Gray Mgonja: Kufikishwa Mahakamani na matokeo yake

Bado siamini kama kweli hizi kesi za mafisadi zitazaa matunda yoyote ya maana ingawa vile vile sina sababu ya maana ya kutoiamini serikali hii kuwa inafanya ukweli.

Network ya mafisadi hapa kwetu imekuwa kama vile taa za krismas, kuwa ukiunguza moja basi kuna nyingine kadhaa pia hazitawaka. Tatizo liko pale kwenye ambazo hazitawaka, kwani inawezekana mojawapo ndiyo yenye rangi nzuri sana, ambayo hutaki izimike.
 
Mzee wa V. G. Cent ( Andrew Chenge) naye alikamatwa, akazirai. Nikipata habari zaidi na kuzithibitisha nitawarushia.

Dah inawezekana kesi hizi ni za kweli na zinawatisha mafisadi kama kweli mzee wa vijisenti alizirai. Vipi alilowanisha au kuchafua suruale aliyovaa?
 
nyakati hizi, viwanda vya bia na soda vinatengeneza sana fedha, si kwa sababu ya x-mass, idd n.k ila kwa haya!!!! wale wa kuvuta bangi Mungu awasaidiea msivute bangi kwa furaha, wale wa bia please, msinywe kwa furaha. heri tukutane pamoja tucheze mdundiko wa kizaramo tukaendela tena kujadili na kuwasaka wengine, ili tusilewe kwa mvinyo tukaona kazi imeisha ndio kwanza inaanza, mafisadi wakubwa na wabaya nji hii bado hatuwajui! wengi mno!

waberoya
 
Bado siamini kama kweli hizi kesi za mafisadi zitazaa matunda yoyote ya maana ingawa vile vile sina sababu ya maana ya kutoiamini serikali hii kuwa inafanya ukweli.

Network ya mafisadi hapa kwetu imekuwa kama vile taa za krismas, kuwa ukiunguza moja basi kuna nyingine kadhaa pia hazitawaka. Tatizo liko pale kwenye ambazo hazitawaka, kwani inawezekana mojawapo ndiyo yenye rangi nzuri sana, ambayo hutaki izimike.

unajua watu wameshalishwa limbwata la kesi za kimaigizo na sasa focus yote hiko huko Kisutu. Issue za msingi zimeachwa. Tunashindwa kujiuliza je haya ni maandalizi ya 2010? nini Kimemtisha JK hadi kuamua sasa kuyavalia njuga vilio vya wananchi? is it a mere coincidence? au ni kujiweka katika mazingira mazuri akiteleza 2010 awe juu katika kinyang'anyiro cha Dr. Mo ( awezo kuungana na kina Chisano wa Msumbiji katika kupata pensheni ya nguvu). Je ni changa la macho? nategemea pundits wa humu ndani haya ndo yatakuwa sehemu ya uchambuzi wetu wa hizi kesi.

Maana yake haya mauzo hayakuanza leo, so why now? tena wanawaleta kwa mafungu ili mfunge mwaka mkishangilia na kusahahu maisha magumu na kufilisika kwa mashirika yaliyobinafishwa chini ya JK Na Nkapa. Mfano Air Time Cancelled Limited ( ATCL) ambayo technically ni muflisi.

Judge of a tree by its fruit, not by its leaves

Shadow
 
..my gut feeling ni kwamba kati ya mafisadi kuna watakahukumiwa vifungo jela.

..off course wengine watanusurika lakini siyo wote.

..Kiula alinusurika, lakini Mlingwa alihukumiwa miaka 6 kwa kuidanganya mahakama.

NB:

..Naziri Karamagi hatashitakiwa na Raisi Kikwete. labda mtawala anayekuja.
 
It's true kuna watako shinda/kusindwa kesi, BUT what the 4th Phase goverment is doing is setting a precidence, Kuwa kama itatokea huko mbeleni ukapewa dhamna ya uongozi basi ujue una dhamana ya taifa na si familia yako!!!!

