Dr. Namala Mkopi (kiongozi wa MAT) afikishwa mahakama ya Kisutu

Wacha twende mahakamani, ni mara ngapi serikali imeshindwa baada ya kushtaki au kushtakiwa?
 
Madaktari wote waliokwenye mgomo na kuacha ndugu zetu wakifa hovyo nawaona kama mazuzu tu

kama mimi navyokuona wewe zuzu unaowaangalia madaktari waliogoma tu huku wale wanaosababisha hospitali zetu kuwa duni,vifaa duni,n.k huku wao wakipongezana kwa rushwa ndogo ndogo,vitafunwa vya mabilioni,magari ya kifahari hata kupelekea madaktari kugoma ukiwa hauwaoni..wewe ukipeleka mgonjwa wako pale ukaambiwa alale chini vitanda hakuna,au usubiri kuna foleni,au hapa hatuna kipimo mpaka india ndio unaona poa eeh!Halafu akifa wa kwanza kusema Madaktari wazembe!!
 
Kinachoendelea sasa hivi ni kuuwa kabisa sekta ya afya.
Kweli mkuu. Tutawapoteza madaktari wengi vijana ambao wataondoka nchini kutafuta kazi wanapothaminiwa. Wengine wataachana kabisa na hii kazi. Wanafunzi wengi ambao bado wako shule za sekondar ambao walikua wanatamani kuwa madaktari watakatishwa tamaa. Inauma sana utawala dhaifu umelifikisha hapa taifa letu!
 
Hivi wewe unajua sheria zaidi kuliko DPP na wengine? Ina maana serikali hawajaliona hilo?

Huyo DPP ameshafungua kesi ngapi mwisho wa siku zikamshinda ikaonekana hana ushahidi wa kutosha? Serikali imebwagwa mara ngapi na kesi ilizofungua yenyewe kupitia kwa huyo DPP?
 
Inakuwaje Mwenyekiti wa MAT kushtakiwa kwa kosa la Mwenyekiti wa Jumuiaya ya Maktari. Ina maana Polisi hawaoni kuwa anaweza kuwashinda na kama sheria ingekuwa inaruhusu angewadai fidia. Lakini sheria hairuhusu Mtuhumiwa kudai fidia ndio maana wamemfikisha mahakamani.

Huu ni uonevu tu sasa!!!:redface:
 
Sasa ndio kitaeleweka kile kinachowasukuma kuwagomea waTanzania licha ya kuwasomesha.
Kama mliajiriwa kwa ajili ya kipato karibuni mitaani kuna pesa hata zaidi ya milioni kumi kwa mwezi.
Katika sakata hili tunasubiri tu kuokota vidole maana hamjui kuwa upande wa pili ndio umeshika mpini.
mwenye mpini anapopukutisha vidole anaonesha alivo hayawani kabisa! Aliyetusaliti ni yule anayeficha hela kule uswisi, aliyechukua hela za epa, mwenye matumizi ya anasa,....nk. Huku akitulazimisha kuamini kuwa selikali haina hela.
 
Ndugu zangu wanawahishwa India sina tabu na hili tatizo
Juzi kulikua na sredi ya kifo aliyekuwa mkuu wa CCP Moshi,kamanda J. Mwesiga. Alikua na uwezo wa kwenda India,SA,hata Ulaya,lakini hakufika huko,alifia hapa kwa tatizo hospitali zetu zingekua na vifaa labda maisha yake yangeokolewa. Magonjwa mengine yanampata mgonjwa kwa kasi ya ajabu,kama hakuna huduma sahihi karibu anapoteza maisha bila kuangalia uwezo wake wa kifedha!
 
duuh!hiii kali yani mwenye kuitisha mgomo mwingine aliyekamatwa na kushitakiwa mwingine hakika hii haiitaji kuwa profesa kugunduwa kuwa kuna ushawishi wa kisiasa katika hili haya ngoja tuone mwisho wa picha hili itakuwaje

