Fikra za Mwalimu: Hizi hapa.. mzikubali au mzipinge!

Wakuu hapa nashindwa kuchangia kwani sielewi kinachoendelea kabisa...
Fikra za mwalimu na kufanikiwa kwake kunahusiana vipi lakini?... mbona hata Yesu hakufanikiwa akiwa hai leo tuna wakristu mabillioni...ambao kwa matendo yao naweza sema ni asilimia chini ya 20 wanaofuata Ukristu alofundisha Yesu. Je, tuseme kuwa mafundisho ya Yesu hayana maana ni upuuzi mtupu kutokana na results zetu sisi tunaokataa kuabudu kwa vitendo!..
Jamani hata Nyerere ktk mifano yake midogo aliweza toa mfano wa kuhesabu wakristu wanaoingia kanisani ili ku judge mafanikio ya dini ya Kikristu. Na hata kama hesabu ya wakristu ama waislaam jina iwe kwa mabillioni lakini kama sote hatufuati hizo dini kwa matendo yetu haiwezekani kuwa hao viongozi wetu walikuwa na fikra mbovu, zisizofaa kuwa biblia ama Kuran.
Yawezekana sisi wenyewe ndio tumepotea na ktk fikra zetu mbovu ndio maana tunaona maandishi ya Biblia na Kuran ni mawazo ya kizamani hasa kama tunataka kuupigia debe ufuska na ujunya..
Mwalimu aliupiga vita Ubepari kwa sababu za msingi. Kwanza nchi yetu kwa asilimia zaidi ya 99.9 tulikuwa maskini, sasa huyo bepari angetokea wapi ikiwa nchi nzima haina mwekeshaji wa ndani ambaye angeweza endesha hata tawi moja la Benki...I mean ebu nambieni nyie huo Ubepari ungeanza vipi kama sio kwa njia hizi hizi tunazoziona leo hii viongozi wakivamia mali za Umma kama vile ni mirathi yao halali ili wapate kuwa Mabepari wa kesho. Is this real Capitalism, viongozi kuiba mali zenu wakitumia wadhifa wao! ebu nipeni darasa wakuu inawezekana mimi ndio nipo kizani... maanake nasikia siku hizi Ujanja ni KUPATA sio KUWAHI tena.

Mnazungumzia maswala ya Benki ktk Ujamaa kama vile vitu hivi vimekuja toka mbinguni. Hiyo CRDB, NMB zingeweza vipi kuwepo kama sio nguvu ya serikali mwanzoni kuzipa Boost hadi zilipoweza kusimama... leo mnakuja jaribu kufananisha uendeshaji wa Benki hizo na leo wakati mnafahamu kabisa kuwa bila kuanza kutambaa na malezi ya mama (serikali) kwa benki hizo leo hii zisingeweza simama wima, sasa baada ya kujua kutembea na suruali zetu za Kata Kundu tunalinga na kumsahau mama na malezi yake..Na ajabu kinachozungumziwa hapa ni kazi ya kutambaa na kutembea ipi bora!..

Jamani jamani Fikra ni pamoja vision za mwalimu ambazo kama alivyosema MLK kwamba anaweza kutokuwa nasi kufikia hiyo promise land lakini tutafika!..Hakuhitaji yeye kuwafikisha Waamerika weusi ktk hiyo promise land lakini fikra zake ndizo zinatumika hata kama iwe kwa mbinu tofauti lakini malengo yao yanajulikana. Na ukitazama jinsi MLK alivyokuwa akipigania Uhuru wa mtu mweusi Marekani miaka hiyo huwezi kabisa kuitumia leo (maandamano na migomo) kwani sasa hivi hao Waamerika weusi wapo hatua nyingine kabisa ya ubaguzi hivyo mapambano yake pia yamebadilika..
Leo hii baada ya kifo cha siasa za West na East, tupo ktk hatua tofauti kabisa kama vile South walivyokuwa wakimwona Kaburu kabla ya Uhuru wao. Hatuwezi sema fikra za Steve Biko na kina Oliver Tambo hazina mpango kwa sababu tu walisema - Utawala wa Kaburu utasokomezwa baharini!..Fikra za mwalimu tuzienzi kwa kukumbuka safari alotuambia tuifanye kufikia maendeleo yetu sote bikla kumwacha mtu nyuma. Sasa iwe Ujamaa, Ubepari na lugha yoyote ile mnayotaka kuitumia lakini muhimu ni kuelewa kuwa tulikuwa na malengo. Malengo hayo yatafikiwa ikiwa tu tutazingatia mambo muhimu hata kama mbinu zetu za kufika huko zitabadilika. The vision remains!
Wakuu nipeni point nzito nipate kuelewa kinachoendela maanake naona vidole tuuu zuri silioni upande wa pili iwe fikra wala matendo.
 
