18 JANUARY 2024
Hamad Masoud Hamad katibu mkuu wa CUF asema hakuna haja ya kuweka mbinyo miswada ya sheria ya uchaguzi na sheria ya Tume ya Uchaguzi zibadilishwe kupitia maandamano ya amani yaliyoitishwa na CHADEMA 24 January 2024.
Katibu mkuu wa CUF alipobanwa zaidi kuwa kiuhalisia bunge ni la chama kimoja dola kongwe yaani CCM, je chama cha CUF wanauhakika gani CCM yenye wabunge wengi ktk bunge na kamati ya kudumu ya Bunge masuala ya utawala, sheria na katiba wanaweza kusikiliza maoni ya wasio wanaCCM na wadau.
Katibu mkuu wa CUF Bw. Hamad Masoud Hamad alipobanwa kuwa anatarajia kitu tofauti kutoka CCM, akasema kwa kuwa chama hicho dola kongwe CCM kina wabunge zaidi ya 97% ya wa wabunge wote katika bunge la 2020 hategemei CCM kusikiliza maoni ya vyama ya upinzani na wadau walio nje ya bunge la sasa, akasema ingekuwa bunge la sasa ni kama la mwaka 2015 angekuwa na matumaini ya kitu tofauti maana wapinzani ndani ya bunge walikuwa zaidi ya 40% hiyo ingeleta majadala mzito.
CUF YASEMA SUBIRA ITUMIKE, MAANDAMANO YASITISHWE HADI BUNGE LIPITISHE MISWADA YA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA UCHAGUZI NA TUME YA UCHAGUZI