kokudo
JF-Expert Member
- Oct 26, 2010
- 2,535
- 1,650
Hivi wewe ni Dr W Slaa wa ukweli au jamaa kaamua ku2mia jina la m2?Kama wewe n slaa nahc kuzimia kila kila nikilimnna jna lako najua pamoja 2naweza kukijenga chama che2 chadema mungu akupe afya tere 2015 ni ye2PASCO,
Mwanajamvi nimefurahi sana kujitambulisha kama Political analyst. Ningelifurahi sana kusaidia Taifa lako kama analist kama ungelitusaidia yafuatayo:
i) Utafuti unaonyesha nini duniani kuhusu Leader of the Opposition katika mifumo ya mabunge yaliyoko Duniani. Kwa mtu yeyote anayefanya analysis angelitegemea kuona American Model na WestMinster Model zinaeleza nini. Analysis yako ime base kwa personalities badala ya Model na analysis ya aina hii kwa maoni yangu ni ya hatari sana kwa kuwa inakosa misingi ya kisayansi. Politics is science and should never be reduced to anything less than empirical analysis to be scientific.
ii) Analysis yako imetoa Conclusions kabla ya kujenga plausible major and minor. Scientific and logical conclusion can only be based on a well founded "major and minor". Ili tunaofuatilia tuweze kunufaika na analysis yako ningelitegemea a properly constitued logical arugement inayofuata clasical logical construction ambayo ndio msingi wa analysis yoyote ambayo ni credible.
iii) Analysis yako inaonekana kukosa basic and simple facts. Kwa mfano unapoeleza muundo wa Kambi ya Upinzani tungelitegemea misingi ya hoja yako, analysis ya kwanini tuko hapa tulipo ambapo Chadema wameunda Kambi bila kuwashirikisha CUF and reasons leading to the same, kama kulikuwa na majadiliano yeyote yalikuwapo kwanini yalishindikana, Political Statusquo ya CUF ndani ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inayoongozwa na CCM kama ambavyo Serikali ya Jamhuri ya Muungano inaongozwa pia na CCM hiyo hiyo na Thesis na Antithesis inayotokana na hali hiyo na matokeo yake au conclusions zinazotokana na situation hiyo kutokana na empirical analysis. Vinginevyo analysis unayojenga inaweza kuwa flawed na ikawa msingi mkubwa sana wa political fallacy ambayo ni ya hatari sana katika analysis ya kisayansi, na athari yake ni mbaya kwa kuwa wako wengi ambao watatumia analysis hiyo bila kuifanyia uchambuzi independent wakiamini umetolewa kwa msingi wa kisayansi. Athari za Fallacies katika historia inajulikana sana kwa historical philosophers pamoja na political philosophers.
iv) Maneno "Kuhodhi", "ubinafsi", "umimi", bila kuwa qualified ni manifestation ya "emotion", na kwa kiwango kikubwa ya "ego". Bila vigezo sahihi ya kisayansi maneno hayo ni manifestation kuwa ya kuwa subjective ambayo kimsingi ni kinyume na dhana ya "objective Political analyist unayoijenga. Hivyo ili tunufaike na matumizi ya maneno haya ningelitamani sana kuona qualification ya maneno hayo ili yaweze kulisaidia Taifa letu, kuliko kuyatumbukiza kwa mfumo unaoweza kutafsiriwa kwa sura mbalimbali. Na kwa bahati mbaya hoja hizi zimekwisha kujitokeza mara nyingi kwenye jamvi letu. Kwa vile nia na lengo la jamvi ni kusaida Taifa letu, na Taifa linajengwa na watu wenye uchungu wenye sifa na ujuzi mbalimbali, na hasa kwa kuwa umejitokeza hadharani kama Political Analist ambaye ni "objective" basi nilikuwa nimefurahi sana kupata analysis ambayo inatumia objective criteteria katika hoja zote ulizokuwa unajenga.
Natanguliza shukrani za dhati, na ninategemea kupata objective political analysis ya mapendekezo yako.
Mungu Ibariki Tanzania.