Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,468
- 113,583
- Thread starter
- #21
Asante Bantugbro, nitazingatia.Pasco,
Naona bado tatizo lako liko pale pale: unataka kulazimisha kitu ambacho hakiwezekani ile mradi tu message yako iwe sent!, Hata sisi wananchi wa vijijini unaotusemea kuwa hatuelewi haya mambo tayari tumeshatambua kuwa CUF imeshajiunga rasmi na CCM!. Hivi kuna tija gani kutaka CHADEMA lazima ishirikishe CUF kwenye uongozi wa vyama vya upinzani bungeni wakati CUF tayari wako serikalini???:bowl:
Suala la kwanini mhe. Zitto asiwe kiongozi wa upinzani bungeni nalo halina mantiki kwa sababu mhe. Zitto tayari ni makamu wa kiongozi wa upinzani bungeni. Kwanza hivi bunge lililopita wakati mhe. Zitto akishirikiana na Dr.(Ph.D) Slaa kutoa hoja nzito nzito bungeni mbona hakuwa kiongozi wa upinzani bungeni?. Mhe. Mbowe ni kiongozi wa chama na kwa bahati nzuri naye amefanikiwa kuwamo bungeni, ndio maana emeendelea kuwa kiongozi wa wabunge wake kule mjengoni. Lakini hili halimzuii Mhe Zitto ama kamanda SUGU kutoa hoja zao na kuzizimamia kisawasawa kule mjengoni.
Dr.(Ph.D) Slaa alishasema kwamba tusubiri CAHDEMA kama chama watakuja na maelezo ya kina kwa wananchi juu ya nini kilitokea wakati wa uchaguzi na nini cha kufanya huko mbeleni lakini wewe unaita ni political immaturity! . Bila shaka siku ile angeenda pale, wewe ungekuwa ni mtu wa kwanza humu jamvini kumtuhumu kwanini alihudhuria!!!
Kwakuwa umekiri mwenyewe hukufanya research ni vema ufanye research kabla ya kutoa maoni ambayo yanaweza kuleta mgawanyiko usio na msingi haswa kipindi hiki ambacho tunatakiwa kushikamana zaidi.