I said no spin zone. Mwanakijiji aliniuliza kuhusu Africa. Na nikasema maoni yangu kuwa tuache longolongo.
Na kuhusu IMF, IMF imesaidia. Bila IMF tungekuwa tunavaa viroba.
Kwa hiyo hii ndiyo solution uliyokuja nayo toka kwenye drawing board. IMF?
I said no spin zone. Mwanakijiji aliniuliza kuhusu Africa. Na nikasema maoni yangu kuwa tuache longolongo.
Na kuhusu IMF, IMF imesaidia. Bila IMF tungekuwa tunavaa viroba.
Afrika lazima ibadilike; kutoka bara ambalo linasubiri matukio nje yake yenye kusababisha mabadiliko kuelekea bara ambalo watu wake wanasimamia mabadiliko yao wao wenyewe.
Ni nini kuarticulate ukweli kuwa lazima tuwe "a continent which challenges the environment and adapts it to man's need." Hakuna aliyeonesha ubaya wa fikra hii.
Kuhusu suala la Afrika kubadilika unakubali fikra hizo au zinamakosa mahali?
.... sasa wasomi wa maandishi ya Mwalimu, si watataka kuja bongo kujionea the works za mkali wa intellectulism za change katika Afrika, exactly kuna nini cha kuonyesha? Leo Tanzania kuna nini cha kuonyesha ili kuthibitisha umahiri wa Mwalimu, on change katika baara la Afrika?
.....
Tunapozungumzia kuzingatia misingi ya utawala wa sheria, kuwa na maadili n.k tunachosema ni kuwa vitu hivyo havipo sasa na tunataka tubadilike. Hivyo tunakubaliana na Mwalimu kuwa we need to change our "attitudes and practices to accord with the objectives." Kuna ubaya gani katika ukweli huu mwingine kuwa kama kweli tunataka kufikia malengo yetu hatuna budi kubadilika? Hakuna aliyeonesha hadi hivi sasa.
1. Kabla ya kushauri kubadilika kisheria, Mwalimu alipaswa kusema wazi kwa nini baada ya miaka 23 ya uhuru under utawala wake hatuheshimu sheria, maana wewe mwenyewe unasema kuwa vitu kama sheria havipo sasa swali linapaswa kuwa why? yaani chanzo chake ni nini wakati mtoa mawazo yako ya change alikuwa rais mwenye uwezo wote wa kuweka mawazo yake hayo ambayo sasa unayaita kuwa ni superior na tunahitaji kuyarudia?
Halafu ulipaswa kueleza madhara ya kutokuwa na hivyo vitu kama sheria kwa karibu muda wote huo, mpaka hiyo change itakapokuja, ni nini madahara yake? Na how far yame-reach kwenye jamii na how long hiyo change itachukua kuweza kufagia the effect baada ya kuishi bila sheria, mpaka siku ya change ya mawazo ya Mwalimu itakapofika?
Labda alipaswa kusema kuwa yeye kwanza alipaswa kubadilika ili awe mfano kwetu, maana maneno tu alishindwa kuyatfsiri kwa vitendo.
mungu akubaliki msee FMES, maana huyu bwana MKJJ mie hata sielewi motive(s) yake ni nini!!?? inatisha namna hii, yaani mjuvi kama huyu aweza kuwa bwiga namna hii, sasa hao wakina bwana kabwela huko main street wapoje sijui!? nyerere alikuwa na miaka 23 ya kutengeneza legacy yake......... he failed and failed miserably, yaani hata 'F' hakupata!! full stop.
KIONGOZI ANAPIMWA KWA HIBA; NYERERE HAJAACHA HIBA
Azimio la Arusha: Limechanwa! Tuna Azimio la Zanzibar.
Mfumo wa Chama Kimoja: Falsafa za kuhodhi siasa zilitupiliwa mbali 1992
Siasa za Ujamaa: Zilitoswa kabla hata hajaacha madaraka
Sera za Kujitegemea: aaaaaah Tanzania haijawahi kujitegemea. Hakuwa mkweli hapa!
Elimu ya Bure: Siku hizi unalipia elimu
Uzembe na Uzururaji: Hakuna sheria za Kangaruu kama hizo siku hizi
Maadili ya Viongozi: Yeye mwenyewe alisema wananuka rushwa
Azimio la Iringa: Hakuna anaeongelea 'Siasa ni Kilimo' siku hizi. Tafadhali bwana!
Vijiji Vya Ujamaa: Kuna cha kusema hapa?
Heshima ya Nchi kwa Misimamo Mikali: Siasa yetu inaandikwa na wahisani
Umiliki wa Njia Kuu za Uchumi: Tumeuza kila kampuni
Suti za Kichina: Zaidi ya Malecela na Kingunge hakuna anae taka upuuzi wa Kichina!
Muungano: hapa kaacha hiba
Umoja wa Kitaifa: na hapa kaacha hiba
Ina maana unamaanisha haya unayosema kuwa hakuna chochote cha kuonyesha aliyofanya Nyerere?