Mkuu wangu MWK,

Ninasema hivi tena kutoka kwenye damu na mifupa yangu ya mwili, kwamba kiongozi wa kutusaidia wa-Tanzania, ni yule tu atakaye yaacha yote tuliyoyapitia huko nyuma, na kuanza upya na fresh ideas, na hasa atakayesema wazi tena hadaharani kuwa mawazo ya Mwalimu mengi yalishindwa, hatutayarudia tena, na akaweza kukubaliwa na wananchi, ujue huyo ndio mkombozi hasa wa taifa letu,

Je hiki sio ambacho Mtikila amekuwa anasema miaka yote hii hata kufikia hatua ya kumwita Nyerere shetani?

Wa-Tanzania ni lazima tuwe macho sana na viongozi kama Mwalimu na Mwanakijiji, ambao ni wengi sana Tanzania, toka tupate uhuru, wameshikilia intelectualism na elimu ambayo mwisho wake ni mikogo tu kwa wasomi wengine na viongozi wasiosoma, lakini in-applicable kwa maisha ya wananchi wa kawaida ambao ndio hasa taifa letu, hawa watafikia ku-change hata the un-changeable, watasema maneno magumu ya darasani kujaribu kuweka sera kwa taifa, ambazo kila mtekelezaji atashindwa, kama Mwalimu alivyokuwa, maana it always give them an-edege ya kusema kuwa mmekosea kwa sababu mmefanya vingine na nilivyosema, mimi nilisema kii-intellectualism, nyinyi mmefanya kirahisi sana haiwezi kuwa hivyo mlivyofanya, yes mara ngapi Mwalimu alikuwa akimtupia lawama Kawawa, kuwa hakumuelewa kwenye utekelezaji wa mawazo yake ya change, kwa mfano change ya maduka ya ushirika,

Ni watanzania wangapi unaweza kusema kuwa walizaliwa wakati wa Nyerere? jibu rahisi ni kuwa ni chini ya asilimia 50? sensa ya Tanzania imeongezeka zaidi ya mara mbili kuanzia mwaka 1985.

Haya ya Nyerere yanaathiri wangapi?

Wakuu mengi yamesemwa kuhusu Marehemu Sokoine, ukweli ni kwamba all the man did ilikuwa kujaribu kutafuta change ya kufuata utawala wa kuheshimu sheria, off course kuna hitilafu nyingi sana zinazojadilika on njia alizojaribu kuzitumia kutekeleza, lakini nia ilikuwa njema sana na somehow aliweza kupata our nation's attention of what he was trying to do in only six months, lakini miaka 23 ya Mwalimu, we had no idea alikuwa anasema au anajaribu kufanya nini?

Mwalimu was the greatest ever, lakini muda wake uliisha, sasa tusonge mbele na mapya.

Na hawa viongozi waliokutana huko Butiama, na kuamua kuwa turudi kwenye mawazo ya Mwalimu, tuwaangalie vizuri sana hawa, ninasema hivyo kwa sababu ninajua kuwa sio wote walioshirki kwenye hayo maamuzi, au waliokubaliana nayo.
Ahsante wakuu!

Inaonekana unakubaliana na wale wanaosema kuwa ccm watolewe toka madarakani kama kweli haya ndiyo wanaletea watanzania ambao wengi hawamjui hata huyu Nyerere.
 
Kuhani,i thought you would get it, but still dont ! he admitted he failed on some, but also exelled on some as well. sasa wewe fanya choice, mfanye mazuri au yale ya kijinga ! hakukataa, na yeye mwenyewe alisema sio malaika, HIVYO MSIMTUKUZE !!
 
Ni viongozi wachache sana duniani wenye bahati ya kupata nafasi na kujenga nchi kwe kutumia sera wanazotaka.

Dunia ina mabadiliko mengi na kiongozi akiwa madarakani inabidia aachane na sera zake na kufuata reality ya dunia. Na viongozi wengi wanaofanikiwa ni wale wenye kufuata reality ya dunia kuliko sera.

