Gray Mgonja: Kufikishwa Mahakamani na matokeo yake

JF= the MOB... if the law actually listened to ubwabwa ambao watu wanaongeaga humu.. society wud be very dangerous..lol
 
...Nakiri ukihiyo kwa maana uliyoiweka hapo kwani nilipitia LL.B ya kuzugia tuu hata kuipata degree yenyewe ni kama kuiokota tuu baada ya Supp nyingi na DISCO kadhaa ikiwemo kurudia mwaka.
Sentensi hazina ukinzani wowote one needs only to be a deep thinker to grasp the meaning. Sorry you are not.

Sasa kama wewe ni ``deep thinker`` mbona ulikuwa unafeli feli ma supplementary exams mpaka kurudia rudia miaka ? Au ni Kihiyo unaezuga kwamba ulisoma wakati darasani ulikuwepo kama haupo ?

Kitendo cha kutetewa na mmoja wa walimu wangu wa sheria pale Mlimani, Prof. Shaidi ni uthibitisho tosha kuwa the case against him has no merit

... a good example, ukisikia kesi yoyote inatetewa na Prof. Issa Shivji, ujue kesi hiyo ni ngumu

Hiyo gibberish uliuoandika hapo ndio sense ya mwanasheria ``deep thinker`` hiyo? Acha kujichora chora humu wewe pseudo.
 
Mkuu FMES kwanza heshima mbele.
Pili, nimekubali yaishe na tusubiri matokeo.
Yote mliyoyasema nimeyakubali naomba mjadala kuhusu comments zangu ufungwe na tuendelee na hoja husika. Please no more quoting me
Natanguliza shukrani. Tuendeleze jamvi.

Hongera kwa kuonyesha ukomavu mkuu, safi sana!
 
Mgonja aunganishwa na Mramba na Yona
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam, leo imemuunganisha aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Grey Mgonja, katika kesi ya watuhumiwa wengine wa ufisadi, Basil Pesambili Mramba na Daniel Yona.


Wote hawa wanakabiliwa na tuhuma za kutumia vibaya madaraka yao na kulisababishia taifa hasara ya takribani bilioni 11.Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Hezron Mwankenja alifikia hatua hiyo kufuatia ombi la upande wa utetezi katika kesi ya Mgonja unaoongozwa na Profesa Leonard Shaidi, kuiomba mahakama hiyo kumuunganisha mteja wake na akina Mramba na Yona kwa kile alichodaiwa kuwa kesi hizo zinafanana.

Source: JIACHIE
 

Attachments

  • Washitakiwa.jpg
    Washitakiwa.jpg
    32.5 KB · Views: 193
Mgonja, Mramba,Yona sahani moja
Mwandishi Wetu
Daily News; Friday,January 02, 2009 @20:16
Kesi iliyokuwa inamkabili Katibu Mkuu wa zamani wa Hazina, Gray Mgonja, imefutwa jana, badala yake mshitakiwa huyo sasa ameunganishwa katika kesi inayowakabili mawaziri wawili waandamizi wa zamani Basil Mramba na Daniel Yona.

Kutokana na Mgonja kuunganishwa kwenye kesi hiyo ya kutumia vibaya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 11.7, washitakiwa hao waliomba kurudishiwa sehemu ya mali zao walizowekeza kortini kama dhamana.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam haikuwa na pingamizi na iliamua washitakiwa watakuwa nje kwa dhamana ya Sh bilioni mbili kila mmoja au kuwasilisha hati yenye kiasi hicho cha fedha kutokana na idadi yao kuongezeka.

Awali, Mgonja alikuwa nje kwa dhamana ya Sh bilioni 5.9 kutokana na kushitakiwa peke yake na aliwasilisha hati zenye thamani ya Sh bilioni 6.2. Kwa upande wa Mramba na Yona, walikuwa nje kwa dhamana ya Sh bilioni 2.9.

Kutokana na uamuzi huo, washitakiwa watachagua hati ambazo watapenda kuziondoa mahakamani. Tayari Mgonja ameshaomba aondoe hati ya nyumba ya kitalu 29 iliyoko Adda Estate ya thamani ya Sh bilioni 1.7 na hati ya kitalu namba 80 iliyoko Mikocheni yenye thamani ya Sh bilioni mbili.

