUURD38LIxZWcW5RXD7goNoYJWFVWEj8kMEyL1bPXqHWB5CmfrXmD1mA=w329-h566-no

Kushoto Mama Daisy na mbele yake ni Bi. Titi Mohamed
na Bi. Zainab mke wa Tewa Said Tewa

Katika mazungumzo kama haya ndipo siku moja akanihadithia habari za Chief Luumbuzya. Anasema walitoka Dar es Salaam yeye mumewe kwenda Nansio, Ukerewe kumtembelea Hamza Mwapachu.

Anasema walipanda meli Mwanza pamoja na Chief Lukumbuzya kuelekea Nansio. Lukumbuzya alikuwa anatokea Makerere Uganda alipokuwa anasoma anarudi nyumbani likizo. Abdul Sykes na Michael Lukumbuzya hawakuwa wanajuana.

Hamza Mwapachu alikuwa amekusanya wananchi na kikundi cha ngoma kuja kumpokea bandarini Nansio President wa TAA Abdulwahid Sykes. Lukumbuzya alishangazwa kukuta sherehe bandarini akifanyiwa mtu ambae yeye hakuwa anamjua na akiuliza anaambiwa ni mgeni kutoka Dar es Salaam.

Lukumbuzya alipigwa na butwaa kuona mapokezi ya watu wake wa Ukerewe wakiwa katika nderemo wakati yeye chief hakuna hata mtu alikuwa anajua kuwa yumo katika meli ile ile. Baadae Hamza Mwapachu alimfahamisha yule mgeni waliokuja kumpokea pale alikuwa nani katika siasa za Tanganyika.

proxy

Hamza Kibwana Mwapachu​

Simulizi kama hizi zilinifikirisha sana katika kutaka kuwajua wazalendo wa wakati ule. Hamza Mwapachu alikuwa anafanya haya ya kukusanya wananchi kumpokea kiongozi wa Waafrika chini ya pua za Waingereza bila kujali nini kitampata licha ya kuwa yeye kupewa uhamisho kupelekwa kisiwani Ukerewe peke yake ilikuwa ni adhabu, kwa hakika ni kifungo khasa cha kumtia kuzuizini asiweze kuenedeleza mipango yake ya kuunda chama cha siasa.

Uhuru ulipopatikana Chief Michael Lukumbuzya alipelekwa nje ambako alikuwa balozi na mwisho akawa balozi Canada ambako huko ndiko umauti ulikomfika.

6La5FUdYcnEadMYf6JSIrrWhkpElkSUYiAFTlRs_Bz4mDSXPmSD4EMzk4gTvEnMGuvf8pxy__jBGacnsvJHLYxP_wyS0OA25OYba8__txYHDI2z5TOfGkl7O_IoMO3NAleFvmru20T-YQF39hdK_UD7K79l2x2k40bDIMbiMoIB_ArerygwQ5oIGK11itARq1AoviA_D4OZrLGJZ-mOTiDWEC0pNQPmQPCS-cXzyWVr9raFuGLLKTwCz1GYMrJwsoBIeqCiy_AoHfwRMiTgHgBNRPHowAkwTnbtPxlJ_q9CTx_Ny6xhgBxkIMIBwc9Y79KJA7DXbYcODNB5X-lEL7SxzUEASzHc9r77_ByOVTHcN0j-HCDs2tr7oGw85M3YPXBv0OHG_2pnc_yZefK7n9_UyaxLXX1pmIeP1p01hc6LGf1QcrRusRSirpgfDZrxPMGTwr3EcKUjvY8vh1Kj2_zL9VnkUc-uHdQCSgUi6JBUaZrDi_2LVFAy1ImbD9BwIspcf8aHvXSBLQFSWfC2m3EGmjIMKOU2CDUXZv8NTjsn7UCfaBiWfrRT4ab3OSNhVpvB2GqLU1Rgk5_YjnfJgAxeKukdqeFoc=w476-h657-no

Abdulwahid Sykes​
 
Amwkwishaanza simulizi........hadithi hadithi....hadithi njoo, ukiona manyoya ujue kaliwa zamani.
 
Amwkwishaanza simulizi........hadithi hadithi....hadithi njoo, ukiona manyoya ujue kaliwa zamani.
Bigirita,
Katika uandishi unapotumia ''dots,'' sheria ni kuwa ziwe tatu tu ...

Mhariri wa kitabu cha Abdul Sykes Bi Mkubwa mmoja wa Kiingereza alipomaliza kuhariri kitabu alinitumia, ''note,'' akasema ''Mohamed you are a brilliant story teller I enjoyed your book...''
 
Inapendeza. Hizi ndiyo historia za kufundisha watoto wetu badala ya kujifunza sana historia za ulaya.

Kuna kisa kimoja, kuna wazungu walikuja hapa kwetu. Na katika majadiliano na vijana wa nyumbani wakashangazwa kuona vijana wenzao wanafahamu sana historia ya bara la Ulaya kuliko historia za bara la Afrika na matukio yake mengi muhimu.
 
Baada ya Uhuru Abdulwahid Sykes alikuwa na cheo gani/alifanya shughuli gani?
Kitulo,
Nimeandika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes unaweza kukipata
Ibn Hazm Media Centre Bookshop Msikiti wa Mtoro na Manyema
Dar es Salaam, Slip Way Novel Idea Bookshop na Soma Bookshop
Mikocheni.

Bei ni shs: 10,000.00.

Baada ya uhuru Abdul alianza kuandika historia ya TANU akisaidiana
na Dr. Klerruu hii kama tutaiita kazi na ofisi yake ilikuwa pale Lumumba
TANU HQ na baada ya mradi ule kupata matazizo Abdul alikwenda Cairo
alipokaa kwa muda kisha akarudi Dar es Salaam.