Wanaong'ang'ania sera siku zote wanaawacha watu wao masikini (Nyerere, Mugabe, Kaunda you name them). Na hii ipo mpaka kwenye nchi zilizoendelea. Chukua Bush alivyoingia madarakani, ameng'ang'ania sera za Iraq na mambo hayanyooki.

nilidhani kuwa hii ya kushindwa sera ndiyo ilipelekea Nyerere kuachia madaraka badala ya kungangania kama mabepari majirani zake wa wakati huo Mobutu na Kenyata?
 
Kuhani,i thought you would get it, but still dont ! he admitted he failed on some, but also exelled on some as well. sasa wewe fanya choice, mfanye mazuri au yale ya kijinga ! hakukataa, na yeye mwenyewe alisema sio malaika, HIVYO MSIMTUKUZE !!

Kuhani is dumb as a rock....don't expect much from him...
 
Kuhani,i thought you would get it, but still dont ! he admitted he failed on some, but also exelled on some as well. sasa wewe fanya choice, mfanye mazuri au yale ya kijinga ! hakukataa, na yeye mwenyewe alisema sio malaika, HIVYO MSIMTUKUZE !!

Wale wanaosema kuwa Nyerere alipumbaza watanzania wote kuanzia Mtwara hadi Moshi wanamtukuza zaidi kuliko wanavyofikiria hapa. Huyu alikuwa binadamu tu wa kawaida, huu uwezo wote aliutoa wapi?
 
Wale wanaosema kuwa Nyerere alipumbaza watanzania wote kuanzia Mtwara hadi Moshi wanamtukuza zaidi kuliko wanavyofikiria hapa. Huyu alikuwa binadamu tu wa kawaida, huu uwezo wote aliutoa wapi?

ilifanyika hadi misa ya kumpa utakatifu ! maskini wee mwenyewe sidhani kama angekubali !

Lakini over all, he was a great citizen, leader, humbe man with integrity ! he achieved a lot for his people !
 

Unaweza kudhani Nyerere kakiri makosa katika ile hotuba. Lakini nimekuwa nikisema kwamba usiseme tusijadili makosa yake kwa sababu amekiri. Mjadala sio kama amekiri au hakukiri makosa. Hakuna anayedhani Nyerere, au awaye yote mwingine, ni mtakatifu, nimerudia tena na tena. Kwa hiyo huwezi kuweka hatamu katika hoja zinazo kosoa mtu eti kwa vile hakuna aliyekamilika. Ingekuwa hivyo ndivyo, basi mtu akikukanyaga barabarani asingekuomba msamaha kwa sababu hakuna aliye kamilika. Sijui unanielewa?

Hii hotuba ya Nyerere kuna upande mwingine wa kuyaangalia aliyo yasema ukaona kwamba anajitetea zaidi ya kukubali. Halafu hapo hapo badala ya kuonyesha masikitiko na majuto ya mwomba radhi anadiriki kusema tunafuata ya kijinga aliyoyafanya. Anahamishia lawama kwa wengine. Ndio maana nikasema huyu hapa anajitetea. Baada ya hapo nikakataa huu utetezi kama uthibitisho wa kwamba hajafanya makosa kwa sababu maneno ya mtuhumiwa ni buruhahi tu, hayabainishi chochote.

Ile hotuba nimeiona mara mia kidogo. Baada ya kustaafu alitembea dunia nzima akisema -kama alivyosema kwenye hicho kipande - alikuwa hana wataalam ndio maana aliharibu. Lakini, wahakiki wa Nyerere ambao hawatumii hotuba za Nyerere mwenyewe kumtathmini Nyerere, tumekataa hilo kwa sababu ni ashakum za kufunika makosa. Sera zake zilikuwa mawazo yake mwenyewe, sio ya wataalam. Bunge la Nyerere lilikuwa linapiga mihuri mawazo yake. Waliompinga waliishia kuishi na Kambona UK au na maafande Oysterbay Polisi bila mashitaka -na hivyo hatia- kama nilivyosema kwenye tundiko lingine juu. Azimio la Arusha aliliandika mwenyewe, akawaita wana CCM Arusha kulisaini, toka hapo akatembea nchi nzima kulinadi. Baadae fikra zake zote potofu na njema zimetupiliwa mbali na Watanzania.

