Dr. Namala Mkopi (kiongozi wa MAT) afikishwa mahakama ya Kisutu

Kiongozi wa madaktari nchini Dr. Namala Mkopi (daktari bingwa wa watoto),amefikishwa katika mahakama ya Kisutu asubuhi hii kujibu shutuma za uchochezi na kupuuza amri ya mahakama ya kusitisha mgomo wa madaktari unaoendelea nchini.

N.B. Mgomo huo haukunzishwa na MAT, ulianzishwa na inayoitwa Jumuiya ya Madaktari chini ya kamati inayoongozwa na Dr. Ulimboka, na kuungwa mkono na madaktari nchini.

Tusubiri kuona hili saga litakavyoendelea....

Keep your friend close and your enemies closer. Don Coleorne

Hapa naona ni baada ya ile mbinu yao ya teka, peleka mabwepande, ua kushitukiwa/kushindikana.
 
Kaka, tangu lini mbwa wakawa na akili ya kufikiri binafsi zaidi ya kuamrishwa tu hata na mlevi so long as mlevi ndiye mwenye mbwa!

Ni kweli Mkuu, maana sifahamu kisheria kama naweza kushtakiwa kwa kosa alofanya jirani yangu kwa sababu tu jana nilionekana naye maeneo fulani !!!!
 
Madaktari wote waliokwenye mgomo na kuacha ndugu zetu wakifa hovyo nawaona kama mazuzu tu
Matatizo ya kupenda dezo, ubwabwa, kofia, kanga, fulana. Ukasahau utu wako afadhali hata CD inafanya hivyo kwa shida tu.
 
Kiongozi wa madaktari nchini Dr. Namala Mkopi (daktari bingwa wa watoto),amefikishwa katika mahakama ya Kisutu asubuhi hii kujibu shutuma za uchochezi na kupuuza amri ya mahakama ya kusitisha mgomo wa madaktari unaoendelea nchini.

N.B. Mgomo huo haukunzishwa na MAT, ulianzishwa na inayoitwa Jumuiya ya Madaktari chini ya kamati inayoongozwa na Dr. Ulimboka, na kuungwa mkono na madaktari nchini.

Tusubiri kuona hili saga litakavyoendelea....

Keep your friend close and your enemies closer. Don Coleorne
Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi au kuanza kutoa majibu ya anachotakiwa kukijibu yeye mahakamani .......ana akili timamu na atajibu hivyo ila ninachojiuliza na nimeuliza wenzangu humu bila kupata majibu ni kwamba.....je alipopata court order aliitekeleza?? Mtasema hakuwa ameitisha mgomo yeye lakini wanachama wake (MAT- Chama kinachotambuliwa kisheria) walikuwa katika mgomo na amri ya mahakama ilimtaka awatangazie kuwa mgomo ni batili hadi mahakama itakapofanya uamuzi wa shauri lililopo mbele yake.....na je katika kutekeleza amri hiyo ..yeye binafsi alikwenda kazini??
 
Madaktari wote waliokwenye mgomo na kuacha ndugu zetu wakifa hovyo nawaona kama mazuzu tu
Nakukumbusha kuwa Thread ni hii Dr. Namala Mkopi kiongozi wa mat afikishwa mahakama ya kisutu asubuhi hii

huo mchango wako uanzishie thread yake!!!
 
Nendeni mkamuwekee dhamana maana hana cha kujibu hapo, mahakama imeishaigiliwa na mhimili mwingine wa DOLA katika maamuzi.
Mahakama ikitaka kutenda haki itoe tamko juu ya DOLA kuingilia mhimili wake, inaonekana mahakimu wetu wanasukumwa na DOLA katika kutekeleza majukumu yao? Jaji mkuu alishasema kuwa serikali inaingilia mahakama.
Mwisho kinachotakiwa ni vitendea kazi mahospitalini siyo kuandama mtu mmoja mmoja kisa Daktari.
Management by FEAR! Aende kutishwa tu lakini tuchunge MABWEPANDE
 
u r right,,serikali inajaribu kutumia mbinu zote kuwatisha na kuvuruga mshikamano wao. Kimsingi hata kutekwa,kupigwa kwa dr ulimboka ilikuwa mojawapo ya mbinu ya ccm/serikali. Hawakukusudia kumuua bali torture ili kutisha wengine

nani kasema walitaka afe lkn kwa mateso makali ambayo kiongozi atakaekuja badala yake awe kaama hosea
 
