Dr. Namala Mkopi (kiongozi wa MAT) afikishwa mahakama ya Kisutu

Nendeni mkamuwekee dhamana maana hana cha kujibu hapo, mahakama imeishaigiliwa na mhimili mwingine wa DOLA katika maamuzi.
Mahakama ikitaka kutenda haki itoe tamko juu ya DOLA kuingilia mhimili wake, inaonekana mahakimu wetu wanasukumwa na DOLA katika kutekeleza majukumu yao? Jaji mkuu alishasema kuwa serikali inaingilia mahakama.
Mwisho kinachotakiwa ni vitendea kazi mahospitalini siyo kuandama mtu mmoja mmoja kisa Daktari.

Kimsingi tafasiri ya kesi hii umegibikwa na utata,mahala kesi hii ilipofunguliwa na jaji anayesikiliza, atoe amri hii hiyo .napata shida amri ya kwanza imetolewa na mahakam kuu, hati ya kukamatwa kwake imetolewa na mahakama ya kisutu na kesi kuwa mahakama ya kisutu .tfasiri hii inanipa tabu kidogo.Jinai hiyo nafikiri ingeonekana kwenye mahakama kuu na si mahakama nyingine ambako kesii haikufunguliwa.Pia kama kuna utofauti wa MAT na jumuiya ya madakitari , hapa haki iko wapi?kesi inasema MAT huyu anayekamatwa ni wa jumiya ya madaktari , huku ni kulazimaisha kuwa raisi anataka kuua madaktari wote.Kimsingi raisi kapotoka suala hili mbona bado mahakam ya kazi haijatoa uamuzi polisi na mwendesha mashitaka wanaamza kesi nyingine, maake wameizalau kesi ya msingi basi.Pia ukiangalia bila ushabiki tatizo la mgomo huu haliwezi kumalizwa na mahakama, bali na hekima yenye busara maridhawa.hao wanazuoni wa madhehebu ya dini wako wapi nao wamepewa rushwa?
 
Wacha twende mahakamani, ni mara ngapi serikali imeshindwa baada ya kushtaki au kushtakiwa?

huwezi kuamini hata yel jamaa waliyesema ameeneza uzushi kuwa kuna kontena la kura bandia liko huko mbeya nae alishinda kesi.....kwa maana hiyo kura bandia ziliingia nchini!!!
 
Kiongozi wa madaktari nchini Dr. Namala Mkopi (daktari bingwa wa watoto),amefikishwa katika mahakama ya Kisutu asubuhi hii kujibu shutuma za uchochezi na kupuuza amri ya mahakama ya kusitisha mgomo wa madaktari unaoendelea nchini.

N.B. Mgomo huo haukunzishwa na MAT, ulianzishwa na inayoitwa Jumuiya ya Madaktari chini ya kamati inayoongozwa na Dr. Ulimboka, na kuungwa mkono na madaktari nchini.

Tusubiri kuona hili saga litakavyoendelea....

Keep your friend close and your enemies closer. Don Coleorne

Kwani kuna mgomo wa madaktari?? Mbona mgomo bado haujaanza?? UKIANZA MTAONA....amini wanajamii, siku madaktari wakigoma, dunia itajua
 
Asiwe na wasiwasi kabisa huyu Dr. Namala, kwani haki ipo japo hucheleweshwa, serikali wanahaha tu sasa hivi kwani kila kitu kimekaa vibaya. Na inaonekana uwezo wao wa kufikiri juu ya jambo hili umefika mwisho au pengine damu na mateso aliyopata ulimboka yanawapa uchizi. Maana sasa wamezidi vituko na kukosa uelewa.
 
Nafikiri ni vizur watu wa Tz kuelewa nchi yenu inaongozwa kwa Rules of Law. Kwa misingi hiyyo kila muhimili unajitegemea katika kuendesha nchi. yaani Mahakama, Serikali na Bunge. Na vyote haviwezi kungiliana katika maamuzi.

Fuateni sharia mlizojitungia wenyewe katika Katiba yenu
Haya huyawezi, nenda kashiriki mjadala wa kizushi wa mzee mwenzio Mohamed Said kuwa waislam wanaonewa!
 
tunaposema baadhi ya watanzania ni wajinga wewe ni mmoja wapo....bado una nafasi ya kupanua fikra na ndio maana nakuweka kundi la wajinga na si wapumbavu... serikali kwa mara kadhaa imesema na kutanga mgomo umekwisha na huduma zimerejea...Namala Mkopi aliitisha mkogo? hivi unajua mipaka ya kazi yake? ...serikali yako dhaifu imeshachukua hatua ya kuwafukuza madaktari walio kwenye mafunzi na sasa kila mmoja alefunguliwa mashitaka..sasa wanachotafuta kwa Dr Namala ni kitu gani wakati wao walishachukua hatu?...

wanachotafuta ni kumuadabisha ili aache kuchezea maisha ya watu. akome kabisa. we subiri hukumu inakuja. chezea serikali wewe!
 