Ndo maana nikasema Nyerere hajatuachia hiba. Fikra zake zote Watanzania wamezitupa!



 
well, sasa hapa nadhani kuna mambo ya KUDHANIA.... what he said was plain and simple to me, kwamba amekiri awamu yake ilifanya makosa na kama ulisikiliza kwa makini zaidi alisema, awamu inayofuata inatakiwa kusahihisha yale makosa. Sasa swali mzee wa kuhani, unaweza kusahihisha kitu kama hujakosa ? HAPANA, HUWEZI ! So, to me that was simple, ndio alikiri kwamba amekosa, na sidhani kwamba kuna haja ya kujitetea ukiangalia the fact kwamba, dakika chache baadae baada ya kusema hivyo katika speech hiyo hiyo alisema wao sio malaika, SO HAKUNA EXCUSE KWA MAKOSA WALIYOFANYA. Ajitetee kwani watu walimuhoji au ndio unasema alijistukia, hivyo ilibidi ajitetee ?

The truth is clear, lakini kama utataka kufuata kile akili yako inachokwambia ufikirie pia sio vibaya maana you might as well come up with new ideas. ndio uzuri wa kufikiri huo !
Kutokuwa na wataalam inaweza ikawa moja ya sababu ya kufanya mambo ya kijinga katika nchi haswa kwa kipindi kile. Lakini LAZIMA YOU HAVE TO FACE THE FACT KWAMBA, nchi ndio kwanza ilikuwa imetoka mikononi mwa mkoloni, unategemea nini mzee ? Sio kama namtetea nyerere, lakini ukweli lazima usemwe pale unapohitajika. Siwezi nikakaa kimya hata siku moja iwapo nitaona jambo misleading linajitokeza !
Hivi unataka kuniambia alichoaccomplish nyerere, in terms of the state of country as a whole up to now, jumlisha na ethics njema alizokuwa akisimamia, unadhani kiongozi gani tena toka tz anamkamata huyu mzee nyerere ?? hata ukijumlisha wote, still the man (Nyerere) was/is still wayyyyyyy far ahead of the game. He understood the world, and most likely the kind of environment the country was in and he worried about that UNLIKE na viongozi wa sasa !

Kuhusu hoja zake kupigiwa mihuri, i have never heard that, na hata kama ilikuwa so, that might be one of the "ujinga" as he calls it, walioufanya !




"fikra" na "vitendo", keep this in mind !
 
Kwanza, kama hujawahi kusikia kwamba Bunge la Nyerere lilikuwa kazi yake kupiga mihuri mawazo ya Nyerere basi tuko mbali sana kuweza kukutana tukaelewana kuhusu Nyerere.

Halafu, umenisaidia na kuunga mkono hoja yangu bila wewe mwenyewe kujua: Nyerere mle anajitetea! Na wewe ukazidi kumtetea badala kung'ang'ania hoja yako ya awali kwamba mnakubali makosa!

Oooooh, aksante. Umethibitisha ninacho kisema: A-n-a-j-i-t-e-t-e-a!
 
Tutaendelea kwenye mjadala wa fikra za Nyerere. Tumeiona ya kwanza kuhusu change na hitimisho ni kuwa hakuna aliyekataa susbtance ya hotuba hiyo. Wengi ambao wanapinga wanapinga kwa sababu aliyesema ni Nyerere.

Ni sawasawa na mtu kukataa uzuri wa Azimio la Uhuru wa Marekani kwa sababu waandishi wake walikuwa ni slave owners! Ni sawasawa na mtu kupinga uzuri na tunu ya Hotuba ya "Nina Njozi" ya MLK kwa sababu leo tumeambiwa kuwa kumbe jamaa alikuwa anajisasambua pembeni (wengine walikuwa wanajua hilo); Ni sawasawa na watu kuikataa ile hotuba ya Mandela kizimbani ati kwa sababu baadaye aliamua kumuacha mkewe hivyo hotuba ilikuwa mbaya!

On substance alone the piece was ground breaking, historic, and if I may be bold prophetic. Hakuna kitu ndani yake ambacho watu wamepingana nacho substantially. Hivyo tutaenda kwenye "theme" ya pili mapema leo (nikiweza kudonyoa keyboard na kuhamisha from hard copy to soft copy).

Asante kwa michango yenu yote. Anayetaka kuzungumzia legacy ya Nyerere na alifanikiwa wapi n.k naomba anzisha mada ya namna hiyo na nina uhakika watu watachangia.
 
Bwana Yesu alipokuja duniani, alihubiri sana kuhusu Ufalme wa Mbinguni. Alitoa mifano mingi ya mafumbo na hata mambo mepesi. Je ilikuwa ni jukumu lake kuhakikisha wote tunafuatiilia amri za Mungu au tunakuwa Wakristo kamili?

Kuna mtu kasema Nyerere alifukuza mbali waliompinga. Mungu alimfukuza Ibilisi alipompinga na kukataa kutii na kufuata mwongozo.

