CCM bado ina muda mrefu sana wa kuongoza, ni zaidi ya 2020

Mgombea Mwenza Wa Chadema Mwaka Jana Alikuwa Na Elimu Ya STD 7, Mwizi wa Magari Tutampa Waziri Wa Mambo Ya Ndani, Form Four Failure Sugu Waziri Wa Habari na Michezo, Form Four Vicent Nyerere Wizara Ya Elimu...Form Four Msigwa Wizara Ya Tamisemi,..Shibuda Tutamfikiria...SIPATI PICHA BARAZA LA MAWAZIRI KWA MTINDO HUU, MANAKE WABUNGE WASOMI WA KUHESABU

Yaani yule mbunge mmoja Tundu Lissu ni sawa na wabunge 200 wa magamba bado hapo sijataja wabunge wengine!
 
Kujiunga jana sioni ka ni tatizo,..Hz post nne ni nyingi sana au chache!? We ulitaka aanze kutoa post zake lini baada ya kujiunga!?
mko pamoja la sivyo una tatizo.. jibu hoja acha majungu.. tetea post yake au ipinge...
 
Mkuu kwavile umezoea mfumo wa maslahi ya chama kwanza, ndio maana ni rahisi kwako kuamini haya uliyaandika.

Pia mfumo wa kiserikali ambao CHADEMA daima kinapendekeza (wa kutotumia wabunge katika nafasi za serikali yaani katika executive organs) ilo la kuwa na wabunge 23 wala si hoja ya msingi. Hapa pia kwavile umezoea kutokana na mfumo wa serikali za CCM za kuwa na wabunge ambao ni mawaziri, makatibu wakuu wa wizara ambao ni makada wa chama, wakurugenzi makada, wanachama wa bodi za mashirika ya umma, makada etc.

Hivyo wala sikushangai wewe kuwaza hivyo.

Wakati wa uchaguzi mkuu, kwenye kampeni za urais na wabunge nilimsikia Dr. Slaa alisema akichukuwa nchi serikali itakuwa na wazari 15 na manaibu 15..

Wamekwenda bungeni wameunda Baraza la Mawaziri kivuli 24..

Chadema bado sana kuunda serikali
 
mko pamoja la sivyo una tatizo.. jibu hoja acha majungu.. tetea post yake au ipinge...

Nilikuwa namuweka sawa jamaa yako anayemponda aliyeleta thread kisa kajiunga jana...
Kuhusu issue ya experience sidhani ka nitatizo kubwa kuna watu ka Zitto, Mnyika, Lissu wanaweza kuongoza wizara ambao ni wachache mno na sina wasiwasi nao kulinganisha na hao wengine?
Na G'ment sio tu baraza la mawaziri kuna wakuu wa mikoa, wilaya na mabarozi., Je hao watu wapo?!!
 
Chadema mtaongozaje Dola wakati hamna itifaki?
Hivi nani awe Rais, nani awe waziri na kabineti yenu ita comprise nani na nani? Hapa ninamaana nani ambaye yuko experienced kushika nafasi muhimu za kiuongozi ambazo ni za kisiasa?
Hivi huyu Lema ndo aje kuwa waziri? Au Wenje? Au Mchg. Natse?
Acheni unafiki.
Chadema bado sana.

Tatizo lako unakuwa kama wale wanocheza mpira kwa kuangalia majina. Ukitajiwa akina Sitta, Mwinyi, Makinda, Lowasa, Rostam, ndio unadhani wanajua kuongoza. Hivi unajua kuwa nyerere akichukua utawala alikuwa na umri gani? Hivi unajua kuwa kijana mdogo wa Madagascar tena DJ alivyochukua nchi imetulia? Kabila alikuwa na uzoefu gani? Sembuse CHADEMA wana vijana waliotulia na wenye uwezo wa kuona mbali wengi kama akina Mnyika, Zitto na wengineo wengi. Nyie ndio mnataka mtawaliwe na wala rushwa wakubwa mpaka nchi itakapobaki mifupa mitupu ndio utazinduka.
 
Chadema mtaongozaje Dola wakati hamna itifaki?
Hivi nani awe Rais, nani awe waziri na kabineti yenu ita comprise nani na nani? Hapa ninamaana nani ambaye yuko experienced kushika nafasi muhimu za kiuongozi ambazo ni za kisiasa?
Hivi huyu Lema ndo aje kuwa waziri? Au Wenje? Au Mchg. Natse?
Acheni unafiki.
Chadema bado sana.
Hakika Chadema inawanyima sana usingizi.Vyama vingine hujaviona umeona CHADEMA tu?Ni lini CHADEMA walipewa jukumu la kuongoza nchi na wakashindwa?Au unaleta hoja za kufikirika hapa.Tena ni bora tuwe na viongozi kama hao uliowazungumzia wa CHADEMA kuliko kua na viongozi WEZI,MAFISA NA WASIO NA UCHUNGU NA NCHI.
 