Jamani, tulifika pa baya mahali ambapo mkuu wa polisi anaongoza majambazi badala ya kulinda maisha na mali za watu!!!!! Je huyo huyo aliye na dhamana ya hazina yetu ulitegemea angefanyaje kama si kujichotea tu?
 
Huoni kama tumefika mahali kama ni gari lazima ishushwe injini na kusukwa upya mfano huko polisi ulipopagusia!
 
Huoni kama tumefika mahali kama ni gari lazima ishushwe injini na kusukwa upya mfano huko polisi ulipopagusia!

Mzee wamepasuka, ... umesahau kuwa wata walikuwa wanaingia benki cku watakayo na mtutu ngwi ...? haiwezekani uhalifu usiwepo kabisa lakini kuko shwari
 
Kama PCCB wanahusika ni kwa nini hawawi charged with corruption ?

Na ni kwanini ofisi ya DPP ndio inashitaki na sio PCCB ? Huyu DPP analeta kesi zinazo sound kama vile administrative misjudgement zilizosababisha hasara. Hawashitaki kwamba wamejineemesha na rushwa. Why not? Kama hakuna rushwa why involve PCCB then?

Halafu wanawarundika wote kwenye criminal complaint moja, wakati wengine wako Hazina wengine Madini, ina maana mmoja akikutwa not guilty basi wote rrrrrrrrrrrrr... not guilty!

Na kama walishirikiana mbona hakuna conspiracy charges ?

Inawezekana kuna usanii hapa.

Kuhani nakubaliana na wewe moja kwa moja..Excellent analysis..Mjadala huu unatakiwa ubase kwenye maswali hayo hapo juu...Usanii ni lazima upo ama la sivyo wajibu ni kwanini uchunguzi ulisimamiwa kama uchunguzi wa rushwa na ushahidi ukapatikana lakini eti JK na PCCB wanadai DPP ndiyo atakayefungua kesi...Kesi zenyewe hakuna madai ya rushwa...Usanii usanii...
 
Huoni kama tumefika mahali kama ni gari lazima ishushwe injini na kusukwa upya mfano huko polisi ulipopagusia!

Inamaana huoni juhudi za polisi au na we ndio wale wale wanaoyasema maovu tu mazuri mnayakali kimya?? kwa kiasi kikubwa sana Nchi imetulia wimbi la ujambazi limetulia na hata wadokozi nao wametulia kwa kiasi kikubwa sana, Ni vyema tukajenga mazoea ya kushukuru pale kwenye maendeleo si kukurupuka na kulaumu tu kila kukicha alafu tunategemea nchi yetu iendelee mwe!
 
Kuhani na JMushi 'mmeua'!

mmenifungua macho nianze kuliangalia swala hili kivingine! du ama kweli! "You can fool some people sometime......................"

waberoya
 
Ni vyema tukajenga mazoea ya kushukuru pale kwenye maendeleo si kukurupuka na kulaumu tu kila kukicha alafu tunategemea nchi yetu iendelee mwe!

Nani amesema kuwa maendeleo hujua kwa kushukuru na kwamba kulaumu hufifisha maendeleo, nadharia gani ya maendeleo hiyo?
 
Kulikua na zile tetesi kwamba muungwana anaitwa OP ikamaanisha wenye uwezo wao walikua wanaandaa mpango wa kumwondoa 2010, naona hapa ajiandaa kukabiliana na nguvu za fedha (ambazo ndizo zenye uwezekano mkubwa wa kumuondoa 2010).
Kwa staili (hopefully sio maigizo) muungwana atajenga nguvu ya umma nyuma yake, then 2010 kumwondoa itakua impossible. Lakini ikiwa hii ni maigizo..........the big boy shall be in big trouble when 2010 pops in.

Tuko pamoja mkuu...Bottom line tutajuwa tu...Kama JK anafanya kweli basi kilichobakia ni kuunda sirkali ya mseto na kuanza upya ujenzi wa Taifa jipya lenye malengo.
 
Nani amesema kuwa maendeleo hujua kwa kushukuru na kwamba kulaumu hufifisha maendeleo, nadharia gani ya maendeleo hiyo?

