Je, naweza kutumia gari yenye usajili wa Zanzibar, Tanzania Bara?

hp4510

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
6,451
6,325
Wandugu,

Nina gari Zanzibar, nataka kuja nalo bara, na niweze kulitumia kwa miezi michache.

Swali langu: je, ni process gani zinatakiwa kufuatwa?

Kama kuna mtu yeyote amewahi kupata changamoto kama hii naomba aniambie alitatuaje.
 
Tanzania ina maana Tanganyika na Zanzibar, kwahiyo nenda nalo tu hakuna usumbufu alimradi uwe na nyaraka muhimu za usajili na hasa kadi ya gari.
 
Sahau kulitumia hilo gari kwa usajiri wa Zanzibar huku bara lazima ukifika utaambiwa kubadili ila chaajabu mtanzania akienda na gari kutoka bara anatumia tu vizuri kule Zanzibar bila shida ndio.
 
Sahau kulitumia hilo gari kwa usajiri wa Zanzibar huku bara lazima ukifika utaambiwa kubadili ila chaajabu mtanzania akienda na gari kutoka bara anatumia tu vizuri kule Zanzibar bila shida ndio

Hizi gari ambazo ziko hapa Dar zenye namba za Zanzibar inakuwaje?
 
Pamoja na kuwa hizi ni nchi ni Muungano lakini kuna vitu vinafanya ziwe kama nchi mbili tofauti kabisa.
 
Inawezekana lakini utaratibu wake umekua mgumu kidogo siku za hivi karibuni.

Naomba nitoe maelezo kidogo, Zanzibar ni tofauti na Bara, ukiwa Zanzibar unaweza kulipia ushuru 30%, 40% au 50% na ukachukua gari yako bandarini ukaendelea na maisha, hivyo magari mengi yanadaiwa ushuru.

Bara ni nadra sana kama sio haiwezekani kuitoa gari bandarini bila kukamilisha malipo ya ushuru.

Hapo ndio changamoto inapoanzia, awali ilikua unaandika barua kuomba kutumia gari yako bara kwa miezi mitatu na ilikua unapewa kibali, ikaonekana wajanja wanatumia huo mwanya kupeleka magari bara wanafanya manuva, gari haiurudi, inapigwa juu kwa juu huko huko na kubadilishwa usajili.

Sasa hivi utaambiwa uache dhamana sawa na kiasi cha kodi inayodaiwa gari husika. Sasa kwa huo usumbufu si bora umalizie kodi iliyobaki ili hata ukivuka nalo hakuna mlolongo mrefu?

Ikiwa gari yako imelipiwa ushuru asilimia zote, haidaiwi, unaandika tu barua TRA/ ZRB kisha utamalizana na Agent na usafirishaji ambazo gharama zitategemea na ukubwa wa gari.

Nafikiri umepata mwanga kidogo mkuu.
 
Sahau kulitumia hilo gari kwa usajiri wa Zanzibar huku bara lazima ukifika utaambiwa kubadili ila chaajabu mtanzania akienda na gari kutoka bara anatumia tu vizuri kule Zanzibar bila shida ndio

Gari zote bara zinalipiwa ushuru wote, hauwezi kusumbuliwa ukivuka nalo visiwani. Magari ya Zanzibar sio lazima ushuru wote ulipwe ili uondoke na gari.
Kwa muktadha huo, ili ivuke kuja bara, lazima deni lilipwe.
 
Inawezekana lakini utaratibu wake umekua mgumu kifogo siku za hivi karibuni.

Naomba nitoe maelezo kidogo, Zanzibar ni tofauti na Bara, ukiwa Zanzibar unaweza kulipia ushuru 30%, 40% au 50% na ukachukua gari yako bandarini ukaendelea na maisha, hivyo magari mengi yanadaiwa ushuru.

Bara ni nadra kama sio haiwezekani kuitoa gari bandarini bila kukamilisha malipo ya ushuru.

Hapo ndio changamoto inapoanzia, awali ilikua unaandika barua kuomba kutumia gari yako bara kwa miezi mitatu na ilikua unapewa kibali, ikaonekana wajanja wanatumia huo mwanya kupeleka magari bara wanafanya manuva, gari haiurudi, inapigwa juu kwa juu huko huko na kubadilishwa usajili.

Sasa hivi utaambiwa uache dhamana sawa na kiasi cha kodi inayodaiwa gari husika. Sasa kwa huo usumbufu si bora umalizie kodi iliyobaki ili hata ukivuka nalo hakuna mlolongo mrefu?

Ikiwa gari yako imelipiwa ushuru asilimia zote, haidaiwi, unaandika tu barua TRA/ ZRB kisha utamalizana na Agent na usafirishaji ambazo gharama zitategemea na ukubwa wa gari.

Nafikiri umepata mwanga kidogo mkuu.

Nimepiga simu tra bara kuulizia, na wao wameniambia, niende ZRB watanipa kibali then nakuja na gari Dar kwa miez mitatu
 
Back
Top Bottom