Hamad Rashid (CUF) na Ole Sendeka on TBC1

Sijaelewa msimamo wa Julius Mtatiro wa CuF kwani naona wabunge wa CuF wameunga mkono kila hoja ya ccm. Labda atuambie yeye amejiweka kwenye kundi gani katika hili suala.
 
Wamerudi sasa ole sendeka anaongea sheria ikipitishwa inaanza kutumika dec 1 2011:

Eti ni sawa rais kuteua wajumbe kwa kuwa sifa za wajumbe zimeainishwa. Sasa jaman sis tumeona uteuzi mbovu wa jk duh duh si atajaza watu watakao kuwa pro CCM.

Anashangaa watu kuhoji madaraka ya rais

Huyo ole sendeka si wanasema alitaga pale old moshi secondary?
 
Bunge litapitisha tu..... acheni kupoteza muda, focus iwe kwa wananchi kukataa au kukubali through referrendum.

Heri kupoteza muda sasa kuliko kupoteza muda huko baadaye. Watapitisha lakini hawataweza kulazimisha mawazo yao kutekelezwa.
 
Sijaelewa msimamo wa Julius Mtatiro wa CuF kwani naona wabunge wa CuF wameunga mkono kila hoja ya ccm. Labda atuambie yeye amejiweka kwenye kundi gani katika hili suala.
Umesikia amehama chama? Atakuwaje kinyume na maazio ya chama kumbuka huwa kunakuwa na vikao vya chama ili kuwa na msimamo wa pamoja juu jambo fulani hivyo hata Mtatiro anaunga mkono ingawa hajasema kwani yeye ni boss
 
We unazungumza.kwa nafasi aliyokuwa nayo mtei lazim angeshauri hivyo.
Kwan IMF NA WORLD BANK hazifanyi kazi nchin?(kama watoa mikopo katika miradi ya maendeleo)?
Wanafanya, ila ngoja nikuulize kama unajua IMF kazi yake ni nini?
Kwanini walitoa mikopo kwa Uruguay ambayo ilikuwa na positive balance of payments, wakaitolea nje Tanzania ambayo ilikuwa na negative balance of pyments?
Kamuulizeni mkuu wenu atawajibu.
 
Heri kupoteza muda sasa kuliko kupoteza muda huko baadaye. Watapitisha lakini hawataweza kulazimisha mawazo yao kutekelezwa.
Wangepitisha watu wao hata kama tungetumia mfumo wa Kenya. Tatizo ni Bunge kuwa 80% CCM.
 
Umesikia amehama chama? Atakuwaje kinyume na maazio ya chama kumbuka huwa kunakuwa na vikao vya chama ili kuwa na msimamo wa pamoja juu jambo fulani hivyo hata Mtatiro anaunga mkono ingawa hajasema kwani yeye ni boss

Mtatiro na CUF Tanganyika wameachwa solemba na CUF Zanzibar. Sitashangaa nikisikia siku moja Seif Sharrif Hamad na wenzake akina Hamad Rashid wameamua rasmi kuachana na CUF na kurudi nyumbani CCM waliko lelewa na kukulia!
 
Hapana mkuu. Ila ukweli unabaki palepale, CCM iliridhia uwepo wa vyama vingi kinyume na referrendum.

@SOBY, on the red, ni Mwl Nyerere sio ccm. Na tangu huyu Mwl aondoke we can see clearly ccm are nothing but a collection of dangerous imposters who cannot tell the difference between thier pocket and public purse.
 
Sendeka anaumwa? Hivi kwanini wanashikilia kuwa ni CCM iliyoruhusu vyama vingi?

Ni mtu mwenye matatizo ya afya ya akili pekee anayeweza kuimba wimbo wa kwamba ccm ndiyo iliruhusu vyama vingi, kwakuwa atakuwa hajui kwamba upepo wa mabadiliko ulikuwa umeshavuma pande zote za dunia na kwa namna ya pekee barani afrika na kwahiyo hakukuwa na njia mbadala isipokuwa Tanzania kama nchi kuanzisha mfumo wa vyama vingi. Hii hawawezi kamwe kuigeuza kuwa fadhila hata siku moja, ni kama wanavyojaribu kupotosha watu kwa kusema katiba mpya ni fadhila ya raisi!!
 