1. Hakuna watu waliosoma bure wakati wa Nyerere?
2. Hakuna hospitali zilizojengwa na serikali?
3. Hakuna majengo ya serikali yaliyojengwa?
4. Hakuna barabara hata moja iliyojengwa?
5. Hakuna eneo hata moja lilipatiwa umeme?
6. Hakuna watu wazima waliosomeshwa na wakajua kusoma?
7. Una maanisha hakuna chochote kabisa kilichofanyika?
Jamani wakati mwingine tujaribu kuwa fair. Ni kweli kuwa sera za mwalimu zilishindwa kufanya kazi kwa kiwango fulani lakini si kweli kuwa hakuna chochote ambacho hakufanya kabisa......
Hao watu wanaokuja Afrika leo, je hawaoni kuwa Nyerere aliacha kuchimba madini kwa vizazi vijavyo tofauti na Mobutu ambaye yeye na familia yake walifaidika na madini karibu yote ya Zaire na kuwaachia wanazaire ya leo makorongo na mabonde matupu?
Serikali zinajenga juu ya serikali, Nyerere aliwaomba kina Mwinyi na Mkapa kuacha mabaya aliyofanya na kuchukua mazuri. Je nini kimefanyika kuanzia mwalimu astaafu? Katika hili je bado wa kulaumiwa ni mwalimu?
Labda niulize swali la haraka haraka kidogo wakati mjadala huu ukiendelea. Je ikiamuliwa kuwa Nyerere alishindwa kabisa na wale wote wanaomtetea ni mabwiga. Na pia je ikiamuliwa kuwa Nyerere afutwe kabisa kwenye historia cha Tanzania maana yeye ndiye chanzo cha matatizo yote ya watanzania na waafrika wengine kama wamalawi, wazaire, wazambia, wasumbiji ambao wana matatizo kama ya Tanzania leo. Je Tanzania itafaidika nini? Je kutakuwa na mabadiliko yoyote ukichukulia kuwa viongozi wa ccm kina Kikwete na wenzao hawafuati sera au chochote alichosema na kufanya Nyerere kwa sasa?
Mkuu wangu MWK,
Heshima mbele, mimi sio intellectual, ninakubali kuwa kuna mazuri aliyoyafanya Mwalimu, ambayo mpaka leo yanaweza kuhesabiwa, lakini tatizo ni kwa yale ambayo hakuyafanya kwa sababu ya mapungufu ya kibin-adam, huku akiendelea kuimba nyimbo za change ambazo hata yeye mwenyewe hakuweza kuzifanya kwenye miaka 23 ya utawala wake, sasa tutegemee nini kwa wananfunzi wake wanaotawala miaka 10 tu per term?
Kuna ambayo hujayataja ambayo ni ya muhimu zaidi kama something to show kuhusu uzuri wa Mwalimu, lakini otherwise uliyoyataja hata Mwinyi, Mkapa, na Muungwana sasa wameyafanya, maana mengi ya hayo uliyoyasema yanategemea sana bureaucratic sysytem ya serikali, kuliko uamuzi wa rais.
Mobuttu, kama Mwalimu, walitegemea kutawala kwa kutumia upepo wa the Cold War, Mwalimu hakuwa mroho wa mali, Mobuttu alikuwa, lakini Zaire mkuu wangu kama hujafika, kuna barabara, hospitali, shule na the rest, lakini sio kwa idadi kama yetu bongo. Mwalimu aliacha kuchimba madini? mbona kulikuwa na kiwanda cha almasi Mwadui, na kiwanda cha kusafishia almasi Iringa? au?
Hakusema wazi mabaya aliyoyafanya, na nimemuomba sana Mwanakijiji aweke hizo hotuba ambazo Mwalimu alisema wazi mabaya yake huko magereza, sijawahi kuzisikia ningependa kuzisikia, ili tuweze kuwakaba Mkapa, Mwinyi na Muungwana, kwa nini hawakusikiliza, maana huenda wao wanaendeleza mabaya walioachiwa na yeye bingwa Mwalimu, bila ya kujua kuwa ni mabaya,
However, you are right kuwa matatizo yetu tuliyonayo sasa ni yetu wenyewe, ila tu hata Mwalimu, hakuwa na majibu ya matatizo yetu, na mengi yeye ni chanzo, sasa kama ni change yeye kwanza ndiye aliyepaswa kubadilika kwanza, ili tufuate mfano wake.
Otherwise, una strong argument mkuu!
Na mengineyo mengi ambayo ni kinyume na sera za Nyerere. Sasa haya mawazo ya kuwa inabidi sumu ya Nyerere itoke ndio tuendelee yana msingi upi?
........kutofautiana kimawazo sijambo baya....ili mradi iwe katika kujenga na si kubomoa.........watu tunatofautiana pia ktk perceptions kulingana na wakati.....
Idea za Mwl JKN alizoweka Mwanakiji ndio kinachojadiliwa hapa and nothing less......kama uliona nimekuwa off (kwa mtizamo wako)....fine.......however hainizuii kuonyesha niliyoyaandika
ya kwamba pamoja na kuwa ideas za JKN hazikufanikiwa.....haimaanishi kuwa zilikuwa mbaya......na baadhi ya watu wamejaribu kulinganisha na yanayotokea sasa na idea alizokuwa nazo JKN (they were out of ishu as well)......na ndio maana nikaweka ulichokisoma........
....other stories are out of context.......
tuendelee kujadili ideas za JKN