Mkulu wanee kitila ni nduwe utakile uga Polisi hawafanyi kazi nzuri?? concept yangu hapo ni kwamba... tupunguze kulalamika hata pasipo na sababu za msingi, kama tutabakila kulaumu tu sidhani kama tutaona mazuri yafanywayo maana tayari tutakuwa tumeshajenga imani kuwa hawa ni watu wa kutudanganya tu
 
Waga, walikuja kwa mbwembwe na akina Komba wao, wakaomba kura(siyo kula) wakajieleza tukawafanyia interview(kujinadi) tukawabeba juu, wengine hawakulala! JK ALIZIMIA JANGWANI! alikuwa anatafuta kututumikia watanzania, tumempa ofisi, mamlaka, jeshi, fedha zetu, mali asili, kila kitu!!!!!! kila kitu!!!!!! anachotakiwa ni kuilinda katiba na kufanya tulilomwambia kufanya, mkuu Masihi amesema miaka 2000 iliyopita, kiongozi ni mtumishi!

Dhana ya kuwasifu watumishi wetu haipo!!! walitakiwa kufanya hivi bila shinikizo la wafadhili, mbaya zaidi utawasifu pale hii kitu isipokuwa sanaa!!!!

sanaa ni ya ajabau sana, unapigiwa makofi hapohapo, na unazomwewa hapohapo, na watanzania wengi wanapenda wasanii, msanii akiwa jukwaani akichekesha au akiboa, siku nyingine akikuita tena ukumbini unaenda tena!! umesahau!

waberoya
 
Date::12/15/2008
Gray Mgonja kortini ashindwa dhamana apelekwa rumande Keko
*Mwingine aongezwa katika orodha ya ufisadi wa EPA

Na Nora Damian
Mwananchi

Mahakama ya Kisutu Jumatatu yalikuwa eneo la pilikapilika kwa mara nyingine baada ya aliyekuwa katibu mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Grey Mgonja kupandishwa kizimbani akituhumiwa kutumia vibaya ofisi na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh11 bilioni, huku mfanyabiashara Jonathan Munisi pia akipandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuiba fedha kwenye Akaunti ya Malimbikizo ya Madeni ya Nje (EPA).

Munisi, ambaye alikuwa mfanyakazi wa Benki Kuu (BoT) amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuiba Sh2.6 bilioni kutoka kwenye akaunti hiyo iliyokuwa kwenye benki hiyo na kufanya idadi ya watuhumiwa waliopandishwa kizimbani hadi sasa kufikia 21.

Lakini macho ya wengi kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu yalikuwa kwa katibu mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha, Mgonja ambaye alipandishwa kizimbani kwa tuhuma za kutumia vibaya ofisi yake na kuisababishia serikali hasara hiyo.

Mtendaji huyo mkuu wa serikali alilazimika kwenda kulala mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti yote ya dhamana, likiwemo la kuwasilisha fedha taslimu au mali zenye thamani ya Sh5.9, ikiwa ni nusu ya fedha anazodaiwa kuisababishia serikali hasa.

Mgonja, akionekana kufedheheka, alifikishwa mahakamani hapo saa 7:00 mchana akiwa kwenye gari aina ya Toyota Rav 4 yenye namba T 123ATW huku akiwa amevalia shati la rangi nyeupe na suruali ya rangi ya bluu. Alipelekwa chumba cha mahabusu hadi saa 8.28 mchana alipopandishwa kizimbani.

Wakati akiwa mahakamani hapo Mgonja alionekana kujishika tama mara kwa mara na wakati mwingine kuinama chini.

Wakili wa serikali, Fredrick Manyanda alimsomea mashtaka nane mtuhumiwa huyo mbele ya Hakimu Mkazi Hezron Mwankenja. Mgonja alikana mashitaka yote.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa kati ya Desemba 18 mwaka 2003 na Novemba 15
mwaka 2005, akiwa katibu mkuu wa Wizara ya Fedha, alitoa taarifa za serikali (government notice) ambayo iliipa msamaha wa kodi kampuni ya M/S Alex Stewart kinyume na ushauri uliotolewa na Mamlaka ya Mapato (TRA).