Watachagua vyama vingi. Ila hiyo haiondoi fact kwamba CCM iliruhusu vyama vingi, ingawa referrendum ilikataa.

Acha kujishaua. It was in CCM's best interest kuruhusu multiparty politics or else CCM ingeishia mwisho usio kuwa na jina. Si unajua recommendations za nyalali commission zilivyostate? So only option iliyokuwapo kwa ccm ilikua ni kuleta vyama vingi ila kwa kuudhibiti na kuumiliki mchakato wa kuanzishwa vyama vingi in favour of CCM. Political forces zilizokuwapo wakati ule zilikubaliana ingawa havikuridhishwa na uanzishwaji vyama vingi ndani ya mfumo kandamizi wa CCM unaothibitishwa na katiba ya mazingira ya chama kimoja na muunganiko uliopo hadi leo wa CCM na dola (msome Makulilo, Alexander (2008): tanzania a defacto one party state). Assumption ya political forces ilikuwa peace meal approach they were right, now wakati umefika umeiva sasa tunataka vyama vingi katika mazingira ya vyama vingi na hivyo katiba mpya ni lazima.
 
Ni mtu mwenye matatizo ya afya ya akili pekee anayeweza kuimba wimbo wa kwamba ccm ndiyo iliruhusu vyama vingi, kwakuwa atakuwa hajui kwamba upepo wa mabadiliko ulikuwa umeshavuma pande zote za dunia na kwa namna ya pekee barani afrika na kwahiyo hakukuwa na njia mbadala isipokuwa Tanzania kama nchi kuanzisha mfumo wa vyama vingi. Hii hawawezi kamwe kuigeuza kuwa fadhila hata siku moja, ni kama wanavyojaribu kupotosha watu kwa kusema katiba mpya ni fadhila ya raisi!!
Tanznia unayoizungumzia wewe ni tofauti na hii ya sasa hivi. Wananchi hawakutaka vyama vingi for whatever reasons.
CCM ikaridhia vyama vingi for whatever reasons. Na hakuna mtu aliyezungumzia mambo ya fadhila.
Mkuu, as lon as you don'thave the parliament, maamuzi yenu au uwakilishi wenu wa wananchi hauna mshiko. Nationally and internationally.
You gonna have to deal with it.
 
Tanznia unayoizungumzia wewe ni tofauti na hii ya sasa hivi. Wananchi hawakutaka vyama vingi for whatever reasons.
CCM ikaridhia vyama vingi for whatever reasons. Na hakuna mtu aliyezungumzia mambo ya fadhila.
Mkuu, as lon as you don'thave the parliament, maamuzi yenu au uwakilishi wenu wa wananchi hauna mshiko. Nationally and internationally.
You gonna have to deal with it.

Sijui miaka ya mwisho wa 80 na mwanzo wa 90 ulikua na umri gani na kama ulikua mtu mzima ni mwenye upeo kiasi gani na hizi siasa za kidunia mpaka utoe upupu wa aina hii! Jiulize swali dogo ni kwanini karibu nchi zote za Kiafrika zilianzisha mfumo wa vyama vingi ktk hicho kipindi?
 
Asilimia 78 ya watanzania walikataa vyama vingi. Unaikumbuka ile referrendum?

kiongozi kipindi hicho wengi tulikuwa bado wadogo na wazazi wengi awakuwa na elimu walikariri alama ya jembe na nyundo.wadhubutu sasa hivi waone graph itapanda upanda upande upi.we unafananisha kizazi iki na kile walichokuwa wanawekewa picha ya mwinyi na kivuli.gosh!
 
Nasikiliza hapa Hamad Rashid anatia kinyaa. Anatetea madaraka ya Rais kwamba katiba ya sasa ndio inayompa madaraka makubwa. Ndio maana tunataka katiba mpya isiyompa rais madaraka makubwa na lazima tuanze hapa kumnyang'anya madaraka. Hivi CUF wamepewa nini jamani wamekuwa wapumbavu sasa. Wanatetea kuliko hata ccm yenyewe. Mtu mwenye akili ndogo kabisa atajua kuwa rais ana mamlaka hata ya kubadilisha draft kupitia baraza la mawaziri na kwa vile yeye ndie anateua wabunge wengi wa bunge la katiba, kupitia bunge la katiba anaweza kubadilisha kabisha maoni ya wananchi. Ni zezeta tu ambaye hawezi kuona kuwa katiba hiyo italinda maslahi ya ccm na hivyo hakuna sababu ya kuwa na mchakato


