CCM bado ina muda mrefu sana wa kuongoza, ni zaidi ya 2020

Chadema mtaongozaje Dola wakati hamna itifaki?
Hivi nani awe Rais, nani awe waziri na kabineti yenu ita comprise nani na nani? Hapa ninamaana nani ambaye yuko experienced kushika nafasi muhimu za kiuongozi ambazo ni za kisiasa?
Hivi huyu Lema ndo aje kuwa waziri? Au Wenje? Au Mchg. Natse?
Acheni unafiki.
Chadema bado sana.

Najua una post 7 hivyo unafanya haraka kupata u senior member hata kama kwa kutapikia humu.
-Lakini kwa kukusaidia kama experience ndio hii inayotupeleka kwenye umasikini kwa kasi kubwa namna hii Tanzania needs NO experience.
-Mwisho kabisa wewe ni mmoja wapo cdm inataka kukukomboa kutoka mawazo mgando yanayokusababishia kukata tamaa bila hata ya kujaribu kingine for 50 yrs nw
-Nyerere mpka anang'atuka madarakani kulikuwa na viwanda vingi kuliko leo hii
 
Roho ya ubaguzi italiangamiza taifa.Haya niambie idadi ya wabunge wachagga.

Kwa taarifa yako Kilmanjaro CDM ina wabunge watatu tu Rombo,Hai na Moshi mjini.CCM ina wabunge Same Mashariki,Same Magharibi,Mwanga,Siha na Moshi Vijijini ie CCM ina wabunge watano.Mpaka hapo utagundua CCM inakubalika zaidi Mkoa wa Kilimanjaro kuliko CDM.Hizi siasa za kugawa watanzania kwa misingi ya ukabila na udini ni za kupigwa vita na kila mtanzania.

CCM wakitembelea mkoa wa Kilimanjaro hawasemi CDM ni chama cha Wachagga kwakuwa wanajua watazidi kuwaongezea umaarufu.Hadithi kwamba CDM ni chama cha wachagga utazisikia mikoa mingine kama Mwanza,Mbeya,Dar na nk wakifika Kilimanjaro lugha inabadilika.

Dhambi hii hii iliwahi kutumiwa na CCM dhidi ya CUF kwamba ni chama cha kiIslam mabwege wakaingia mkenge lakini utashangaa CCM haikuwa ikisema CUF ni chama cha kiIslam walipokuwa mikoa yenye waIslam wengi ei Tanga,Pwani,Lindi,Pemba na Unguja.Lugha kwamba CUF ni chama cha waIslam ilitumika zaidi mikoa na wilaya zenye waKristo wengi eg Arumeru,Simanjiro,Vunjo na nk.

Inashangaza mpaka leo bado lugha ya kutugawa kwa misingi ya makabila na dini bado inaendelea kutumiwa bahati mbaya wapo wanaokubali kirahisi bila kuhoji uhalali wake.

Ukitazama uongozi wa CDM kuanzia Mwenyekiti hadi naibu katibu mkuu Mchagga ni mmoja tu Freeman Mbowe ?.


[1] Makamu Mwenyekiti Bara ni Mheshimiwa Said Amour Arfi anatoka Mpanda Rukwa

[2] Makamu Mwenyekiti Zanzibar mheshimiwa Said Issa Mohamed anatoka Pemba

[3] Katibu Mkuu Mheshimiwa Dr W P Slaa anatoka Karatu mkoa wa Arusha

[4] Naibu katibu Mkuu Bara Mheshimiwa Zitto Z Kabwe anatoka Kigoma

[5] Naibu Katibu Mkuu Visiwani Mheshimiwa Hamad Mussa Yusuph anatoka Pemba kaskazini

Naomba kujuzwa viongozi watano wa juu CDM lini walibadili makabila yao wakawa wachagga.
Bahati nzuri najulikana sana hapa jamvini msimamo wangu dhidi ya CDM wakikosea nawananga kisawa sawa sifichi hisia zangu lakini hili la ukabila au udini mtanisamee najua hizi ni propaganda za watawala wetu wanachota rasilimali za taifa wanatugawa kwa propaganda nyepesi ukabila na udini !!!!!!!!!!!!!!!!!!!.

Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika.


Serikali nzima watajazana wachaga. Mawaziri watakuwa ni wake zao, wakwe zao, na watoto wao.
 
Chadema kupata viti 200? naona umeshika mikoba ya marehemu Sheikh Yahaya...endelea na utabiri wako

Dah! Hakika wewe mkuu ni kiboko!! Sasa nawewe una tofauti gani na huyo Sheikh Yahya?!? Maana unaupinga utabiri wa huyu mdau; ikimaanisha wewe utabiri wako ni kwamba CHADEMA hakiwezi kupata viti 200!!
 
Chadema mtaongozaje Dola wakati hamna itifaki?
Hivi nani awe Rais, nani awe waziri na kabineti yenu ita comprise nani na nani? Hapa ninamaana nani ambaye yuko experienced kushika nafasi muhimu za kiuongozi ambazo ni za kisiasa?
Hivi huyu Lema ndo aje kuwa waziri? Au Wenje? Au Mchg. Natse?
Acheni unafiki.
Chadema bado sana.

Sina shaka utakuwa na mtindio wa ubongo
 
Kama wameshindwa kuchagu wabunge viti maalum kwa usawa. Wakaamua kugawana na familia zao. Hawa watajimikisha nchi.
 
Yaani mashambulizi ya CCM ni chadema tu na siyo cuf siku hizi, hii kwa sisi analysts inaonyesha cdm inaipa taabu sana ccm na ndicho chama (cdm) kinachoweza kuunda dola. Na hata ukiangalia mashambulizi ya cuf yamehama toka ccm kwenda cdm, yaani tuseme tu wote; tlp, nccr, sijui udp, call them all, wanaishambulia cdm kwa kwenda mbele, maanake nini, cdm are on they right road to 2015, wakiwa makini (cdm) ushindi ni wao. Halafu mtoa mada nani kasema cdm inaunda serikali sasa, ngoja ikifika 2015 cdm washinde urais na wakiwa na wabunge 23 tu ndo useme hayo, sasa hivi unaongea none sense and not from reality
 
Mkuu Mapurende,

Kwanza naomba kujuzwa maana ya Itifaki ulivyoitumia kwenye swali lako ?.Naomba kukujibu swali lako nilivyolielewa mimi,Nadhani Itifaki ulikuwa na maana ya wabunge wa kutosha ie Idadi.

Ni kweli CDM haina wabunge wengi ukilinganisha na wabunge wa CCM.Lakini pia usisahau CDM wana wabunge wa viti maalum [wanawake].Usisahau kuna viti kumi vya magogoni ambavyo Rais wa Tanzania kapewa mamlaka ya kumteua mtanzania yoyote.CDM wapo wasomi kama

[1] Prof Safari huyu ana uwezo wa kuongoza wizara ya sheria na katiba.

[2] Prof Mweisiga Baregu huyu anafaa sana Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu

[3] Zitto Z Kabwe Wizara ya Fedha na Uchumi

[4] Halima Mdee Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na Serekali Mitaa

[5] Tundu Lissu Waziri wa Mambo ya Ndani

[6] Mustapha Akonay Waziri wa mali asili na Utalii

[7] John Mnyika Waziri wa Habari Vijana na Michezo

[8] P ndesamburo Waziri wa Biashara na Viwanda

[9] Willy Lwakatare Waziri wa Ulinzi na jeshi la Kujenga Taifa

[10] Prof Silvester Kulikoyela Waziri wa Elimu

[11] Eng Salvatory Machemuli Waziri wa Ujenzi

[12] Dr Mbasa Gervas Waziri wa Afya

[13] Opulukwa Meshack Waziri wa Kilimo na Mifugo

[14] Said Arf Amour Utawala Bora

[15] Simon Peter Msigwa Waziri wa Nishati na Madini.