Mgonja anadaiwa kuwa Oktoba 18 na 19 mwaka 2003 alitoa taarifa ya serikali namba 423, Desemba 19 mwaka 2003 taarifa ya serikali namba 424, Oktoba 15 mwaka 2004 taarifa ya serikali namba 497, Oktoba 14 na 15 mwaka 2004 taarifa ya serikali namba 498, Novemba 15 mwaka mwaka 2005 taarifa ya serikali namba 377 na Novemba 15 mwaka 2005 taarifa ya serikali namba 378.

Mtuhumiwa huyo pia anadaiwa kuwa kati ya mwaka 2003 na 2007, kwa makusudi na
kwa kutokuwa makini, alisaini taarifa hizo ambazo ziliipa unafuu kampuni hiyo kulipa kodi, kitendo ambacho inadaiwa kiliisababishia serikali hasara ya Sh11,752,350,140.

Hata hiyo, wakili huyo wa serikali alidai mahakamani hapo kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Baada ya hoja za upande wa mashitaka, kiongozi wa jopo la mawakili watano wanaomtetea Mgonja, likiongozwa na Profesa Leonard Shaidi alidai kuwa mashitaka na kiwango cha pesa kilichotajwa yanafanana na ya mawaziri wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona na kwamba wanashangaa kwanini hawakufikishwa mahakamani pamoja.

Akijibu hoja hizo, Wakili Manyanda wa serikali alidai kuwa upelelezi ulikuwa bado haujakamilika na kwamba wanaweza wakawaunganishwa.

Baada ya kusikiliza hoja hizo, Hakimu Mwankenja aliahirisha kesi hiyo kwa dakika 15 hadi saa 9.30 mchana wakati alipotoa masharti ya dhamana.

Mwankenja alitoa masharti manne ya dhamana kwa mshitakiwa huyo akimtaka kuwasilisha fedha taslimu au hati za mali zenye thamani ya Sh5.9bilioni.

Pia mshitakiwa huyo ametakiwa kuwasilisha hati yake ya kusafiria, asitoke nje ya jiji la Dar es Salaam bila kuwa na kibali maalum cha mahakama, na awe na wadhamini wawili watakaosaini dhamana ya Sh 5.9 bilioni.

Mshitakiwa huyo alitimiza sharti moja tu la kuwa na wadhamini wawili ambao walikuwa wafanyakazi wenzake, Ramadhan Mlinga na Delfina Mlaki, lakini akashindwa kutimiza masharti mengine yaliyowekwa na mahakama na hivyo Mgonja kulazimika kupelekwa rumande mpaka atakapotimiza masharti hayo.

Kesi hiyo imehairishwa Desemba 29 mwaka huu kwajili ya kutajwa tena.

Kabla ya kufikishwa mahakamani hapo, ulinzi uliimarishwa. Zaidi ya polisi 10 waliwasili mahakamani saa 2:00 asubuhi, wakiwa na mbwa wawili. Walitumia gari la polisi lenye namba PT 0948.

Mara baada ya kesi hiyo kumalizika mtuhumiwa huyo alisindikizwa kuelekea rumande na mbwa hao pamoja na gari ya polisi iliyokuwa imetanguliaa mbele.

Kufikishwa mahakamani kwa katibu huyo mahakamani kunafanya idiadi ya vigogo waliofikishwa mahakamni hapo kwa tuhuma za kutumia vibaya madaraka yao na kuisababishia serikali hasara, kufikia watatu.

Tayari mawaziri wawili wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona wameshafikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutumia vibaya ofisi na kuisababishia serikali hasara. Wapo nje kwa dhamana.

Katika anga za EPA, Munisi anadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 25 mwaka 2006 mkoani Arusha.

Wakili wa serikali Boniface Stanslaus alidai mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ady Lyamuya kuwa mtuhumiwa alijipatia fedha hizo kupitia kampuni ya Njeki Enterprises akidanganya kwamba amenunua deni kutoka kampuni ya E. Itoh ya nchini Japan.