Nafikiri ni vizur watu wa Tz kuelewa nchi yenu inaongozwa kwa Rules of Law. Kwa misingi hiyyo kila muhimili unajitegemea katika kuendesha nchi. yaani Mahakama, Serikali na Bunge. Na vyote haviwezi kungiliana katika maamuzi.

Fuateni sharia mlizojitungia wenyewe katika Katiba yenu

Hiyo kitu haipo wala hatujawahi kujitungia katika katiba yetu! Labda upo Timbuktu huko Mali.
 
Mungu yupo...ata Roma haikujengwa kwa siku moja penye kudai haki uongo hujitenga..uzen magorofa mnayojenga kama miti kila mkoa na masheli makubwa kwa kodi za watanzania mmboreshe maslahi,mazingira ya kufanya kazi na mishahara ya kaka,dada,baba na mama zetu...kuna siku watachoka..dunia imebadilika jamani watawala..
IN GOD WE TRUST
 
Kiongozi wa madaktari nchini Dr. Namala Mkopi (daktari bingwa wa watoto),amefikishwa katika mahakama ya Kisutu asubuhi hii kujibu shutuma za uchochezi na kupuuza amri ya mahakama ya kusitisha mgomo wa madaktari unaoendelea nchini.

N.B. Mgomo huo haukunzishwa na MAT, ulianzishwa na inayoitwa Jumuiya ya Madaktari chini ya kamati inayoongozwa na Dr. Ulimboka, na kuungwa mkono na madaktari nchini.

Tusubiri kuona hili saga litakavyoendelea....

Keep your friend close and your enemies closer. Don Coleorne

watawala wa hii tanganyika hawana akili kabisa,wana upeo finyu sn wa kuchambua mambo,sio hao kweli walio utangazia umma wa watz kuwa mgomo umekwisha,sasa iweje tena wamkamate tena huyo dr kw mgomo ambao haupo?embu zomba,greenstar,webondo,ritz wawasaidie mawazo magamba wenzao wajarib kudeal na tatizo na sio watu
 
Kwanini wamlazimishe kutoa tangazo la kusitisha mgomo wakati sio yeye aliyetangaza mgomo, naona serikali inachezea kodi zetu kwa kesi amabazo huna hata hja ya kuweka wakili kushinda.

Shida ya madaktari wetu wanafikiri sheria inaogopa udaktari wao, kwanza ni kwanini hakutii amri ya mahakama? hivi mnajua ni kwanini serikali ilikimbilia mahakamani? nimeamini ndo maana wanasheria wanamuita layman mtu yeyote ambaye hajasoma sheria! hiyo kesi itamsumbua na asipoangalia anafungwa, anafikiri kuna faini hapo, ooh chezea sheria weye....
 
hwaw ogopeni Mungu madaktari na serikali,mnapogombani ninyi sisi ndio tunaoumia.Chonde chonde viongozi wa dini saidieni serikali maana hawa wote sasa hatujui yupi kichaa wote wanafukuzana uchi.,mwenye nguo na anayekimbia nazo hatujui yupi si kichaa.Aanzishe mgomo mwingine ashitakiwe mwingine sas tueleweje?/??????
 
Sawa kabisa nimefurahi kusikia hivyo na bado tunaiomba serikali iwachukulie atua madaktari wote waliogoma na kusababisha vifo vya watanzania wenzetu,ujue unaweza unga mkono mgomo wa madaktari na kuufurahia kiushabiki kwa sababu kifo kutokana na mgomo huu hakijamkuta ndugu yako wa karibu au huna huruma na binadamu wenzako lakini kama yangekukuta nafikiri katika hali ya kawaida ungeungana na watanzania wengi kupinga mgomo wa madaktari na yeyote atakayejifanya anahamasisha watu kuandamana kuipinga serikali atua inazochukua dhidi ya madaktari waliovunja sheria huyo atakuwa ni mwendawazimu na hafahi kuitwa binadamu ni mnyama kwa nini asihamasishe maandamano kipindi kile cha mgomo kuwashinikiza madaktari warejee kazini ili kuokoa maisha ya watanzania waliokuwa wanaumwa! Jamani migomo yote hapa nchini ni ya kisiasa inachochewa na inafadhiliwa na chadema ili kuifanya serikali ya CCM ionekane haiwajali wananchi wake lengo kuidhoofisha CCM kisiasa na kuijenga Chadema ili wananchi wawaone chadema ndiyo wanafaa kushika dola,Ewe mtanzania makini na mzalendo popote ulipo chukua hatua ya makusudi kuelimisha jamii iliyokuzunguka kuikataa chadema kwa namna yoyote ile ili kulinda Amani,Umoja na mshikamano wa watanzania !