Hakimu Mkazi Hezron Mwankenja alisema masharti mengine ya dhamana kama kutoruhusiwa kutoka nje ya Dar es Salaam, kukabidhi hati ya kusafiria kwa waendesha mashitaka na masharti mengineyo yatabaki kama yalivyokuwa awali.

Hatua hiyo ya kuunganishwa Mgonja kulifanya upande wa mashitaka kusoma upya mashitaka kwa washitakiwa wote watatu, huku Mramba akiendelea kukabiliwa na mashitaka yote, Mgonja mashitaka manane na Yona akibakiwa na mashitaka sita.

Hata hivyo, mashitaka yaliyosomwa jana na waendesha mashitaka wa Serikali na wale wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), yamepungua kutoka 13 hadi 12. Kesi hiyo itatajwa tena Februari 2, mwaka huu kutokana na upande wa mashitaka kutokamilisha upelelezi wa shauri hilo.

Katika hatua nyingine, Yona na Mramba wameiandikia barua mahakama kuomba waruhusiwe kusafiri nje ya Dar es Salaam. Yona ameomba siku saba kuanzia leo ili asafiri kwenda kwao Same kuwaona wazazi wake ambao wanaumwa.

Mramba ameomba kusafiri kwenda jimboni kwake kuanzia leo hadi Februari mosi ili kutembelea wapiga kura wake. Pia ameomba aruhusiwe kusafiri kwenda katika vikao vya Bunge Dodoma. Bado hajaruhusiwa uamuzi utatolewa Jumatatu.

Mramba na Yona, wote waliowahi kuongoza wizara nyeti ya Fedha, wanatuhumiwa kutumia vibaya madaraka yao waliyokuwa nayo kwa kuipendelea Kampuni ya Alex Stewart (Assayers) ya Uingereza kwa kuipa mikataba minono na baadaye kuisamehe kodi.

Mkataba unaotajwa katika kesi hiyo ni wa kukagua hesabu za kampuni zinazochimba dhahabu nchini; bila kufuata sheria za manunuzi ya umma. Baadaye washitakiwa hao wanadaiwa kuiongezea mkataba wa miaka miwili kampuni hiyo bila kufuata taratibu.

Makosa yanayowahusisha vigogo hao wawili ni ya kutumia vibaya madaraka kwa kusaini na kuingia mkataba na kampuni ya ukaguzi wa hesabu kwenye migodi ya dhahabu nchini kinyume cha sheria ya manunuzi.

Kosa hilo la kuingia mkataba na kuiongezea mkataba kinyume cha taratibu wanadaiwa kulifanya kati ya Juni 14, 2005 hadi Juni 23, 2007.

Kosa la tatu pia linawahusu washitakiwa wote watatu ambao wanadaiwa kati ya Machi 2005 na Mei 28, 2005 wakiwa mawaziri walitumia vibaya madaraka yao kwa kuiachia kampuni hiyo kujiongezea mkataba.

Katika shitaka hilo inadaiwa viongozi hao walimwachia Dk. Enrique Segura wa Alex Stewart kukamilisha mkataba wa kujiongezea miaka miwili kabla ya timu ya serikali kufanya majadiliano juu ya suala hilo.

Washitakiwa hao pia wanadaiwa kati ya Machi na Mei 2005 wakiwa mawaziri, waliliachia suala la udhibiti wa madini ya dhahabu kufanywa kienyeji na kampuni hiyo bila kulipeleka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama ilivyoamriwa na timu ya majadiliano ya serikali.

Upande wa mashitaka ulidai kuwa uamuzi wa mawaziri hao uliisababishia Kampuni ya Alex Stewart kuongezewa mkataba wa miaka miwili kabla hata ya suala la ada kuafikiwa na pande zinazohusika pamoja na masuala mengine ya mkataba.