Kuleta kwangu mifano hii miwili, hakuna mana ya kumfananisha Nyerere na Mungu au Yesu au kumpigia debe jinsi Wakatoliki wa Tanzania wanavyotaka awe mtume.

Tanzania imekuwa huru miaka 46. Nusu ya hiyo miaka, tulikuwa tunaongozwa na Nyerere. Kuna mema mengi na pia kuna mabaya na mapungufu.

Katika moja kubwa ambalo Mwalimu alilijenga na tunalipuuzia kwa kuwa si la kipato au maendeleo mali ni Umoja wa Kitaifa.

Nyerere alikuwa kiongozi wa nchi changa, ambayo ilikuwa inaanza kujiongoza. Ndiyo fikra na mawazo yake yalikuwa makubwa sana hata kwa nyakati zetu. Si dhambi kwake kwa kuwa mwanafunzi wa Historia kutumia elimu yake kujenga mtazamo na hoja za fikra zake.

Nyerere alitoa changamoto, alitoa hutuba, alileta sera. Kuna zilizofanikiwa na zilizoshindwa.

Swali langu kwa wale wanaosema Nyerere hakuleta la maana, je ni lipi mlilonalo la kuijenga nchi yetu?

FMES amediriki hata kudai kuwa na vision ni njozi na talk of change is rhetoric in addition to 23 years of suffrage. Swali kwa Mkuu ES, what alternatives do you have?without vision or ideology how can we claim ourself to be a Nation?

If the only visions we have been using for the last 46 years were Nyerere's or inspired by Nyerere, what were alternatives offered by the likes of Kambona, Kasanga Tumbo or all those listed to be anti-Nyerere? where are their publications so that we can have opposing views to Unyerereism?

If we blame CCM or Nyerere, he stepped down after 23 years, he has been dead (RIP) almost 10 years, what have Watanzania or current CCM people do to provide Watanzania with new fikra, sera and vision?

Sad enough, kuna wazee wangu wawili that I know them personally in addition to the other 2. These guys were known to stand firm when Nyerere wanted to bulldoze people. Malecela and Msuya. Let me add Warioba and Salim. These 4 guys were Waziri Mkuu na Makamu wa Rais. They all have tried to become Rais wa Muungano, but even in Nyerere's absence, wamedhihakiwa, kukejeliwa na kuaibisha na kuvunjiwa utu wao. Je kama walimdindia Nyerere, inakuwaje wanashindwa kuondoka CCM na kuanzisha harakati zao kutumia mawazo yao kuwapa Watanzania alternative kutoka zile fikra mbofumbofu za Nyerere?

Naomba ninukuu sehemu iliyonigusa sana kwenye hii hotuba
For a revolution has begun in Africa. It is a revolution which we hope to control and channel so that our lives are transformed. It is a revolution with a purpose, and that purpose is the extension to all African citizens of the requirements of human dignity. The task before us is a big and complicate one. In the process we shall have many decisions to make which involves clashes of principle – where we have to choose, let us say, between rapid development and individual freedom, or between efficiency and equality. There is and will be no simple o universal answer to such problems; the choice will have to be made in the light of historical circumstances and the conflicting needs of present and future.

Nikiangalia matamshi haya, mimi nayaona kama ni challenge ambayo ni evident mpaka leo.

Sisi tunataka njia fupi ama tunapumbazwa na mazingira ya ugenini na kutaka tupate mafanikio ya overnight "overnight success and sensation". Tulitaka Nyerere afikirie, aende shamba, avune na atafune.

No we need to take advantage of opportunity and define ourselves as a Nation and Continent.

The question that I will throw to FMES, Kitila, Bin Maryam and Kuhani, since Nyerere departed this earth, what efforts have been made to correct his shortcomings? are we waiting for the day CCM falls? what if CCM does not fall in next 25 years, will we continue to blame Nyerere and the foundation? Should it be time to pick what he said about change even if it may be difficult and we may differ on our approaches (principles)?
 

Tutaendelea kwenye mjadala wa fikra za Nyerere. Tumeiona ya kwanza kuhusu change na hitimisho ni kuwa hakuna aliyekataa susbtance ya hotuba hiyo. Wengi ambao wanapinga wanapinga kwa sababu aliyesema ni Nyerere.