Wewe Ndiyo zuzu,jamani ubunge ata wewe unaweza kugombea na kupewa mshahara mzuri kwa hiyo ata madaktari wanaweza kuacha taaluma yao na kwenda kugombea ubunge na kupewa mshahara mzuri,ukiona udaktari haufahi unaweza acha na kwenda kwenye ubunge!

Hapo kwenye red - sasa mbona wameacha na mnawalazimisha???? Mara muwang'oe kucha, meno, muwatese
na sasa mnaanza kuwagawanya kwa kuwapeleka mahakamani mmoja mmoja -

kama hamjali - si muwaache??? IMEKUWALA KWENU - FANI YA DAKTARI NGUMU - WAAMBIE WABUNGE WATIBIE WATU KAMA WANAWEZA.........................SI WANAONA RAHISI???? MBONA WANATUMIA NGUVU??

- Ujuzi ni wao wenyewe
- Madaktari sio wasanii - ndio maana hawataki kwenda kusaini kuwa wako kazini na kukaa tu kama wanavyotuibia Wabunge - wangeweza sana kufanya hivyo - lakini ni WASOMI, WAADILIFU

NARUDIA TENA KAMA NYIE MNA UJUZI - JITIBIENI BASI WENYEWE TUONE... OTHERWISE FANYANI MNAVYOSHAURIWA NA MADAKTARI - NA MUACHE KUWASUMBUA - OTHERWISE SUBIRINI MAANDAMANO YA NCHI NZIMA YA WOTE TUNAOUNGA MKONO MADAI YAO - YES I HAVE SAID IT.:hurt:
 
Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi au kuanza kutoa majibu ya anachotakiwa kukijibu yeye mahakamani .......ana akili timamu na atajibu hivyo ila ninachojiuliza na nimeuliza wenzangu humu bila kupata majibu ni kwamba.....je alipopata court order aliitekeleza?? Mtasema hakuwa ameitisha mgomo yeye lakini wanachama wake (MAT- Chama kinachotambuliwa kisheria) walikuwa katika mgomo na amri ya mahakama ilimtaka awatangazie kuwa mgomo ni batili hadi mahakama itakapofanya uamuzi wa shauri lililopo mbele yake.....na je katika kutekeleza amri hiyo ..yeye binafsi alikwenda kazini??

Kaka, ukitumia akili sana kwenye hili swala kichwa kitakuuma bure. JF siyo tena jamvi la kujadili kwa akili, ni kijiwe cha kupotezea muda tu. Usitegemee kuna mtu atayekupa jibu la maswali yako ya msingi na yenye tija...
 
Vijana Tanganyika si Lybia na mnajidanganya kufikiri hivyo.
Kama wewe ni daktari nenda pale umma wa kariakoo na ujigambe- kama hujararuriwa kama mpira wa kona.

kariakoo kuna watu waelewa sana pengine kukuzidi wewe na wanatambua matatizo ya madaktari kwa upana wake na wanawaunga mkono.....
 
Kaka, ukitumia akili sana kwenye hili swala kichwa kitakuuma bure. JF siyo tena jamvi la kujadili kwa akili, ni kijiwe cha kupotezea muda tu. Usitegemee kuna mtu atayekupa jibu la maswali yako ya msingi na yenye tija...

Sana sana utaishia kutukanwa na kuambiwa umetumwa na Nape......Lol magreat thinkers wa upande mmoja hadi kichefuchefu.....unajiita GT wakati huwezi kujadili jambo objectively??
 