Shitaka la kusababisha hasara ya Sh bilioni 11.7 linawahusu washitakiwa wote watatu ambao wanadaiwa kufanya kosa hilo kati ya Juni 2003 na Mei 28, 2005 wakiwa mawaziri na Katibu Mkuu wa Hazina katika Serikali ya Awamu ya Tatu.

Shitaka la tano linamhusu Mramba na Mgonja wanaoshitakiwa kwa kudharau ushauri uliotolewa na Mamlaka ya Mapato (TRA) wa kuwataka wasiruhusu msamaha wa kodi kwa Kampuni ya Alex Stewart. Mramba na Mgonja pia wanashitakiwa walitoa msamaha wa kodi kwa kampuni hiyo kinyume cha ushauri wa TRA.

Wanadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 10, 2003 na kutoa tangazo la serikali namba 423/2003 la kutoa msamaha wa kodi zote zilizokuwa zinalipwa na kampuni zilizokuwa zinaisambazia vifaa Kampuni ya Alex Sterwart kinyume cha ushauri wa TRA.

Katika kosa lingine Mramba na Mgonja wanashitakiwa kuwa Desemba 19, 2003 wakiwa waajiri wa Wizara ya Fedha walitumia vibaya madaraka yao kwa kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni hiyo kinyume na ushauri wa TRA.

Oktoba 15, 2004 Mramba na Mgonja pia wanadaiwa waliipa msamaha mwingine wa kodi kampuni hiyo kinyume cha ushauri wa TRA.

Kosa kama hilo Mramba na Mgonja wanadaiwa kulitenda tena kati ya Oktoba 14 na 15 baada ya kutoa tangazo namba 498/2004 la kuruhusu msamaha wa kodi kwa Kampuni ya Alex Stewart kinyume na ushauri wa TRA.

Katika shitaka la 10 Mramba na Mgonja wanatuhumiwa kutoa msamaha mwingine wa kodi kwa kampuni hiyo. Walitoa msahama huo kupitia tangazo la Serikali namba 377/2005 na kutoa upendeleo huo wa kutolipa kodi kwa kampuni hiyo.

Shitaka la 11 linawahusu Mramba na Mgonja ambao wanadaiwa kutoa msamaha wa kodi kwa Alex Stewart kitendo wanachodaiwa kukifanya Novemba 15, 2005 kupitia Tangazo la Serikali namba 378/2005.
 
Hivi haka kazee kalikuwa kanafanya nini pale hazina? ndo maana wazee wa eac walikasomea albadir. nimetembelea wesite ya hazina majedwali yote yanaishia mwaka 2005! majendwali hayo yanaonyesha New Mwanza hotel, Hotel newafrica bado mali yaserikali. Ukiondoa 11.7m dividend iliyolipwa na mwanza hotel hakuna dividend tuliyopata katika mashirika yote ya umma! je kati ya mashirika 183 ya umma ni mwanza hotel tu iliyopata faida? Hivi vipare vipumbavu tu.
 
Tusihamanike sana na hizi kesi za ufisadi kwa ajili ya hasira na machungu ya umasikini wa nchi yetu. Kuna mafisadi tena mafisadi kweli, watashinda kesi na serikali italipa fidia ya mabilioni mengine. Na kuna kondoo wa kafara miongoni mwa mafisadi, watahukumiwa na watakwenda jela kwa kulinda maslahi ya mafisadi wanene zaidi ambao wanaendelea kutesha kwenye mavogue yao, vioo vyeusi na kiyoyozi kwa kwenda mbele. Only time will tell.

mi siombei hilo.
mi natamani mafisad wote wapate adhabu zinazostahili ikiwemo kurudisha walichotukosesha.

lasivyo wengi wengine wataiga. na hakuna kibaya kama hicho.
watu watakuwa wanatoana jasho na hata roho kugombea nafas ili wakaibe na kupokea rushwa vizur.

dili la kila mtu itakuwa kufisad tu. ikifikia hapo kaz na madili ya halali itakuwa kama sumu
 
Simtetei kwamba Mgonja ni mtu safi maana yale yanayofanyika chini ya kapeti siyajui bali ni mtu ninayemfahamu kwa karibu, amini usiamini ni mtu mwadilifu na naamini yoyote aliyoyafanya yawe mema ama maovu, he did in good faith.