Mradi wa kuandika historia ya TANU ulikuwa chini ya Mwalimu Nyerere.
Hakujiingiza tena katika kazi ya kuajiriwa hadi umauti ulipomfika 1968.
 
Kwanini Abdul hakupewa cheo kikubwa serikalini
Onxy,
Swali lako limekwenda mbali na mbele zaidi kuwa kwa nini
Abdul hakupewa cheo kikubwa serikalini.

Kuna mambo mengi sana mimi yakikuwa yananitatizo wakati
nafanya utafiti wa kitabu chake.

Jambo la kwanza nnilikuwa najiuliza kwa nini yeye alikuwa na
nafasi nzuri ya kuchukua uongozi wa TAA kuanzia mwaka wa
1951 alipokaimu nafasi ya president wa TAA lakini yeye akawa
anataka nafasi ile aishike Chief David Kidaha Makwaia.

Na ilipofika mwaka wa 1952 alipokutana na Nyerere na mwaka
wa 1953 alitaka kauli ya mwisho ya Hamza Mwapachu kuwa
yeye amuuunge mkono Nyerere achukue nafasi ya president
wa TAA na yeye amsaidie Nyerere kukubalika kwa Waislam wa
Dar es Salaam.

Kote nilipopita sikuona mahali popote ambapo baada ya uchaguzi
wa yeye na Nyerere 17 April 1953 na Nyerere akapita kwa shida
hakuna mahali popote pale Abdul alisimama kutaka nafasi katika
TAA na baadae TANU.

Ukipitia historia ya Abdul unaona kuwa kutoka 1953 hadi kuunda
TANU 1954 akawa yeye kabakia zaidi kama ''party financier,''
akitoa fedha nyingi sana kupeleka TANU na kwa Nyerere kuliko
yeye mwenyewe kuwa ''active,'' katika siasa kama alivyokuwa kati
ya 1947 hadi 1954.

Mwaka wa 1960 Nyerere alipotaka jina la mmoja katika vijana wa
Dar es Salaam kutoka kwa Abdul kuingia katika serikali ya kwanza
Abdul alipendeleza kwa Nyerere jina la Tewa Said Tewa.

Inawezekana labda huku kuwapeleka wengine mbele ndiko khasa
kulikofanya asiwe katika nafasi za uongozi wa serikali baada ya uhuru.

Inawezekana hizi ndizo sababu rafiki kwa ukarimu wake jina la utani,
''The Sweet Abdulwahid Sykes.''
 
Onxy,
Swali lako limekwenda mbali na mbele zaidi kuwa kwa nini
Abdul hakupewa cheo kikubwa serikalini.

Kuna mambo mengi sana mimi yakikuwa yananitatizo wakati
nafanya utafiti wa kitabu chake.

Jambo la kwanza nnilikuwa najiuliza kwa nini yeye alikuwa na
nafasi nzuri ya kuchukua uongozi wa TAA kuanzia mwaka wa
1951 alipokaimu nafasi ya president wa TAA lakini yeye akawa
anataka nafasi ile aishike Chief David Kidaha Makwaia.

Na ilipofika mwaka wa 1952 alipokutana na Nyerere na mwaka
wa 1953 alitaka kauli ya mwisho ya Hamza Mwapachu kuwa
yeye amuuunge mkono Nyerere achukue nafasi ya president
wa TAA na yeye amsaidie Nyerere kukubalika kwa Waislam wa
Dar es Salaam.

Kote nilipopita sikuona mahali popote ambapo baada ya uchaguzi
wa yeye na Nyerere 17 April 1953 na Nyerere akapita kwa shida
hakuna mahali popote pale Abdul alisimama kutaka nafasi katika
TAA na baadae TANU.

Ukipitia historia ya Abdul unaona kuwa kutoka 1953 hadi kuunda
TANU 1954 akawa yeye kabakia zaidi kama ''party financier,''
akitoa fedha nyingi sana kupeleka TANU na kwa Nyerere kuliko
yeye mwenyewe kuwa ''active,'' katika siasa kama alivyokuwa kati
ya 1947 hadi 1954.

Mwaka wa 1960 Nyerere alipotaka jina la mmoja katika vijana wa
Dar es Salaam kutoka kwa Abdul kuingia katika serikali ya kwanza
Abdul alipendeleza kwa Nyerere jina la Tewa Said Tewa.

Inawezekana labda huku kuwapeleka wengine mbele ndiko khasa
kulikofanya asiwe katika nafasi za uongozi wa serikali baada ya uhuru.

Inawezekana hizi ndizo sababu rafiki kwa ukarimu wake jina la utani,
''The Sweet Abdulwahid Sykes.''
Mzee Mohamed Said, ingawa umejibu lakini yaonekana zipo sababu nyingine zaidi. Jibu lako bado halijatosheleza kiu ya watu wanafuatilia harakati za uhuru na kwa nini baadhi ya watu hawamo katika "historia rasmi". Napata shida sana kulimeza jibu lako.
Mzee wangu, haiwezekani muungwana kama Abdulwahid Sykes 'akasusa' na 'kukataa'(?) kujumuika na wenzake ili kuendeleza kile walichokiamini na kukipigania huku akichotumia muda, nguvu na raslimali kubwa.
Je kwa nini Julius Nyerere hakupenda kuwatumia kina Sykes katika kukiendeleza kile walichokiamini na kukipigania (Uhuru wa Tanganyika) ila ikawa vyepesi sana kuwatumia kina Mwapachu?
 
Back
Top Bottom