Sana sana utaishia kutukanwa na kuambiwa umetumwa na Nape......Lol magreat thinkers wa upande mmoja hadi kichefuchefu.....unajiita GT wakati huwezi kujadili jambo objectively??

JF ya great thinkërs iliisha rasmi mwezi June mwaka 2010.
 
Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi au kuanza kutoa majibu ya anachotakiwa kukijibu yeye mahakamani .......ana akili timamu na atajibu hivyo ila ninachojiuliza na nimeuliza wenzangu humu bila kupata majibu ni kwamba.....je alipopata court order aliitekeleza?? Mtasema hakuwa ameitisha mgomo yeye lakini wanachama wake (MAT- Chama kinachotambuliwa kisheria) walikuwa katika mgomo na amri ya mahakama ilimtaka awatangazie kuwa mgomo ni batili hadi mahakama itakapofanya uamuzi wa shauri lililopo mbele yake.....na je katika kutekeleza amri hiyo ..yeye binafsi alikwenda kazini??

Majibu ya maswali unayouliza serikali inayo na uzuri Namala is verysmart guy so he will beat them up. Yaani hata sheria hawazijui au? Hivi hajaitisha mgomo na hana taarifa yeyote inayomweleza kuwa kuna wanachama wake walioko kwenye mgomo, atakurupukaje kuanza kusema mgomo batili, je akitoa taarifa hiyo na kumbe waliogoma ni kina Dr. Lucy Nkya (ambaye si mwanachama wa MAT atasemaje, si atakuwa kama Aminiel anayewaambia watu kuwa hamna mgomo wakati ukweli mgomo upo!

je mnafikiri madaktari wote ni wanachama wa MAT, je akisema mgomo umesitishwa kumbe wote wanaoripitiwa kufana kazi ndio wanachama wa MAT si inabidi awaambie wanachama kwa nini amewadhalilisha? Na kumbuka hawezi kutoa maamuzi bila kuitisha mkutano wa dharura je amefanya hivyo? mbona nyie ni mambumbumbu kiasi hicho.?

Ninachojua mahakama imemshitaki yeye kama yeye na si MAT (upumbavu mwingine), je hamna viongozi wengine wa MAT? kwa nini yeye tu?

BTW: I hope weye si mba--tia!
 
Inakuwaje Mwenyekiti wa MAT kushtakiwa kwa kosa la Mwenyekiti wa Jumuiaya ya Maktari. Ina maana Polisi hawaoni kuwa anaweza kuwashinda na kama sheria ingekuwa inaruhusu angewadai fidia. Lakini sheria hairuhusu Mtuhumiwa kudai fidia ndio maana wamemfikisha mahakamani.
Hivi wewe unajua sheria zaidi kuliko DPP na wengine? Ina maana serikali hawajaliona hilo?
 
Ndo maana hata nickname yako ni panadol. Mtuhumiwa namba 1 katika mauji ya watz ni Mr dhaifu.Migomo kila kukicha,huna habari hata walimu walishagoma na matokeo yake yasikilizie baada ya matokeo ya darasa la saba,f4 na form 6!
Kwako ni sawa wagonjwa kukosa dawa,kulazwa zaidi ya 2 kwenye kitanda kimoja,vituo vya afya kukosa magari ya kubebea wagojwa, madaktari kukosa vitendea kazi, WASIRA kusinzia bungeni na kulipwa posho 200,000/= na daktari anayekesha akihudumia Watanzania kulipwa posho 10,000/=, Salma Kikwete kutumia mamilion ya fedha zetu kwa mambo yake,kutumia mabilion ya pesa za watz kwa safari zisizokuwa na tija, kusherehekea miaka 50 ya uhuru,kulipia simina za Ngurdoto na ufisadi wa kutisha kuendelea kuitafuna nchi, twiga na maliasili zingine kuibwa kupitia viwanja vya ndege na wazee wa intelijensia na usalama wa taifa wapo. Panadol tafakari ama tafuta mtandao wa magamba wenzio uchangie huko hapa si mahala pako.
 
Back
Top Bottom