Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,354
- 1,943
Kuwakosesha wapiga kura wake uwakilishi katika kipindi hiki ambacho bunge la bajeti ndio kikao muhimu sana kilichobaki, tena mwaka wa fedha wa mwisho katika tenure yake, ni usaliti. Ni kujijali maslahi binafsi kuliko ya waliomchagua. Hajaikimbia CCM huyu, kawatosa wapiga kura wake. Angekuwa mwema huyu, angewawakilisha vema wananchi amalize mkataba wake waliompa, kisha aondoke.
Ni sawa na baba kusikia vishindo nje usiku, kisha anaikimbia nyumba na kuacha mlango wazi ilhali wanaomtegemea wako ndani! Usaliti wa dhahiri.
Hao mafisadi anaowakimbia ndio aliowaachia jimbo lake la Kishapu wajivinjari watakavyo! What a shame! And you call this patriotism! Amechemsha bana!
Maslahi gani binafsi kwa kuhamia upinzani? Kuna usaliti mkubwa kuliko ule wa kusaliti nafsi yako? Kuna mijitu kibao ambayo dhamira zao zinawasuta kwa kuwa CCM lakini imeshindwa kutoka kwa sababu mbalimbali binafsi na za kimwili, hawa ndio wasaliti!!