[16] Eng.Waberoya wa JF : Waziri wa asiye na wizara maalum

Mpaka hapo Rais atakuwa ametumia nafasi zake tatu kati ya kumi anazoruhusiwa kikatiba !.Uwezo wa kuunda serekali upo sema itategemea busara na hekima za Rais.Baraza la mawaziri linasaidiwa sana na watalam wa wizara kuanzia katibu mkuu,wakurugenzi,makamishna na nk.


Naomba kuwasilisha.


wako wengi mpaka wanakosa wizara!

jamaa aliishachemka kwa sababu u-CCM uko damuni, so kila kitu anataka kiwe ki-CCM tu!
 
Mkuu MAPURENDE,
Umeongea maneno ya ujenzi ni kweli unachosema..

Huwezi kuunda serikali wakati una wabunge 23 tu.

Baraza la mawaziri litakuwaje, na huko bungeni mnatapitishaje bajeti zenu wakati mpo wabunge 23 tu.

Na sijui serikali yenu ingekuwa na ukubwa gani..

Naomba mwana Chadema ajibu hii

kumbe wajinga wengi? Na wewe kumbe humo.
 
..kama Dr.Slaa angeshinda uraisi basi angelazimika kuchagua Waziri Mkuu toka chama chenye wabunge wengi ambacho kingekuwa CCM.

..kwa uelewa wangu baraza la mawaziri lingeweza kuwa na mawaziri toka CDM,CCM, vyama vyenye wabunge, pamoja na nje ya bunge.

..bunge letu litakuwa efficient zaidi kama hakutakuwa na chama kunacho-dominate vyama vingine ndani ya bunge. yaani there should be a slim majority in the parliament.
 
Mkuu MAPURENDE,
Umeongea maneno ya ujenzi ni kweli unachosema..

Huwezi kuunda serikali wakati una wabunge 23 tu.

Baraza la mawaziri litakuwaje, na huko bungeni mnatapitishaje bajeti zenu wakati mpo wabunge 23 tu.

Na sijui serikali yenu ingekuwa na ukubwa gani..

Naomba mwana Chadema ajibu hii

TATIZO
Elimu: Madrasa
Kazi: Mkwezi
CCM inawapenda watu wa namna hii. Akinusurika kupata elimu ya juu zaidi ni shule ya kata isiyo na walimu, madawati, vitabu, maabara n.k. Kusudi: Waendelee kuwa mbux3 ili CCM watawale milele kama ambavyo wamekuwa wakijitapa. Nchi hii tunayo mizoga lakini haijitambui kama imekufa inanuka. Huu ni msiba wa taifa.


 
wana jf,tunahitaji kubadilika kwa kiasi kikubwa sana...
kwanini unaibuka na matusi dhidi ya mtu anaetoa changamoto?
chadema badilikeni vinginevyo wananchi hawatajua tofauti kati ya kichaa na timamu, naona watu wa jf-chadema kila panapotokea mada ambayo hawaipendi wanarusha matusi,huku ni kufilisika kimawazo.kama cdm imekomaa basi wanachama wake wangekuwa wavumilivu,au mnataka kuabudiwa?mmekuwa miungu?cdm ni chama cha siasa kama cck,updp,narea,nra nk.kama cdm imekomaa mbona haikushinda uchaguzi mkuu wa mwaka jana?watanzania waelewa na wanapima kauli na matendo yenu,hawadanganyiki.

We unaumiza kichwa na hawa jamaa, mi nimegundua ni watoto tupu. Usiumize kichwa.
 
TATIZO
Elimu: Madrasa
Kazi: Mkwezi
CCM inawapenda watu wa namna hii. Akinusurika kupata elimu ya juu zaidi ni shule ya kata isiyo na walimu, madawati, vitabu, maabara n.k. Kusudi: Waendelee kuwa mbux3 ili CCM watawale milele kama ambavyo wamekuwa wakijitapa. Nchi hii tunayo mizoga lakini haijitambui kama imekufa inanuka. Huu ni msiba wa taifa.



Ha! Ha! Ha! Ha! Nimecheka sana yote uliosema ni kweli...
 
