Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Ni Asubuhi tulivu ya siku ya Alhamisi.

Kiongozi mkuu wa Upinzani Freeman Mbowe anatarajiwa kuletwa mahakamani Kisutu Leo katika Kesi ya Ugaidi.

Kesi hii inavuta kila mpenda haki na mwanademokrasia kutokana na ukweli Mbowe amebambikizwa kesi hii ili kumnyamazisha kutokana na Kampeni aliyoasisi ya Kudai Katiba Mpya

Mahakama hii inatarajiwa kufurika umati mkubwa wa watu kulaani unyama na uonevu wa vyombo vya dola.Ikumbukwe ni juzi tu bila Aibu alijitokeza IGP Simon Sirro na kuingilia mhimili wa Mahakama kwa kumhukumu Mbowe huku akijua kesi iko mahakamani.

Watu wengine wanaotarajiwa kufurika Kisutu ni Wawakilishi kutoka Jumuiya ya Ulaya, Marekani na balozi kadhaa nchini huku vyombo vikubwa vya Habari Duniani BBC, VOA, DW na Aljazeera vikitarajiwa kuwa live mahakamani.

Molemo media tayari iko kwenye viwanja vya Mahakama hii kuwaletea kila kinachojiri.

Updates
Imethibitishwa kwamba Freeman Mbowe hataletwa mahakamani na badala yake kesi inaendeshwa kwa njia ya Mtandao (Video Conference)

Taarifa za Uhakika ni kwamba dola Wana hofu kubwa kumleta Mbowe Mahakamani kutokana na Hasira ya wananchi.

Pamoja na vitisho vya IGP Simon Sirro alivyotoa juzi dhidi ya watakaohudhuria mahakamani Kisutu na kuongea uongo mwingi dhidi ya Mbowe lakini Leo idadi kubwa ya watu imehudhuria mahakamani na wengine wakiendelea kumiminika kabla ya kuanza kuondoka baada ya Taarifa kwamba kesi itaendeshwa kimtandao.

Kamanda wa Polisi DSM Muliro Jumanne alifika mapema Kisutu kuona Hali ya mambo huku kukiwa na Askari zaidi ya 100 wenye silaha na wengine waliovalia kiraia.

Pamoja na Serikali kuogopa kumleta Mbowe Mahakamani lakini ni wazi Kelele za umma unaotaka haki zimewatisha na kuwaogofya

Kesi Yaahirishwa
Ilipotimu saa 4 na dakika 20 kesi Imeahirishwa hadi kesho Ijumaa tarehe 6 August saa 3 Asubuhi kutokana na kile kilichoelezwa ni matatizo ya kimtandao

=====



KISUTU, DAR: Kesi ya Freeman Mbowe (CHADEMA) imeahirishwa hadi Kesho kutokana na muonekano hafifu wa Video Conference kati ya Mahakama ya Kisutu na gereza la Ukonga

Watuhumiwa wataletwa kesho saa 3 asubuhi mahakamani (Physically) na taratibu nyingine za kisheria zitafata.

77267334-E65C-4608-B6CF-4823286AED6C.png
 
Mulemule naye kaufayta wakati aliapa kuishauri serikali kwa uaminifu!

Na kuishi kote ughaibuni hajui kuwa wazungu hawana dogo kwenye suala la Amani hasa wanaposokia UGHAIDI. Kuna point tunapoteza hapa halafu wanakuja kutumia nguvu kuimarisha uchumi wa kisiasa!
 
Hivi unamkumbuka mdude alijigamba vipi baada ya kusamehewa? Kiongozi gani anakubali maneno ya kejeli kama hayo. Midomo inawaponza
Kiongozi, Mdude alisamehewa na nani na alisamehewa kutoka katika hatia ipi? Kwa lugha hii, unamaanisha kwamba Mbowe anashikiliwa kama kisasi kwa maneno ya mdude? Utekelezaji wa azma hii ni kifungu namba ngapi cha katiba?

Naomba msiseme maneno mengine yanayoweza kuumba hasira kwa watu dhidi ya serikali. Hakuna serikali inaweza kuwa inakamata watu bila sababu, eti kwa kuwa kuna mtu fulani alisema maneno yasiyofaa. Kama mdude alinena vibaya, kwa nini hakuwajibishwa mwenyewe kw amakosa yake, badala yake atafutwe Mbowe? Unasema Mdude alisamehewa, alikuwa katiwa hatiani na chombo gani kwa kosa lipi na hukumu yake ilikuwa namna gani ambayo sasa akasamehewa?

Maneno mengine mnayoyaandika hapa, yanadhalilisha serikali yetu. Siamini serikali yetu inaweza kuwa na tabia za kiwango cha chini namna hiyo. Serikali ina mammbo mengi ya maana ya kufanya, na hatuna serikali iliyo inferior na insecure kiasi hicho. Hiki ni kiwango chako cha kufikiri na kutenda na ndiyo sababu huwezi kuwa kiongozi wa serikali wewe. Unatia aibu.
 
Mbowe angeanza na katiba ya chama chake wakati wanahangaika na katiba ya nchi wakati katiba yake haiko sawa
 
Back
Top Bottom