Serikali ipo makini sana labda tatizo ni watu wasioweza kuona na kutafsiri mambo. Nawashangaa mnaoshangaa serikali kuacha kumshtaki aliyeitisha mgomo na kumshtaki mtu mwingine.
Aliyeitisha mgomo serikali imeshamshughulikia na sasa hivi ina haha kummalizia, wameamua kumshataki Dr. Mkopi ili kumdhibiti, kwa sababu kitendo chake cha kuandika barua UN kuomba ulinzi kwa Dr. Ulimboka kitasababisha washindwe ku-accomplish misheni yao. Hivyo wanajua wanachokifanya.
Na in no time itatangazwa kupitia mahakama kuwa ni marufuku kwa vyombo vya habari na wananchi kutangaza, kuandika au kusoma habari zinazohusu madaktari na Dr. Ulimboka, kwa kufanya hivyo utahukumiwa adhabu kadiri serikala itakavyoishauri mahakama.
 
Jk alisema ayetaka 3.5milion aache kazi, mbona anawalazimisha sasa? Au yuko tayari kuwapa 3.5m?
 
Kiongozi wa madaktari nchini Dr. Namala Mkopi (daktari bingwa wa watoto),amefikishwa katika mahakama ya Kisutu asubuhi hii kujibu shutuma za uchochezi na kupuuza amri ya mahakama ya kusitisha mgomo wa madaktari unaoendelea nchini.


N.B. Mgomo huo haukunzishwa na MAT, ulianzishwa na inayoitwa Jumuiya ya Madaktari chini ya kamati inayoongozwa na Dr. Ulimboka, na kuungwa mkono na madaktari nchini.


Tusubiri kuona hili saga litakavyoendelea....




Keep your friend close and your enemies closer. Don Coleorne

Safi sana utawala wa sheria uchukue mkondo wake, huo ndio utawala bora kwa hili huyu Dr Uchwara hachomoki, na liwe fundisho kwa ma dr uchwara wengine. Na hukumu ya mahakama iwe ni kukifuta hicho chama cha wahuni wachache wenye kuwa driven na political dreams za CDM

 
ALIPEWA BARUA ikimuamuru kutangaza mbele ya waandishi wa habari akisitisha mgomo lkn hakufanya hivyo! ana kesi ya kujibu ya mauwaji. wagonjwa wengi wamefariki kutokana na mgomo ambao aliubariki kwa kukaa kimya
 
Na hukumu ya mahakama iwe ni kukifuta hicho chama cha wahuni wachache wenye kuwa driven na political dreams za CDM


Hivi kumbe kuna mkono wa siasa katika hili !!! Mimi nilidhani wanajitahidi kuomba vitendea kazi ili Watanzania wote waweze kutibiwa nchini badala ya wengine kupelekwa nje kwa kisingizio kuwa hospitali hazina uwezo ?
 
Majibu ya maswali unayouliza serikali inayo na uzuri Namala is verysmart guy so he will beat them up. Yaani hata sheria hawazijui au? Hivi hajaitisha mgomo na hana taarifa yeyote inayomweleza kuwa kuna wanachama wake walioko kwenye mgomo, atakurupukaje kuanza kusema mgomo batili, je akitoa taarifa hiyo na kumbe waliogoma ni kina Dr. Lucy Nkya (ambaye si mwanachama wa MAT atasemaje, si atakuwa kama Aminiel anayewaambia watu kuwa hamna mgomo wakati ukweli mgomo upo!

je mnafikiri madaktari wote ni wanachama wa MAT, je akisema mgomo umesitishwa kumbe wote wanaoripitiwa kufana kazi ndio wanachama wa MAT si inabidi awaambie wanachama kwa nini amewadhalilisha? Na kumbuka hawezi kutoa maamuzi bila kuitisha mkutano wa dharura je amefanya hivyo? mbona nyie ni mambumbumbu kiasi hicho.?

Ninachojua mahakama imemshitaki yeye kama yeye na si MAT (upumbavu mwingine), je hamna viongozi wengine wa MAT? kwa nini yeye tu?

BTW: I hope weye si mba--tia!

He...ivi mahakama huwa inashitaki??

Kwa ufahamu wa namna hii angalieni huyu mnayemtetea asijelamba mvua ambayo hakuitegemea.....Chezea vitu vingine vyooote lakini sio mahakama.
 
