Salam wandugu,
Nilikuwa zanzibar kwa mapumziko mafupi, nimepata gari ambayo imesajiliwa hapa ZNZ sasa nataka mwenye ufahamu juu ya suala hili, je nikivuka nayo huko bara nitaweza kuitumia au ndio hadi nilipe tena ushuru na kubadisha namba
gharama zake zikoje mkuu, ila kama uonevu flani, si ni nchi moja sisi soteUnaweza kulitumia bila wasi wasi wote na ukakata nalo mitaa yote bila bughuza zozote ili mradi tu ufate sheria.
Kwanza lisajili hilo gari huko Zanzibar ili lipate namba mpya zinazoanzia na Z xxx YY. kisha litapata police clearance na kulileta Bara na kulilipia kama gari inayotoka Kenya, Uganda au nchi yoyote ile ya kigeni.