Mkuu wangu MMJ,

Unaweza kuendelea na agenda yako, lakini kama nia yako ni a fair debate na mawazo ya Mwalimu, sioni mahali popote kwenye mawazo yako na yake, yaani Mwalimu, kuanzia unayoyaandika hapa, na yaliyosemwa na yeye mwenyewe miaka nenda miaka rudi, ambayo tumeyasikia maisha yetu yote na hata kuyaishi, umeweza kuya-relate na maisha ya m-Tanzania,

so far kwangu mimi, the more you right hizo imaginations, ni more it is becoming clear kuwa ni kwa nini alishindwa kwa mengi, kuacha machache mazuri aliyoweza, sasa for you kusema mmeshindwa, meaning kwamba wewe ndiye umeweza ni dharau kubwa kwa uwezo wa mawazo ya wananchi wengine hapa JF na hasa walioshiriki huu mjadala so far, na inajisema yenyewe utakapokuwa kiongozi huenda utakuwa ni namna gani, maana haiwezi kuwa tofauti na Mwalimu mwenyewe, that is ver scaring!

Otherwise, unaweza kuendelea
.
 

so far kwangu mimi, the more you right hizo imaginations, ni more it is becoming clear kuwa ni kwa nini alishindwa kwa mengi, kuacha machache mazuri aliyoweza, sasa for you kusema mmeshindwa, meaning kwamba wewe ndiye umeweza ni dharau kubwa kwa uwezo wa mawazo ya wananchi wengine hapa JF na hasa walioshiriki huu mjadala so far, na inajisema yenyewe utakapokuwa kiongozi huenda utakuwa ni namna gani, maana haiwezi kuwa tofauti na Mwalimu mwenyewe, that is ver scaring!

Otherwise, unaweza kuendelea
.

mzee, hoja iliyokuwapo ni ya kuangalia substance ya alichosema mwalimu. Nothing more and nothing less. Mjadala mkubwa umekuwa how Mwalimu failed to implement his ideas; Jinsi gani idea hazikugeuka vitendo n.k Lakini kwenye substance ya kile kilichosemwa haijaoneshwa kuwa ni fikra potofu na ambazo zinapaswa kupuuzwa. Hatimaye wachache tumekubaliana kuwa substance ya hilo ni valid jinsi ya kuimplement ni suala jingine.

Sasa mimi kusema "mmeshindwa" siyo kwa maana ya mtu kutokuwa na uwezo kama unavyotaka kuimply bali kwa kuangalia hoja iliyopo haijaoneshwa kuwa fikra hizo za Mwalimu zilikuwa na makosa. Sasa kusema mtu kashindwa si tusi au dharau bali kutangaza kitu kilichodhahiri.

Mtu akinionesha mahali kuwa "nimeshindwa" kuprove kitu sichukii wala sioni ni dharau bali nakubali kuwa nimeshindwa kufanya jambo fulani. Kukubali makosa si udhaifu ndio maana Nyerere aliweza kukubali makosa na kutoa hotuba yake ndefu ya "Things we Must Correct".

Basi naomba niendelee na theme ya pili. Siyo kusudio langu kumkwaza mtu lakini if it happens kuna vitu vichache sana ninavyoweza kuvifanya for I can only control me linapokuja suala la kureact kwa vitu mbalimbali. Kama hisia zako zimeumizwa pole na nitajitahidi kuwa mwangalifu zaidi mbeleni Mkuu.

Tusonge mbel.
 
Yaani nimechoka mwenyewe na kinachoendelea hapa. Inaonekana huyu Nyerere hata akianzishiwa thread ya kuelezea mabaya yote ya utawala wake kama vile nilivyoanza hapa na watu wakaleta mambo yote ya utawala wake yakiwemo mazuri na mabaya lakini bado kutakuwa na kundi kubwa la watu wanaotaka kuona the guy akifutwa kabisa toka kwenye historia ya Tanzania ili mizimu ya Tanganyika itulie

Kwa kuona hili na kujaribu kustay sane, mimi narudi kule kule ambako nimekuwa for the last 10 yrs. Staying away from Nyerere na ccm yake as far as I can.

Mwanakijiji na FMES, endeleeni na thread hii ili tupate elimu ya kutosha wengine ambao hatumjui Nyerere that much. Katika maisha haya nimekutana na watu wanaompenda Nyerere dearly na kuna wale wanaomchukia to the same extent. There is nothing wrong with either side... coz there is nothing wrong with saying or staying for what you believe in. Kama usipokuwa na msimamo katika maisha basi kila kitu kinayumba na katika hili nawatakia kila heri.

Thanks very much!
 
Back
Top Bottom