Sikupenda kuchangia, ila nadhani kuna kitu ambacho inabidi tuwekane sawa. Unapozungumzia suala la uongozi wa nchi unazungumzia kitu ambacho ni very sensitive. mimi si mshabiki wa siasa za kutukanana ila ni mfuasi wa constructive and scientific politics. Mtoa mada, amefanya analysis na kugundua kuwa Chadema ina wabunge 23! hivyo si busara kupewa nchi waiongoze KWA SASA, hii inamaanisha wale watu 23 ndiyo true picture ya serikali ya Chadema itakavyokuwa. Ninakuhakikishia Chadema wanaweza kupewa kuongoza nchi kwa nafasi ya uraisi(sijui ni nani kati ya unaowajua, Dr. Slaa? Marando? Mnyika? Zito Kabwe? Mdee?...). Ila yeyote kati ya hao atakayepewa huo uraisi hatoweza kuongoza nchi kutokana na sababu zifuatazo. Kwanza CCM inaonyesha katika kipindi cha miaka 10 ijayo(endapo chadema itachanga vizuri karata zake) bado CCM itakuwa na uwiano mzuri wa wabunge kuliko chama chochote cha siasa hapa nchini, na hii inamaanisha kama serikali ya chadema itakuwa na wabunge theluthi moja, ni lazima theluthi mbili ya mawaziri watoke CCM(Soma katiba) na kwa hili serikali itakuwa bado ni ya CCM! Spika wa Bunge penda ukatae lazima atakuwa wa CCM kutokana na wingi wa kura za wabunge wa CCM. Wakuu wa itifaki waliopo sasa hivi ambao ni experienced ni wahafidhina wa CCM. Jeshi, kinadharia tunasema halina chama, ila usijidanganye sana mjomba(haya mambo huyajui). Unapomzungumzia hiyo serikali ya chadema, kwangu bado naiona hiyo serikali ya chadema tunayoitaka itupeleke katika tanganyika tunayoitaka bado haijawa tayari. Ukirudi kwenye mifano sahihi, Chadema hakina mizizi sahihi ya kuweza kusimama kama chama, na hata hao wabunge 23, angalia vizuri na ndani yao utakuta karibu nusu ni mamluki wa CCM, ukianza na Dr. Slaa mwenyewe(fuatilia wapi alipotoka na kwa nini yupo pale?), Shibuda? Marando? na wengine kibao si wa kuaminika na hata wanapokaa kwenye NEC zao fuatilia utaambiwa matatizo kibao. Huyo unayemwita Mr. Obama, fuatilia kwa makini na utaona ni kwa nini alipewa nchi! Huyu jamaa hakupewa nchi kutokana na kuwa hana experience wala kutokana na kuwa alipewa kwa kuwa kwake mwafrica ili apate popular sympath na kuwaonyesha jamaa si wabaguzi, hilo silo! Alipewa nchi kwa kuwa aliandaliwa miaka 33 pamoja na wenzie 11 ambao wote walifuzu katika advanced trainings za kijasusi na system za USA, alipewa uraisi kwa ajili ya kuimarisha uhusiano wa USA na Israel, yeye obama akiwa anadamu ya Jews (soma ujue nini faida ya israel kwa Taifa la Marekani), na zaidi hakuachiwa nchi, ila alipewa Vice President mwenye experience ya hali ya juu. Kama CDM wapo desperate kuitaka nchi, sawa tutawasaport lakini watupe tentackes kiutawala, kimfumo, na strategies zisizo na longolongo. Wangekuwa stable, wasinge enda ikulu kunywa soda, kuutangazia umma yamekwisha, na kesho yake kukurupuka na kudai wameuzwa! Tuwaamini vipi? Tusichangie kishabiki, tufanye critica thinking kidogo.
nimekusoma mkuu
inamaana jeshi letu lina chama kwa hiyo hawataruhusu chama kutoka nje yao kitawale sio? basi kama ndio hivyo tuna kazi ya kufanya ili tuwe na fairness kwenye siasa.
kuna thread moja hapa nimechangia kwamba uwezekana huo(wa chadema kushinda bila kupata wabunge wengi kwa sababu idadi ya wabunge sio prerequisite ya kuupata uraisi) upo na nikasema watalazimika kuamend katiba ili kupata mawaziri nje ya bunge ili kuleta ufanisi.
Pia hakuna sehemu kwenye katiba inayosema kwamba raisi atalazimika kuchagua mawaziri kwa proportions kama ingelikuwa hivyo basi tungekuwa na mawaziri kadhaa wa upinzani ila katiba inasema article 55(1-5) raisi kwa kushauriana na waziri mkuu ilawateua mawaziri/naibu waziri na lazima wawewabunge.
Pia kwa kutumia katiba hii kuna FURSA ya raisi kuteua wabunge 10 ingesaidia kupata mawaziri kutoka nje ya bunge na kuungana na vyama vingine kuunda serikali.
Sijakuelewa mizizi unayoizungumzia ni ipi? kwa sababu tulikuwa na mfumo wa chama kimoja kila mtu mzima alilazimika kuwa kwenye chama hicho sasa kwa mzee kama Dr Slaa ulitegemea asiwe mwanachama????
Kuhusu Obama ni asignment ambayo nitaifanyia kazi kuprove uliyoyasema ila ninachojua ni kwamba alipewa uraisi kutokana na competence/abilities zake.
 