ni uthibitisho tosha kuwa the case against him has no merit bali serikali katika kiherehere chake cha kutafuta kurudisha imani kwa wananchi kwamba iko serious kudeal na madudu yasiyoeleweka na badala yake sasa itaishia kupata aibu.
Hii ni post ambayo kwangu mimi ndio inaongoza kwa kuboa in 2008, ah huu mwaka bwana bora upite tu maana wachekeshaji wapo wengi
Kwa siku hizi za funga mwaka, sio mbaya post yangu ikaongoza kwa kuboa 2008 na ni kweli niliwahi kuwa mchekeshaji siku za nyuma. One good thing is certain, some comedian are teling the truth sometimes. I belive in 'Seek the truth, and the truth will set you free'. Naamini ni ukweli ndio utawadhibitishia umma nani fisadi na nani siye na sio kwa kuwaandika sana hapa JF.
This is the single most ridiculous comment I've ever read in the forum.
............................kweli kabisa.
If its true ndio most ridiculous coments, basi haya ni ya Musa tuu, tusubiri na ya firauni(Pharaoh).
Kusomea sheria sio kuwa mwanasheria.
Wakili ana matter sana kwenye mwenendo wa kesi. Kama kuna wale wenzangu na mimi wa miaka hiyo. Fanya reference ya Wakili Murtaza Lakha.
Kama kumsifia Prof wangu wa chuo ni kosa, tusubiri utendaji wake.
Namalizia kwa kusisitiza nimesema simtetei Mgonja kwa kilichomfikisha mahakani lakini Mgonja ninayemfahamu mimi ni mtu safi.kwa hili naomba tusubiri mahakama itamke vinginevyo.
Kuna mwizi ambaye atakueleza au kukubali kwamba ni Mwizi? kwa nje atakuonyesha ni mtu safi, pili yule unaye mfikiria ni mwizi utakuta si mwizi.
Jamani nilianza kwa kusema simtetei kwa sababu sijui aliyoyafanya yakamfikisha hapo. Nimesema namfahamu Gray Mgonja at personal capacity, he is good man.

Najua watu wana usongo sana na wimbi la ufisadi uliolitafuna taifa letu. Sasa isiwe hata wema tunaowajua maadam wameshitakiwa basi woote ni mafisadi. Kwa nini tuandikie mate wakati wino upo?. Tusubiri matokeo ya kesi ya Mgonja, watakaolia, watalia na tutakaocheka tutacheka.

Baada ya kutoka listi ya makampuni 22 ya ufisadi wa EPA, nakumbuka nilijitokesa nikatetea baadhi ya makampuni kuwa ni watu ninaowafahamu na wamefanya clean deal. Nilishutumiwa hivi hivi. Matokeo yake kesi zimepelekwa mahamani hayo makampuni hayamo.

Sio kila adhaniwaye fisadi lazima awe fisadi na kuna ambao hawadhaniwi kabisa kwa kushinda kwenye nyumba za ibada na michango mbalimbali kusaidia huduma za jamii, kumbe ni mafisadi wanaofidi kuliko hata mafisadi wa EPA. Umdhaniye ndiye....
There is no way kukawa na wizi hazina ama BOT bila ya uhusika wa mgonja...hata wa kunyamaza kimya.....
Tanzanianjema
Kwa mujibu wa sheria zetu, kila mtu anadhaniwa kuwa ni mtu safi mpaka mahakama ithibitishe vinginevyo.Mwenye uwezo wa kuthibitisha kosa ni mahakama pekee.
Hata watuhumiwa wote wa EPA kwa mujibu wa sheria ni watu safi mpaka watakapo thibitishwa.

