Malipo ya magari yenye plate number za Zanzibar kutumika Tz bara

TanGas

New Member
Nov 9, 2018
4
1
Wadau kwa anaejua malipo ya magari yenye usajili wa Zanzibar yanayo tumika huku Tanzania bara.

Ningependa kujua kama malipo yanafanywa kwa kipindi maalum ambacho unaomba kutumia ama kwa mwaka mzima?

Malipo yanategemea cc za gari ama kuna category maalum za kuzingatia?
 
Daaah wakuu wameugomea uzi
 
Nina rafiki angu TRA anasema ukishakuwa na gari uliyotoa Zanzibar ukalera Bara iyo ni sawa na gari mpya so unaanza mchakato kama vile umeitoa bandarini
Hebu panua hii elm. Ina maana Zanzibar ni sawa na Dubai au ni sawa na mkoa kama vile Lindi?
 
Ninavyojua ukisajili gari Mwanza unaweza kwenda nalo hadi Lindi. Kumbe visiwani kuna maneno. Je kama limesajiliwa visiwa vya mafia au ukerewe. Ukiliingiza Tanzania bara kuna maneno ya kulipana?
 
Ninavyojua ukisajili gari Mwanza unaweza kwenda nalo hadi Lindi. Kumbe visiwani kuna maneno. Je kama limesajiliwa visiwa vya mafia au ukerewe. Ukiliingiza Tanzania bara kuna maneno ya kulipana?
Tunazungumzia visiwa vya unguja na pemba wewe. Hivyo visiwa ulivyotaja vipo ndani ya Tanganyika.
 
Ninavyojua ukisajili gari Mwanza unaweza kwenda nalo hadi Lindi. Kumbe visiwani kuna maneno. Je kama limesajiliwa visiwa vya mafia au ukerewe. Ukiliingiza Tanzania bara kuna maneno ya kulipana?
Hapo ndipo pale wazanzibari wanaposema huu sio Muungabo ni Ukoloni lakini nyinyi watanganyika Hantaki kuelewa. Hata huko Zanziba TRA wako na wanakusanya mapato, inakuaje kua Gari iliyotolewa Zanzibar ilipiwe Kodi?
Ndio nakumbuka lile Sakata la Zeco , walikua wakinunua Umeme Tanganyika wanalipia kodi TRA na wao wakiwauzia wateja wanakuja tena TRA wanachukua Kodi. Sasa ZECO wakagoma kulipa, yakaja Mazungumzo, lakini ndugu zetu wa damu baada ya kukubali kosa kua kweli walikuwa wanawadhulumu Wazanzibari, wakajitangazia wamewasamehe deni. Lakini Miaka yote hio ya nyuma zaidi ya 30 waliyowadhulumu hio haitajwi
 
Nisameheni kwa kuuliza uliza. Kwani TRA ya Zanzibar na ya huku bara wanatumia sheria torfaut? Kwamba gari likipiwe kiduchu Zanzibar kwasababu serikali yao haihotaji pesa na huku gari hilo hilo lilipiwe zaidi kwasababu tunajenga hospitali. Kwani wazanzibari hawahitaji huduma za jamii.
 
Ukiingiza gari kutoka znz utaratibu wake ni Kama umeingiza kutoka nchi jirani.utapewa document inaitwa TIP ambayo utakuruhusu kutumia gari yako ndani ya miezi (3) then utatakiwa kulipa ushuru au kila baada ya miezi (3) uwe unaigia znz na kutoka ili upate TIP ya miezi (3) mingine.
 
TIP hiyo inaolewa kwa kiasi gani? Rejea swali la mchokoza mada.
Ukiingiza gari kutoka znz utaratibu wake ni Kama umeingiza kutoka nchi jirani.utapewa document inaitwa TIP ambayo utakuruhusu kutumia gari yako ndani ya miezi (3) then utatakiwa kulipa ushuru au kila baada ya miezi (3) uwe unaigia znz na kutoka ili upate TIP ya miezi (3) mingine.
 
Hebu panua hii elm. Ina maana Zanzibar ni sawa na Dubai au ni sawa na mkoa kama vile Lindi?

Iko hivi Zanzibar ina mamlaka yao ya mapato na inaserikali yao wanamifumo yao hivyo unavyokuja na gari yako bara pia tambua kuna mamlaka zake husika na serikali yake inayohusika na maswala ya kodi hivyo hawafanyi kazi kwa kuingiliana ndo maana unapokuja na gari yako bara unaanza usajili upya as kama umeitoa Japan au Dubai
 
TIP hiyo inaolewa kwa kiasi gani? Rejea swali la mchokoza mada.
Kila mwezi unatakiwa kulipia gharama hizo,ikioverstay yaani baada ya miezi mitatu na siku moja au mbili unapigwa faini ya asilimia 20% ya thamani ya gari,ilishawahi nitokea hii na majamaa flani( wasouth) ilikuwa mbinde sana na nao maafisa forodha
 
Back
Top Bottom