Watawala wa CCM huwezi kuwalinganisha na viongozi wa CHADEMA...Kuna tofauti kubwa sana kati makamanda walioko CHADEMA na wala Rushwa wa Chama cha Mapinduzi...kwenye baadhi ya sehemu ambapo CHADEMA ilishinda uchaguzi kuna mabadiliko makubwa ya kimaendeleo tofauti na sehemu ambazo zinaongozwa na chama kingine(majimbo) kwa mfano Moshi Mjini..Kigoma Kaskazini...Hai...Ubungo..Kawe..etc Binafsi ninaamini CHADEMA wako na uwezo wa kuendesha serikali na ikawa na mafanikio makubwa!
 
Chadema never. Wahuni hao. Kila jambo sharishari. Wabunge wao watano wavita ganja. Wana laana hao
 
Chadema mtaongozaje Dola wakati hamna itifaki?
Hivi nani awe Rais, nani awe waziri na kabineti yenu ita comprise nani na nani? Hapa ninamaana nani ambaye yuko experienced kushika nafasi muhimu za kiuongozi ambazo ni za kisiasa?
Hivi huyu Lema ndo aje kuwa waziri? Au Wenje? Au Mchg. Natse?
Acheni unafiki.
Chadema bado sana.

MAPURENDE, can you sincerely tell me what'd the current ruling party boast to had attained in Tz? Can't you see that the current ruling party has completely failed to steer our country towards better life? Gutter politics has brought our country to a point where people (majority) can't even afford two mwal a day.

It is clear now that you guys do lose much sleep due to apprehension of CDM! Na bado.

wana jf,tunahitaji kubadilika kwa kiasi kikubwa sana...
kwanini unaibuka na matusi dhidi ya mtu anaetoa changamoto?
chadema badilikeni vinginevyo wananchi hawatajua tofauti kati ya kichaa na timamu, naona watu wa jf-chadema kila panapotokea mada ambayo hawaipendi wanarusha matusi,huku ni kufilisika kimawazo.kama cdm imekomaa basi wanachama wake wangekuwa wavumilivu,au mnataka kuabudiwa?mmekuwa miungu?cdm ni chama cha siasa kama cck,updp,narea,nra nk.kama cdm imekomaa mbona haikushinda uchaguzi mkuu wa mwaka jana?watanzania waelewa na wanapima kauli na matendo yenu,hawadanganyiki.
 
CCM ni chaka lililojaa simple minded person. Wamekuwa na kazi ya kujadili watu na matukio basi. Kujadili huyu ana nini yule hana nini ni umbea tu hauna tija. Kwa mbumbumbu wengi wanadhani Serikali ni utitiri wa wabunge, ama kuwa na wanachama wengi n.k. Baraza la mawaziri linaweza kuwa na watu 10 tu wapiganaji shupavu wakatenda kuliko mizigo aliyonayo JK. Waziri ni mtu wa sera na sio mtendaji mkuu wa wizara. Rejea Jairo scandal. Watendaji wa wizara ni watanzania wengine ambao uhusiano wao na vyama vya siasa si jambo la msingi ktk uwepo wao kazini. Point hii CCM hawaielewi kabisa. Unaweza kuunda wizara chache sana zikafanya kazi zake kwa ufanisi mkubwa mfano. 1. Wizara ya Fedha, Uchumi na Mipango - ishughulikie suala zima la fedha, kuweka mifumo imara ya kiuchumi na mipango ya maendeleo (mambo yote ya uwekezaji, uwezeshaji n.k yashuhulikiwe na wizara hiyo). 2. Wizara ya Mambo ya nchi za nje. 3. Wizara ya mambo ya ndani 4. Wizara ya ujenzi 5. Wizara ya ardhi, maji, kilimo, mifugo na uvuvi 6. Maliasili, Nishati, Madini na utalii 7. Wizara ya Elimu 8. Tawala za mikoa na serikali za mitaa (Mazingira yapo mikoani wajameni, huku ndipo tunapoishi, yaani hakuna sehemu ya tanzania isiyohusiana na mkoa fulani) 9. Wizara ya ulinzi na JKT 10. Wizara ya Afya.
Wizara nyingine zote alizonazo JK function zake zimo ndani ya wizara tajwa hapo juu. Huu ni mtazamo wangu tu.
 