Yaani kama jina lako lilivyo - panadol, na huenda unaumwa sasa sijui utajitibia vipi na wewe ndiye panadol.

Au umerogwa?????

MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Hawo wanaoishabikia serikali ni wajinga,hivi watu wanakufa kwa kukosa madoc au madawa na vifaa vingine??????,mfa maji haachi kutapatapa,mnampeleka daktari bingwa mahakamani ili iweje?????????????????seri kali haina ufahamu wala adabu,mwisho wao unaanza kuelekea ukingoni. Mahakama zinaongozwa na ikulu...............kumbe Lema hakukosea
 
Yani Mahakama imempa cheo cha Dr.Ulimboka na kumshitaki juu. Kuna haja ya Nguvu ya Umma nayo ku-excercise power yake. Maana hatuoni umakini wowote katika kushughulikia tatizo hili linalotuumiza sana sisi makabwela.

Mwaka huu utajiuliza maswali na kujijibu hadi ukome! Ndo mawakili wetu hao na akili zao za kuandaa mashtaka kama ya kesi ya kina Zombe.
 
Shida ya madaktari wetu wanafikiri sheria inaogopa udaktari wao, kwanza ni kwanini hakutii amri ya mahakama? hivi mnajua ni kwanini serikali ilikimbilia mahakamani? nimeamini ndo maana wanasheria wanamuita layman mtu yeyote ambaye hajasoma sheria! hiyo kesi itamsumbua na asipoangalia anafungwa, anafikiri kuna faini hapo, ooh chezea sheria weye....

layman unaweza kuwa hata wewe. Kama wewe ni mkrsito umeshawahi kusikia neno WALEI? Hiyo ndiyo kiswahili cha neno 'layman', maana kwa kanisa, mtu ambaye sio Padri au askofu, ni layman. na hivyo hivyo, kwa madaktari, majaji, mahakimu etc ni layman tu inapokuja kwenye mambo ya tiba!
 
Kiongozi wa madaktari nchini Dr. Namala Mkopi (daktari bingwa wa watoto),amefikishwa katika mahakama ya Kisutu asubuhi hii kujibu shutuma za uchochezi na kupuuza amri ya mahakama ya kusitisha mgomo wa madaktari unaoendelea nchini.

N.B. Mgomo huo haukunzishwa na MAT, ulianzishwa na inayoitwa Jumuiya ya Madaktari chini ya kamati inayoongozwa na Dr. Ulimboka, na kuungwa mkono na madaktari nchini.

Tusubiri kuona hili saga litakavyoendelea....

Keep your friend close and your enemies closer. Don Coleorne

Lazima nikiri kwamba mimi siyo mwanasheria lakini hii haimanishi kuwa mimi siwezi kutumia akili ya kawaida kabisa kukosoa haya mashitaka. Mimi nadhani haya mashitaka ni ya kuumba na yamekiuka misingi ya kisheria na utawala bora. Nijuavyo mimi ni kwamba mahakama ya kazi ilitoa amri ya kusitisha mgomo wa madaktari. Nilitarajia basi mahakama hiyohiyo iliyotoa amri ya kusitisha mgomo pamoja na amri elekezi ndiyo ingekuwa imetoa warrant of arrest kwa Mkopi kwa kushindwa kutekeleza amri ya mahakama. Hivyo ndivyo ambavyo angefikishwa mahakamani for, lakini siyo kufunguliwa mashitaka haya ya uchochezi. Kosa ni kwamba polisi walimwita jana kituo cha kati, wakamhoji au wakachukua maelezo na hayo ndiyo maelezo waliyoyatumia kuandaa hati ya mashitaka au kubainisha makosa aliyokiuka. Kitu cha muhimu polisi walitakiwa waseme tunayo amri ya mahakama ya kazi ya kumkamata kiongozi au viongozi wa madaktari kwa kutotekeleza amri ya mahakama. Lakini pia lazima ikumbukwe kuwa amri ilikuwa juu ya MAT as an office na siyo mtu mmoja as an individual. Waliotakiwa kushitakiwa leo kwa kukiuka amri ya mahakama ni taasisi/ofisi nzima za MAT wakiwemo wadhamini au bodi ya MAT na siyo Mkopi peke yake. swali polisi wametumia kigezo gani kumwona Mkopi ndiye mtendaji na msemaji mkuu badala ya katibu au kamati ya utendaji ya MAT? Mimi namshauri Mkopi asihofu kwani hii kesi haina mashiko kabisa haiwezi kufika popote kusudio lake ni kumtisha tu lakini kesi haina merit/legal stand.
 
Back
Top Bottom