Hata hivyo mshtakiwa alikana kosa na kutakiwa kutoa fedha taslimu Sh1.3bilioni na kuwa na wadhamini wawili kwa ajili ya dhamana yake, lakini masharti hayo yalionekana kuwa magumu kwa mtuhumiwa huyo na alipelekwa kwenda kulala mahabusu hadi Desemba 30 mwaka huu.

Watuhumiwa wa wizi kwenye akaunti ya EPA walianza kufikishwa mahamakani Oktoba mwaka huu na mfanyabiashara maarufu nchini Jeetu Patel ndiye aliyekuwa mtuhumiwa wa kwanza kupanda kuzimbani.

Jeetu na wenzake walikaa rumande kwa majuma kadhaa kabla ya kutolewa kwa dhamana ya mamilioni ya fedha ambayo awali iionekana kuwa ngumu kuipata.
 
Waga, walikuja kwa mbwembwe na akina Komba wao, wakaomba kura(siyo kula) wakajieleza tukawafanyia interview(kujinadi) tukawabeba juu, wengine hawakulala! JK ALIZIMIA JANGWANI! alikuwa anatafuta kututumikia watanzania, tumempa ofisi, mamlaka, jeshi, fedha zetu, mali asili, kila kitu!!!!!! kila kitu!!!!!! anachotakiwa ni kuilinda katiba na kufanya tulilomwambia kufanya, mkuu Masihi amesema miaka 2000 iliyopita, kiongozi ni mtumishi!

Dhana ya kuwasifu watumishi wetu haipo!!! walitakiwa kufanya hivi bila shinikizo la wafadhili, mbaya zaidi utawasifu pale hii kitu isipokuwa sanaa!!!!

sanaa ni ya ajabau sana, unapigiwa makofi hapohapo, na unazomwewa hapohapo, na watanzania wengi wanapenda wasanii, msanii akiwa jukwaani akichekesha au akiboa, siku nyingine akikuita tena ukumbini unaenda tena!! umesahau!

waberoya

Asante sana mkuu waberoya,, Mang'ana Gasarikilr( hahahaha) lakini kwa hii post yako unataka kuniambia hata polisi wanavyokamata majambazi na kufanikiwa kuwatuliza hawa jamaa kwa kiasi kikubwa nayo ni sanaa?? hata watu wanasafiri kwa amani sasa hivi huwezi kusikia basi limetekwa ikitokea nii mara moja kwa mwaka
 
Tuko pamoja mkuu...Bottom line tutajuwa tu...Kama JK anafanya kweli basi kilichobakia ni kuunda sirkali ya mseto na kuanza upya ujenzi wa Taifa jipya lenye malengo.

Akifanya hivi mvua kubwa itanyesha siku 40 mchana na usiku, tetemeko la ardhi litatikisa Tanzania, Mlima Kilimanjaro utaanguka na kutengeneza creta kama ya ngorongoro!wafu wa kale wataonekana kwa muda kila kona ya Tanzania! akiwemo Nyerere!

Nitakuwa radhi kila siku asubuhi kumpigia kiwi kiatu chake, na kumyoshea suti yake freely, tu kama akifanya hivi,na hapa sifa zote mnazompa ndipo nitampa!

Au aanze na Kagoda kwanza kabla ya yote! tumuone kama mwanaume!

Otherwise ni kupiga upepo siku ziende! hamna lolote hapa!
 
Asante sana mkuu waberoya,, Mang'ana Gasarikilr( hahahaha) lakini kwa hii post yako unataka kuniambia hata polisi wanavyokamata majambazi na kufanikiwa kuwatuliza hawa jamaa kwa kiasi kikubwa nayo ni sanaa?? hata watu wanasafiri kwa amani sasa hivi huwezi kusikia basi limetekwa ikitokea nii mara moja kwa mwaka

Supported!

Kama umekaa kwenye hiyo kona, basi kila mmoja asifiwe! tuanze na wafagizi maofisini, , mamesenja, kila mmoja kwa nafasi yake, madobi, wapiga kiwi, wauza samaki, wauzaji wa karanga, maji ya Azam, makondakta, nasema kila mmoja wengine malizia list kubwa mno........ !!

Hehehe am out.............
 
Back
Top Bottom