wana jf,tunahitaji kubadilika kwa kiasi kikubwa sana...
kwanini unaibuka na matusi dhidi ya mtu anaetoa changamoto?
chadema badilikeni vinginevyo wananchi hawatajua tofauti kati ya kichaa na timamu, naona watu wa jf-chadema kila panapotokea mada ambayo hawaipendi wanarusha matusi,huku ni kufilisika kimawazo.kama cdm imekomaa basi wanachama wake wangekuwa wavumilivu,au mnataka kuabudiwa?mmekuwa miungu?cdm ni chama cha siasa kama cck,updp,narea,nra nk.kama cdm imekomaa mbona haikushinda uchaguzi mkuu wa mwaka jana?watanzania waelewa na wanapima kauli na matendo yenu,hawadanganyiki.
 
Sisi CCM kwa kuwa tunawatu wa kutosha kuunda Serikali tangia 1961 yafuatayo ndo tumeyafanya:- (a) Tumesaini mikataba bora kwa wananchi na inawanufaisha(the best practice) (b) Uchumi wetu uko imara siku zote(c) Inflation rate iko chini (d) balance of payments tangia Nyerere hadi Kikwete iko favourable ( Export iko kubwa kuliko imports) (e) Shule zetu ziko bora sana- walimu wa kutosha, vitendea kazi vipo, hatutumii madawati bali meza special (d) Barabara zote za mijini Lami tupu (f) Hospitali ndo usiseme: madawa kedelede, madaktari bingwa wapo tu, vitendea kazi kama Appolo (g) flyovers(h) Rushwa kwetu ni historia (i) Tumeweza, tumedhubutu na tunasonga mbele>>>>>!!!!???
 
Mkuu, Chadema wameishasema na tumeona jinsi walivyounda serikali kivuli, walisema wazi hakuna chama makini cha upinzani zaidi ya Chadema..

Na wakajitangaza rasmi kuwa Chadema ni kambi rasmi ya upinzani huku wakiviacha njia panda vyama kama NCCR Mageuzi, TLP, CUF, UDP..

Sasa kama wameshindwa kuwakaribisha wenzao kwenye kwenye kambi ya upinzani bungeni wakichukuwa na nchi ndio wataweza?

Kuhusu kubadili katiba hawawezi sababu katiba si mali ya Chadema ni mali ya watanzania

Leo ndio nimeamini kuwa we ni mvivu wa kufikiri na mkurupukaji.
 
Mgombea Mwenza Wa Chadema Mwaka Jana Alikuwa Na Elimu Ya STD 7, Mwizi wa Magari Tutampa Waziri Wa Mambo Ya Ndani, Form Four Failure Sugu Waziri Wa Habari na Michezo, Form Four Vicent Nyerere Wizara Ya Elimu...Form Four Msigwa Wizara Ya Tamisemi,..Shibuda Tutamfikiria...SIPATI PICHA BARAZA LA MAWAZIRI KWA MTINDO HUU, MANAKE WABUNGE WASOMI WA KUHESABU
Umewasahau Prof Kahigi,Prof Baregu,Prof Safari,Dkt Mabere Marando,Mh Tundu Liss,Mh Mdee etc.Kama unazungumzia elimu mbona humsemi std 7 Lukuvi tena amekabidhiwa na Wizara kabisa.Na vp kuhusu elimu ya Majimarefu?
 
Sisi CCM kwa kuwa tunawatu wa kutosha kuunda Serikali tangia 1961 yafuatayo ndo tumeyafanya:- (a) Tumesaini mikataba bora kwa wananchi na inawanufaisha(the best practice) (b) Uchumi wetu uko imara siku zote(c) Inflation rate iko chini (d) balance of payments tangia Nyerere hadi Kikwete iko favourable ( Export iko kubwa kuliko imports) (e) Shule zetu ziko bora sana- walimu wa kutosha, vitendea kazi vipo, hatutumii madawati bali meza special (d) Barabara zote za mijini Lami tupu (f) Hospitali ndo usiseme: madawa kedelede, madaktari bingwa wapo tu, vitendea kazi kama Appolo (g) flyovers(h) Rushwa kwetu ni historia (i) Tumeweza, tumedhubutu na tunasonga mbele>>>>>!!!!???
Mkuu nimependa hicho kinyume.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom