CHADEMA na mikakati ya kujiimarisha kanda ya Pwani na Zanzibar

Tunakuja Zenji hivi punde,usijali mkuu.Chama chetu ni mikakati na muda ukifika,chombo kitakuja huko tu. M4C is for the whole of Tanzania na kila sehemu itafikiwa kabla ya 2015 hivyo CCM na wapambe wao CUF hawana pa kujificha.
 
Wana jf mimi hawa CDM siwaelewi kabisa. Huku visiwani bado nguvu yao ni ndogo mno sasa kuelekea 2015 ni vyema mh.Mbowe na team yake wakajipanga mapema kusudi M4C isiieshie tu bara tukumbuke rais wa jamhur ya muungano huchaguliwa kote bara na visiwani na hawa magamba wanaweza kutumia advantage ya ZNZ kujiongezea kura.
 
Waende Zanzibar halafu watamuachia nani minyukani ndani ya JF. Jamaa wamekosa dira na wanachoweza sasa ni kuchafuana na kueneza umbea tu. Halafu eti uipe nchi mijitu isiyo na upeo kama hii. Kwa hali hii, sioni ajabu CCM ikiendelea kutawala hadi Yesu anarudi.
 
hata vikombe kabatini huwa vinagongana
 
Vuaneni nguo majirani wafurahie sinema ya bure

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Waende Zanzibar halafu watamuachia nani minyukani ndani ya JF. Jamaa wamekosa dira na wanachoweza sasa ni kuchafuana na kueneza umbea tu. Halafu eti uipe nchi mijitu isiyo na upeo kama hii. Kwa hali hii, sioni ajabu CCM ikiendelea kutawala hadi Yesu anarudi.

Mmmh, kuna ukweli katika maneno yako japo kuteleza si kuanguka, twaja zenji na twanga kotekote
 
Wazo na ushauri mzuri sana. CDM wanapaswa kujifunza toka kwa CUF vinginevyo kama wanataka kugeuzwa nyumba ndogo kama Sharriff waendelee kuipuuzia Zenj.
Wana jf mimi hawa CDM siwaelewi kabisa. Huku visiwani bado nguvu yao ni ndogo mno sasa kuelekea 2015 ni vyema mh.Mbowe na team yake wakajipanga mapema kusudi M4C isiieshie tu bara tukumbuke rais wa jamhur ya muungano huchaguliwa kote bara na visiwani na hawa magamba wanaweza kutumia advantage ya ZNZ kujiongezea kura.
 
Zanzibar hawana haja ya chadema,ccm,cuf wala tlp,haja yao z'br huru yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa.
 
Wana jf mimi hawa CDM siwaelewi kabisa. Huku visiwani bado nguvu yao ni ndogo mno sasa kuelekea 2015 ni vyema mh.Mbowe na team yake wakajipanga mapema kusudi M4C isiieshie tu bara tukumbuke rais wa jamhur ya muungano huchaguliwa kote bara na visiwani na hawa magamba wanaweza kutumia advantage ya ZNZ kujiongezea kura.

Nyie si ndo kila siku mnalia muachwe mpumuwe? Kumbe mnapenda muungano eeh? Haya twaja Zanzibar
 
Waende Zanzibar halafu watamuachia nani minyukani ndani ya JF. Jamaa wamekosa dira na wanachoweza sasa ni kuchafuana na kueneza umbea tu. Halafu eti uipe nchi mijitu isiyo na upeo kama hii. Kwa hali hii, sioni ajabu CCM ikiendelea kutawala hadi Yesu anarudi.

''Salia tunguri pm 7'' nadhani panakufaa
 
MBALI na kukosa ushawishi katika siasa za Zanzibar ikilinganishwa na Bara ambako imewekeza nguvu kubwa kwa muda mrefu, sasa
Chadema imeamua kuitenga Zanzibar. Moja ya dalili za hatua hiyo ni sera yake ya majimbo inayokwenda sambamba na kuondoa
wakuu wa mikoa, ambayo haiihusu Zanzibar kwa namna yoyote ile.

Chadema katika maoni yake ya Katiba mpya, viongozi wake walitaka Katiba hiyo ianzishe majimbo yasiyozidi 10, ili kuweka ilichodai ni
mgawanyo sawa wa rasilimali za nchi. Mapendekezo ya majimbo yaliyotajwa pamoja na mikoa itakayojumuishwa ni Nyanza Magharibi
lenye mikoa ya Kagera, Geita na Shinyanga; Nyanza Mashariki lenye Mwanza, Mara na Simiyu.

Jimbo la Kanda ya Nyanda za Juu litakuwa na mikoa ya Njombe, Mbeya na Ruvuma na la Ziwa Tanganyika lenye mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa. Mengine ni Kati ambalo lina Dodoma, Tabora, Singida na Iringa na la Kaskazini lenye mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro. Chadema ilipendekeza majimbo mengine kuwa ni Pwani ya Kaskazini lenye Tanga, sehemu ya Pwani na sehemu ya Morogoro, Jimbo la Dar es Salaam na la Pwani Kusini lenye Mtwara, Lindi, Mafia, Rufiji na Ulanga.

Katika mapendekezo ya sera hiyo, Zanzibar haikuguswa wala kuzungumzwa kama itaendelea kuwa na mikoa kama ilivyo sasa au italazimika kuwa na majimbo. Gazeti hili lilipotafuta ufafanuzi, Msemaji wa Chama hicho, John Mnyika alisema Chadema inaitambua Zanzibar kuwa nchi kamili inayoweza kujiamulia mambo yake, kutokana na kuwa na Katiba inayojitegemea, uongozi na mifumo ya
kiutawala.

Mnyika ambaye ni mmoja wa wajumbe wa Sekretarieti ya Chama hicho iliyowasilisha maoni mbele ya Tume, alisema chama hicho
kilipendekeza Serikali tatu na kwamba Tanganyika ndiyo itakayokuwa na utawala wa majimbo. Kwa mujibu wa Mnyika, Serikali nyingine zilizopendekezwa ni ya Shirikisho la Muungano na ya Zanzibar.

"Sera yetu ya majimbo na ya kuondoa wakuu wa mikoa itahusu Tanganyika peke yake kwa sababu Zanzibar ni nchi inayoweza kujiamulia mifumo yake ya utawala na ina Katiba inayojitegemea na uongozi uliokamilika," alifafanua Mnyika. Alisema endapo Zanzibar itataka kufuata mfumo huo wa utawala wa majimbo, itakuwa huru kufanya hivyo kulingana na matakwa ya Katiba inayoiongoza ambayo hata hivyo, haitaihusu Tanganyika.

"Hiyo ndiyo sera ya chama chetu sasa, Zanzibar wakitaka kuifuata itakuwa ni juu yao," aliongeza kwa kauli iliyoonesha kama vile chama hicho hakipo Zanzibar. Rais wa miaka 18 Wakati huo huo, NCCR-Mageuzi imependekeza umri wa Rais uanzie miaka 35 huku ikishangaa mapendekezo ya miaka 18 na kudai kuwa itakuwa gharama kubwa kwa Serikali kumtunza rais mstaafu.

Akizungumza jana na waandishi wa habari kuhusu maoni ya chama hicho kwa Tume, Mwenyekiti wa Chama hicho James Mbatia alisema walizingatia Sayansi Jamii na umri wa mtu kuishi. "Tumeangalia mambo mengi ya kisayansi, kijamii, kiuchumi na demokrasia endelevu. Mtu akiwa rais akiwa na miaka 35 baada ya kumaliza uongoziwake atakuwa amefikisha miaka 45 ambao ni kati ya umri wa kuishi wa Mtanzania.

"Nimesoma kwenye gazeti kuwa kuna watu wanataka umri (wa rais) kuwa miaka 18, lakini mtu huyo akimaliza muhula wa uongozi atakuwa amefikisha miaka 28, itakuwa ni gharama kubwa sana kwa Serikali kumhudumia," alisema Mbatia. Chadema ndiyo iliyopendekeza umri wa miaka 18 kwa hoja kuwa kama ameruhusiwa kupiga kura, basi aruhusiwe pia kugombea nafasi yoyote. Umri
wa mtu kupiga kura kisheria nchini ni miaka 18.

"Hata sheria za kazi ya kimataifa umri huu ni kumtumikisha mtoto," aliongeza Mbatia. Kuhusu wabunge na madiwani, alisema NCCR
inapendekeza miaka 21 huku umri wa mtu kushiriki kupiga kura ukiwa ni miaka 18. Maoni mengine Alisema NCCR inapendekeza rais, wabunge na madiwani waongoze kwa mihula isiyozidi miwili ya miaka mitano mfululizo na rais asiruhusiwe kushika nafasi katika ofisi nyingine ikiwamo kuwa mkuu wa chuo au taasisi yoyote ya umma au binafsi na kutofanya biashara ya aina yoyote.

Kuhusu Muungano, Mbatia alisema wanapendekeza Serikali tatu; ya Tanganyika, ya Zanzibar na ya Shirikisho. Alisema muundo wa sasa ulipendelea Zanzibar kuwa Dola tarajiwa, ilidumisha na kutetea utamaduni na maadili ya watu wake, kuwa na Katiba, bendera, wimbo wa taifa na kukosa uhusiano wa kimataifa pekee wakati Tanganyika ilipoteza kila kitu.

Mbatia alisema Katiba inatakiwa kuwa na ibara inayoeleza utaifa wa Mtanzania na sifa za kuwa rais na itambue uraia wa nchi moja. Pia NCCR inataka Katiba mpya iwe na ibara inayohifadhi haki za uhuru wa vyombo vya habari na kuamuru Bunge litunge sheria inayorahisisha masharti na utaratibu wa uanzishaji na uendeshaji wa vyombo vya habari.

Pia inataka Katiba iamuru Bunge litunge sheria inayowajibisha utawala na taasisi zake kutoa habari kwa vyombo vya habari na kwa wananchi kwa jumla na kupiga marufuku taasisi za utawala kuingilia utendaji kazi wa vyombo vya habari na uhuru na haki ya kupata habari kuwa ya msingi kikatiba.

Chanzo. Habari leo.
 
Ni ajabu sana kwa chama cha siasa hasa cha upinzani kuwaza na kupanga mipango kwa ajili ya Zanzibar, ambayo kwa vyovyote vile imeonesha kutokuwa tayari na Muungano. Chadema inaunga muungano wa serikali tatu. Hivyo ndio kusema muundo wa serikali ya Zanzibar italazimika kupangwa na Zanzibar yenyewe. Wao possibility yao kubwa ni ama kuongoza serikali ya Muungano au ya Muungano na ile ya Tanganyika. Ikumbukwe kwamba, kwa mujibu wa katiba ya sasa ya Zanzibar, kama nipo sahihi, swala la Muundo wake, mf uteuzi wa wakuu wa mikoa na mikoa yenyewe linabaki kuwa la Zanzibar. Sioni kwanini tutegemee Chadema waseme katika hilo. Na vyovyote vile iwavyo, kutokuzungumzia Zanzibar sidhani kama ndiko kuitenga 'rasmi'!
 
Back
Top Bottom