Watu wanadai vitendea kazi, nyie mnawashtaki.
Madaktari rudini tu kazini, kwani si kila mmoja anayo lap top,
nendeni tuwe tunabadilishana mawazo humu jf. Kama hakuna hata vya
kupimia homa nini zaidi.

Please rudini tu kazini.

Hivi wakisema wanajiuzulu wote pia watashitakiwa !
 
ALIPEWA BARUA ikimuamuru kutangaza mbele ya waandishi wa habari akisitisha mgomo lkn hakufanya hivyo! ana kesi ya kujibu ya mauwaji. wagonjwa wengi wamefariki kutokana na mgomo ambao aliubariki kwa kukaa kimya

tunaposema baadhi ya watanzania ni wajinga wewe ni mmoja wapo....bado una nafasi ya kupanua fikra na ndio maana nakuweka kundi la wajinga na si wapumbavu... serikali kwa mara kadhaa imesema na kutanga mgomo umekwisha na huduma zimerejea...Namala Mkopi aliitisha mkogo? hivi unajua mipaka ya kazi yake? ...serikali yako dhaifu imeshachukua hatua ya kuwafukuza madaktari walio kwenye mafunzi na sasa kila mmoja alefunguliwa mashitaka..sasa wanachotafuta kwa Dr Namala ni kitu gani wakati wao walishachukua hatu?...
 
He...ivi mahakama huwa inashitaki??

Kwa ufahamu wa namna hii angalieni huyu mnayemtetea asijelamba mvua ambayo hakuitegemea.....Chezea vitu vingine vyooote lakini sio mahakama.

Dr.Namala amepelekwa mahakamani kama njia ya kumtisha juu ya barua iliyowasilishwa UN.....ni njia ya kumtisha yeye na wengine...atashida kesi hiyo kwa kishindo na aibu kubwa kwa serikali...kusema kwamba anashitakiwa kwa kosa la kutokutii amri ya mahakama ni lugha tu wanayotumia watawala dhaifu
 
Safi sana utawala wa sheria uchukue mkondo wake, huo ndio utawala bora kwa hili huyu Dr Uchwara hachomoki, na liwe fundisho kwa ma dr uchwara wengine. Na hukumu ya mahakama iwe ni kukifuta hicho chama cha wahuni wachache wenye kuwa driven na political dreams za CDM

Sitaki kuamini kama hii Move iko supported na CHADEMA na endapo itakuwa hivi for the first time nitawadharau sana.....ninachokiona humu jukwaani wapo wanaotaka kuiharibia CDM kwa kuihusisha na huu uvunjaji wa sheria, dharau kwa amri ya mahakama na umma wa walalahoi wa nchi hii kwa kodi zao zilizotumika kuwasomesha hao madaktari....i will be the last person kuamini kuwa chadema wanahusika na nikithibitisha hilo i will withdraw my love and support to CDM
 
Kiongozi wa madaktari nchini Dr. Namala Mkopi (daktari bingwa wa watoto),amefikishwa katika mahakama ya Kisutu asubuhi hii kujibu shutuma za uchochezi na kupuuza amri ya mahakama ya kusitisha mgomo wa madaktari unaoendelea nchini.


N.B. Mgomo huo haukunzishwa na MAT, ulianzishwa na inayoitwa Jumuiya ya Madaktari chini ya kamati inayoongozwa na Dr. Ulimboka, na kuungwa mkono na madaktari nchini.


Tusubiri kuona hili saga litakavyoendelea....




Keep your friend close and your enemies closer. Don Coleorne

LIWALO NA LIWE yameanza kutimia ss
 
Nafikiri ni vizur watu wa Tz kuelewa nchi yenu inaongozwa kwa Rules of Law. Kwa misingi hiyyo kila muhimili unajitegemea katika kuendesha nchi. yaani Mahakama, Serikali na Bunge. Na vyote haviwezi kungiliana katika maamuzi.

Fuateni sharia mlizojitungia wenyewe katika Katiba yenu

Ndugu yangu Katiba ya sasa hatukutunga sisi, ya kwetu ndio tunaandaa muda huu.
 
Back
Top Bottom