..kama Dr.Slaa angeshinda uraisi basi angelazimika kuchagua Waziri Mkuu toka chama chenye wabunge wengi ambacho kingekuwa CCM.

..kwa uelewa wangu baraza la mawaziri lingeweza kuwa na mawaziri toka CDM,CCM, vyama vyenye wabunge, pamoja na nje ya bunge.

..bunge letu litakuwa efficient zaidi kama hakutakuwa na chama kunacho-dominate vyama vingine ndani ya bunge. yaani there should be a slim majority in the parliament.

CDM wanajua hili?
 
Bado hakijatanuka, hakijajenga misingi imara, chama cha siasa ni Kama kiumbe hai, kinazaliwa, lkn bado kichanga hakina mifupa, bado kina ukaka, udada na ushemeji, maneno na hoja za ni sisi tumeanzisha chama zingali na MOTO, apite mboe,zitto, na current MPs, Hapo tutakuwa na CHADEMA, but hii yenye waanzilishi tabu tupu, bado inapayback, naipenda lkn nitakuwa nayo 2045.
 
Bado hakijatanuka, hakijajenga misingi imara, chama cha siasa ni Kama kiumbe hai, kinazaliwa, lkn bado kichanga hakina mifupa, bado kina ukaka, udada na ushemeji, maneno na hoja za ni sisi tumeanzisha chama zingali na MOTO, apite mboe,zitto, na current MPs, Hapo tutakuwa na CHADEMA, but hii yenye waanzilishi tabu tupu, bado inapayback, naipenda lkn nitakuwa nayo 2045.
Hiyo 2045 utakuwa raia wa nchi gani?
 
Karibu J.F. ila umechelewa sana na unafiki wako. Umechemsha kenge kasoro mkia. a.k.a. magamba kazini.
 
Bado hakijatanuka, hakijajenga misingi imara, chama cha siasa ni Kama kiumbe hai, kinazaliwa, lkn bado kichanga hakina mifupa, bado kina ukaka, udada na ushemeji, maneno na hoja za ni sisi tumeanzisha chama zingali na MOTO, apite mboe,zitto, na current MPs, Hapo tutakuwa na CHADEMA, but hii yenye waanzilishi tabu tupu, bado inapayback, naipenda lkn nitakuwa nayo 2045.
Mtazamo wako una mantiki , lakini huoni kama njia zinazotumiwa na CHADEMA kuwahadaa Watnzania zinaweza kuwafnya Watanzania kukiamini na kukipa ridhaa ya kuongoza nchni ,jambo ambalo linaweza kusababisha yakatokea yale ya LIBYA ,TUNISIA na kwingineko? Watanzania wangekuwa wanaangalia mbali kama wewe wangekuwa wanafnya maamuzi sahihi badala ya kuwa bendera fuata upepo.
 
Back
Top Bottom