Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 56
MWK: Kitu ambacho umeki-miss hapo ni kwamba huko kote ulipokutaja hawakubadilisha kiongozi tu, walibadilisha vyama. Kwa maana ingine ni kwamba walibadilisha mfumo, yaani walibadilisha mvinyo na chupa. Sisi tumekuwa tukibadilisha chupa pekee na kuendelea kunywa mataputapu hayohayo. Ndio maana nami nasema hapa kila siku kwamba kosa tunaloendelea kufanya watanzania wenzangu ni kufikiri kubadilisha watu katika CCM bila kuitoa CCM yenyewe itatusaidia. Kwa hiyo nafikiri unaweza kupata picha kwa nini sisi tumebaki hivyohivyo hata miaka 23 baada ya mwalimu kuondoka. Kwa maneno mengine sisi hatujawahi kufanya mabadiliko. Labda itabidi "tumkope" Barack Obama aja atusaidie kueleza maana ya mabadiliko.
Kitila,
Hapa nakubaliana nawe moja kwa moja. Kitu kikubwa hapa ni kubadili chama. CCM ikitoka madarakani, haya yote yatakuwa na mwisho (angalia mfano wangu wa Kenya na Zambia).
Tatizo ni kuwa kuna baadhi ya wanaccm wanadhani kuwa mimi au wapinzani tutafaidika kwa kumtetea Nyerere. Kati ya watu ambao wangependa Nyerere afutwe kwenye historia ya Tanzania ni mimi. Lakini, inakuja reality kuwa, the guy is dead, hakuna chochote anachofanya leo ambacho kinaathiri maisha yangu au ya watoto mamilioni wanaosuffer kule Tanzania.
Kila mara ninakuja kwenye rescue ya Nyerere kwa sababu watu wengi hapa (ukianza na yule mtetezi mkuu wa Lowasa - Mchambuzi) wanataka kushift blames kwa Nyerere. Wao wanataka watu wakubali kuwa matatizo yetu ya leo Tanzania tunayastahili kwa sababu ni Nyerere ndiye aliyetuletea.
Watu makini wanaweza kubadili nchi yao hata kama kiongozi wa nchi yao amefanya mabaya kiasi gani (chunguza post Reagan, Carter, and Thatcher admin). Katika hili, sikubaliani kabisa na watu wanaotaka niamini kuwa matatizo yangu ya leo ni kwa sababu ya Nyerere. Katika hili nitakataa hadi mwisho.
Ninaamini kabisa kuwa Tanzania ingeweza kuwa imebadilika miaka 20 tangu Nyerere atoke madarakani na karibu 10 tangu kifo chake. Na pia naamini kuwa (ukichukulia na walichofanya kina Mkapa na Kikwete), Nyerere alikuwa na best intention kwa watanzania ila wazazi wangu na wengine wote waliokuwa hai miaka hiyo hawakufanya pia part yao.
Thanks!