Tusihamanike sana na hizi kesi za ufisadi kwa ajili ya hasira na machungu ya umasikini wa nchi yetu. Kuna mafisadi tena mafisadi kweli, watashinda kesi na serikali italipa fidia ya mabilioni mengine. Na kuna kondoo wa kafara miongoni mwa mafisadi, watahukumiwa na watakwenda jela kwa kulinda maslahi ya mafisadi wanene zaidi ambao wanaendelea kutesha kwenye mavogue yao, vioo vyeusi na kiyoyozi kwa kwenda mbele. Only time will tell.
- Mkuu jaribu kua current na how siasa na sheria kwa viongozi works in bongo, ukiwa kiongozi kwanza unashutumiwa kwa ufisadi, then rais anakutema kwenye uongozi au unajiuzulu, halafu unaenda Kisutu so far tuko kwenye the right track na Mgonja,

Mkuu Pasco, Rais wetu hakutemi bila kupewa legal facts against you maana alionywa siku nyingi na wabunge kua awateme wote wachafu, kesi za Mgonja ni kama za Mramba, ni nyingi sana kuliko zilizosemwa tayari kwa hiyo mkuu hii safari ni ndefu sana yaani mpaka 2010 serikali haina haraka.
Mkuu FMES kwanza heshima mbele.
Pili, nimekubali yaishe na tusubiri matokeo.
Yote mliyoyasema nimeyakubali naomba mjadala kuhusu comments zangu ufungwe na tuendelee na hoja husika. Please no more quoting me
Natanguliza shukrani. Tuendeleze jamvi.
Pasco,
..ni kitu gani ambacho kinakufanya uamini kwamba Mgonja ni muadilifu. unaweza kutupa mifano michache?
..mwisho, kwa jicho la mwanasheria, kwanini unaona kesi dhidi ya Mgonja haina merits. kwanini unafikiri serikali imekurupuka ktk kupeleka mashtaka haya? vilevile sheria zetu zinaelekeza adhabu gani kwa watuhumiwa wa mashtaka kama ya Mramba,Yona,na Mgonja.
NB:
..kuna waliopendekeza Mramba,Yona,na Mgonja, washitakiwe kwa uhujumu uchumi. kwa mtizamo wa mwanasheria, kwanini unafikiri serikali haikupeleka kesi ya namna hiyo?

Hivi wewe unadhani mtu mbaya anyezungunziwa hapa ni yuelea anyetukana hadharani,mgomvi,anapiga wezake,anaongea vibaya na watu.............!?

Wake up acha kututea ujinga kama unajua mambo ya sheria na mashtaka kuna kitu kina itwa "wizi wa kuaminika" hii inausisha smart people na wenye sifaa nyingi nzuri tu .Unayemtetea ww anawezekana anasifa nzuri tu za mahusiano na watu kama ww na wengine,pia ni mchapa kazi hodari ,msomi makini na n.k,lakini aliyofanya kafanya akijua nafanya nini so stop talking ya nonesense.
Umeongea vitu vya ajabu hapa yani umeokolewa na uhuru wa kuongea tu,you saved by the bell.
Haya ni mabishano yaliyofuatia kuhusu coment yangu on Gray Mgonja, mlinibeza sana, lakini hatimaye kilichotokea wote mmekishuhudia!, the end justify the means, siku zote ukweli tuu ndio utakaosimama mpaka mwisho!, na kwenye kanuni ya kulia na kucheka, he who laugh last. laugh most!.
Kuna waliolia na waliocheka.

Funzo ni moja tuu, wakati tukibezana humu, tuwe pia tunaweka na akiba ya maneno!.
Nawatakia Saba Saba njema!.

Pasco
 







haya ni mabishano yaliyofuatia kuhusu coment yangu on gray mgonja, mlinibeza sana, lakini hatimaye kilichotokea wote mmekishuhudia!, the end justify the means, siku zote ukweli tuu ndio utakaosimama mpaka mwisho!, na kwenye kanuni ya kulia na kucheka, he who laugh last. Laugh most!.
Kuna waliolia na waliocheka.

Funzo ni moja tuu, wakati tukibezana humu, tuwe pia tunaweka na akiba ya maneno!.
Nawatakia saba saba njema!.

Pasco

justice is never perfect..it is just what seems reasonable!
 
hata mramba na yona watachomoa tu so far as mzee wa bifu muda wake umekwisha, TRA walitoa ushauri,hakuna sheria inayolazimisha wakubaliane na ushauri wa TRA
 
Back
Top Bottom