Ndoa ya CUF na CCM inawafanya CUF kuunga mkono kila jambo linalotetewa na CCM. Kuhusu mjadala wa muswada wa uanzishwaji wa katiba mpya,aliyesikiliza mahojiano idhaa ya BBC jana atakubaliana nami kuwa Spika wa Bunge ndiye mwenye kubeba lawama zote kwa kuvuruga utaratibu wa ukusanyaji maoni kutoka kwa wananchi,kwani alikataa wajumbe wa kamati ya Bunge waliopewa majukumu ya kukusanya maoni hayo kutokwenda mikoani kwenye kanda 10 (kwa mujibu wa Lisu) kukusanya maoni ya wananchi juu ya muswada huo kwa madai kuwa hawawezi kufanya hivyo kwa kuwa yeye (Spika) alikuwa nje ya nchi.Hata hivyo pamoja na muswada huo kubadilishwa lugha kama ilivyoelekezwa na Bunge, wananchi hawajapewa nafasi tena ya kuujadili ukiacha nafasi ya mwanzo ile iliyotolewa kwenye vituo vitatu yaani Dodoma,Dar na Zaznzibar,kwa upand wake mbunge wa ccm Rweikiza ambaye pia
alikuwemo kwenye kamati ya kukusanya maoni amesema wabunge walichukua maoni ya wananchi na kuyaleta kwenye kamati kwa ajili ya kuwa incorporated katika muswada huo jambomambalo tundu lisu alipinga kwa madai kuwa kamati hiyo haikuwa kuketi mpaka ilipokabidhiwa muswada huo oktoba 24 yaani wiki 2 kabla ya kuanza bunge ukiwa na mabadiliko mengi likiwemo suala la lugha. Kwa mujibu wa Lisu ni muswada huo huo ndio sasa umewasilishwa Bungeni kusomwa mara ya pili jambo ambalo ni kinyume na utaratibu. Ndio maana majaji wastaafu,wanaharakati na wadau mbalimbali walishauri usomwe mara ya kwanza kitu. Maoni yangu mimi tukiacha ushabiki mtu mwenye kutafakari sawasawa hapa CCM imewadharau wananchi sanaaaaaaaaaa!!!!! Kinachofanyika sasa ni kwa wabunge wa CCM kutetea ili wasikiangushe chama chao pia kwa CUF kutetea ili wasivunje ndoa yao ndio maana Hamadi anakwepa point na kuingiza mambo ya madai kuwa
wazanzibar wametukana,Nyerere katukana n.k lakini hawataki kujadili nini ambacho spika alisema juu ya ukusanywaji maoni baada ya kubadilishwa lugha kwa muswada au ni kwa nini muswada huo ulipelekwa kwenye kamati oktoba 24?ukiwa na mabadiliko ambayo wananchi hawajayaona?.
 
Ngoja nikupe uzoefu wa Kenya:
Kule kenya Rais alipewa nafasi kumi za kuteua, asasi za kiraia na makundi mbalimbali wakateua wawakilishi wao (kulingana na vigezo na sifa zilizoainishwa) na wote hao walienda kuthibitishwa bungeni. Hiyo ni tofauti kabisa na hii ya Rais kuteua wajumbe wa tume ambao uteuzi wake ni wa mwisho hakuna wa kuhoji.

Hadidu za rejea ziondolewe mikononi mwa rais kwani tume haipaswi kuwajibika kwa rais bali kwa wananchi. Hadidu za rejea ziwe sheria katika muswada ili wananchi wawe na sauti katika matokeo ya mchakato huu.

Hayo ni machache tu!

zaidi kuh uzoefu wa kenya: Ufungamano group was established in Dec 1999 specifically to campaign against a goverment controlled constitutional review process and to agitate for people driven constitutional reform. It had well over 50 stakeholders including human rights organization (KHRC,NCEC,4C's),several faith groups,women organization as well as grassroot human rights groups. Eventually through a presidential initiative the group was merged with parliamentary team leading to the Bomas process- source Kenya constitution History.
 
Back
Top Bottom