Hamad Rashid (CUF) na Ole Sendeka on TBC1

kanyagio

JF-Expert Member
Dec 10, 2009
1,021
365
Naona hamad na ole sendeka wapo live on tbc wamenza kumshukuru jk kuleta muswada. Sasa wanaongelea suala la zanzibar katika katiba
 
Naona ole sendeka anasema kuwa lisu alisema kuwa nyerere alimomonyoa vipengele katika mambo ya muungano na hivyo eti lisu alimtukana nyerere.
 
Sasa wanaongelea madaraka ya raisi katika muswada huu. Hamad anatetea hayo madaraka, anadai eti watu wana wasiwasi.
 
Hamad anaongelea uteuzi wa tume ya katiba. Anatetea rais kufanya uteuzi wawajumbe na kutengeneza hadidu rejea. Eti katiba ya sasa inampa madaraka kufanya teuzi mbalimbali bila kushirikisha bunge. Upupu tu. Naona cuf wameamua kuwa ccm b kabisa kabisa.

Wame break sasa kupata habari za michezo wakirudi ole sendeka naye ataongelea madaraka ya rais katika muswada
 
Nasikiliza hapa Hamad Rashid anatia kinyaa. Anatetea madaraka ya Rais kwamba katiba ya sasa ndio inayompa madaraka makubwa. Ndio maana tunataka katiba mpya isiyompa rais madaraka makubwa na lazima tuanze hapa kumnyang'anya madaraka.

Hivi CUF wamepewa nini jamani wamekuwa wapumbavu sasa. Wanatetea kuliko hata ccm yenyewe. Mtu mwenye akili ndogo kabisa atajua kuwa rais ana mamlaka hata ya kubadilisha draft kupitia baraza la mawaziri na kwa vile yeye ndie anateua wabunge wengi wa bunge la katiba, kupitia bunge la katiba anaweza kubadilisha kabisha maoni ya wananchi.

Ni zezeta tu ambaye hawezi kuona kuwa katiba hiyo italinda maslahi ya ccm na hivyo hakuna sababu ya kuwa na mchakato
 
Unajua ukiangalia kwa umakin wabunge wa cuf wako sawa hasa wale wanaotoka znz,ule muswada umewapendelea sana so itakua ngum kuupiga simply 7bab ya interest za nch yao,tatizo ni kwa haya mambumbu ya bara hata hayajitambui yakiona Hamad Rashdi kagonga meza na yenyewe pia yanagonga.sava.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Wamerudi sasa ole sendeka anaongea sheria ikipitishwa inaanza kutumika dec 1 2011:

Eti ni sawa rais kuteua wajumbe kwa kuwa sifa za wajumbe zimeainishwa. Sasa jaman sis tumeona uteuzi mbovu wa jk duh duh si atajaza watu watakao kuwa pro CCM.

Anashangaa watu kuhoji madaraka ya rais
 
Wamerudi sasa ole sendeka anaongea sheria ikipitishwa inaanza kutumika dec 1 2011:
eti ni sawa rais kuteua wajumbe kwa kuwa sifa za wajumbe zimeainishwa. Sasa jaman sis tumeona uteuzi mbovu wa jk duh duh si atajaza watu watakao kuwa pro ccm.
Anashangaa watu kuhoji madaraka ya rais
Sasa nani ateue?.....
Mbona hamjibu hili?
 
Hamad Rashid ni mfanyibiashara magumashi ambazo zote zinaitaji fadhila ya serikali ili ziweze kuendelea.
Ole Sendeka anashangaza sana
 
Naona ole sendeka anasema kuwa lisu alisema kuwa nyerere alimomonyoa vipengele katika mambo ya muungano na hivyo eti lisu alimtukana nyerere.

Tatizo la Ole Sendeka ni uelewa mdogo. Na pengine hii inachangiwa na elimu ndogo aliyonayo na pia tabia mbaya iliyozoeleka ccm ya kutosoma. Wabunge wa ccm wanaishi kwa semina elekezi. Na kadiri anazidi kuongea huyu Ole Sendeka ndiyo anatufanya tuzidi kubaki midomo wazi - ujinga mtupu!

Na huyo Hamad Rashid anasifia adidu rejea, hivi ana habari cha majaji wastaafu kimepinga hizo adidu rejea? Na pia anaelewa baraza la wawakilishi Zanzibar hawakuabalini na huo muswada kusomwa bila kushirikisha wananchi? Wote Ole Sendeka na Hamad Rashid hawajiulizi kwa nini Samweli Sitta (mwanasheria) amekaa kimya?
 
Hamad anaongelea uteuzi wa tume ya katiba. Anatetea rais kufanya uteuzi wawajumbe na kutengeneza hadidu rejea. Eti katiba ya sasa inampa madaraka kufanya teuzi mbalimbali bila kushirikisha bunge. Upupu tu. Naona cuf wameamua kuwa ccm b kabisa kabisa.
Wame break sasa kupata habari za michezo wakirudi ole sendeka naye ataongelea madaraka ya rais katika muswada

TBC1 at it again, wamefanya kusudi kuwaalika watu wa upande mmoja, halafu watu wenyewe ndio wale wale.

Mmoja ana chuki na husda dhidi ya chadema kwa kupokwa tonge la KUB wakati mwengine zero brain, ni kulipuka tu!
 
Ina maana wote hawa wamekuja kutoa ufafanuzi wa kama wanajadili Katiba Mpya au mchakato?

Inakuwaje wanafanana mawazo (CCM na CUF)?
 
Asilimia 78 ya watanzania walikataa vyama vingi. Unaikumbuka ile referrendum?
Nakumbuka sana!

Who influenced the president?

Iitishwe kura ya maoni sasa ya CCM ifutwe au iendelee, au iulize tuwe na vyama vingi vya siasa au turudi chama kimoja?

Unatarajia kura hiyo ikiitishwa watanzania watachagua lipi?
 
Haiwezekeani rais ateue watu 550 peke yake kwa kushauriana na rais wa zenji
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom