Wana Simba SC Wenzangu mtanisamehe, ila Goli la Chirwa lililokataliwa 100% ni sahihi na tumlaumu Kocha Pablo kwa Ubovu wake

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Hivi Kocha mwenye Akili Timamu unawezaje kuwaanzisha Wachezaji Waandamizi na waliotumia Nguvu Kubwa katika Derby badala ya Kuwatumia wale wasiokuwa na Nafasi na ambao hata Kiufundi tu Mechi hi ndiyo ingewafaa?

Hivi leo Pablo Franco Martin angeanza na Kikosi hiki nani angemlaumu hata kama Kingefungwa ukizingatia kuwa hakuna cha Kupoteza kwakuwa tayari Yanga SC kwa 99% ni Bingwa wa NBC Premier League?

1. Beno Kakolanya
2. Israel Patrick
3. Gadiel Michael
4. Kennedy Juma
5. Pascal Wawa
6. Thadeo Lwanga
7. Yusuph Mhilu
8. Muzamiru Yasin
9. Meddie Kagere
10. John Bocco
11. Jimmyson Mwinuke

Pablo si Kocha afukuzwe upesi Simba.

Kuhusu lile Goli la Tatu lililofungwa na Mshambuliaji Obrey Chirwa na Kukataliwa lilikuwa ni halali ( sahihi ) tena kwa 100% na kwamba Namungo FC wamenyimwa Makusudi Goli / Bao lao zuri tu.

99% ya Wachezaji wa Simba SC leo walikuwa Wamechoka ( Wameshanoki ) na hawakuwa katika Kiwango chao Kilichozoeleka na hata tu Body Languages zao zilisema mengi juu yao.

Cc: NAJYUZ, Laki Si Pesa
 
Wamepandishwa mwewe kwenda Lindi kuambulia point moja. Hebu hawa wachezaji wamuonee huruma muwekezaji. Wakati umefika waanze kukatwa mshahara, wao na kocha wao.
 
Ukiona hadi Watu wanaweka Matangazo yao ya Biashara kupitia Threads zako jua ID yako ina Mvuto wa Kipekee na Ushawishi usio wa Kawaida.

Ahsante sana na mno Mwenyezi Mungu.
Bado matangazo ya waganga wakugangue huo unafiki wako
 
Bado matangazo ya waganga wakugangue huo unafiki wako
Vipi hujaumia Roho Jamaa Kutangaza Biashara yake kupitia Thread yangu na ambayo hata Wewe pia pamoja na Kunichukia Kwako umeisoma na bado tu unaendelea Kuisoma na hata Kuichangia kama hivi?

Na kwa hili unadhani kati yangu na Wewe nani atakuwa si tu ni Mnafiki bali ni Mpumbavu na Mwendawazimu kabisa?
 
Nenda kaombe kazi au show us what you have done/mafanikio yako kwenye hii tasnia ya football
 
Back
Top Bottom