Wapinzani wameshindwa kabla ya Uchaguzi. Katiba ni mbuzi wa kafara

Billal Saadat

Senior Member
Nov 30, 2022
169
356
USHINDI WA RAIS SAMIA 2025 NI ASILIMIA 95.

Tanzania tumezoea Siasa za Ushawishi kufanya siasa bila ya ugumu wa kuhasimia au kugawana hizi ndiyo siasa tunazozitaka. Mawazo tofauti si chuki si uadui ni uwezo wa kuzidiwa ushawishi tu.

Mfumo wa vyama vingi ulipokuja Tanzania Mwaka 1992, ulikuja na mabadiliko mengi na kuzaliwa kwa vyama mbadala na CCM ndiyo maana uchaguzi wa mwaka 1995 ulimfanya Mrema kufahamika na uchaguzi ulipokwisha alisahaulika na maisha yanaendelea hadi leo.

Wabongo wana matatizo ya kupenda vitu vipya upepo ukikata wanarudi walipotoka!

Mrema alivuma kweli kweli wakati ni kama ukuta ukipita umepita naye Mrema akapita na Wakati. Mungu amrehemu lyatonga Mrema amerudi malaloni akiwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Tanzania.

Yuko wapi Prof Ibrahimu Haruna Lipumba na Mzee John Mapalala pamoja na Hayati Maalim Seif Sharif Hamad, Magdalena Sakaya bila kumsahau Ismail Jussa? kipindi chao CUF ilipata umaarufu mkubwa lakini baadaye walizama kwenye mgogoro mzito baada ya Prof Ibrahim Lipumba kuandika barua ya kujiuzulu wadhifa wake Katikati ya uchaguzi mkuu! Miezi 7 mbele Lipumba alirudi na fujo za kuutaka Uenyekiti na chama kikafaa rasmi leo CUF ni jina tu.

Wako wapi CHADEMA ya Dkt. Walid Kaburu? Chacha Wangwe? Zitto Kabwe, David Kafulila na Tundu Lissu, Mdee, Bulaya na Dkt. Wilbroad Peter Slaa..? Chama ambacho leo ni tabu kutoa hata ripoti ya michango ya hiari inayochangwa na watumishi? Ni Chadema hii hii ambayo ilimpokea Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa na kundi la wanachama kutoka CCM..?

Ukiwatizama wanasiasa wa Upinzani ni nani mwenye ubavu wa kwenda na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye uchaguzi Mkuu 2025? Kiukweli wapo hoi bin taabani na jibu ni hakuna may be bado hajazaliwa.

Unaweza vipi kumshinda Rais Samia bila ya umoja wa Kisiasa ambao unaweza kufanikiwa kupata hata asilimia 40 ya kura zote?
Kila chama kinatafuta nafasi kujiimarisha kwa kudhoofisha chama kingine cha Upinzani CDM wapo busy kuidunisha ACT and Viceversa. Watagawana mbao na Dkt. Samia atapita kwa kasi ya 5G.

Wameshachelewa kuamua kusimama kwa pamoja wakikubaliana hata kesho kutakuwa wa ukiukwaji wa makusudi wa makubaliano ya ushirikiano hata wakiingia makubaliano ya kusimamisha mgombea mmoja na kuachiana majimbo ya uchaguzi kuna chama kitavuruga utaratibu.

Mtindo wa kufanya mambo kiholela kwa vyama vya upinzani ni mtaji kwa CCM kushinda Uchaguzi.
Vyama vya upinzani hadi leo wameshindwa kukubaliana kanuni za uendeshaji wa umoja wao wa kisiasa kamwe hawawezi kusimamia kanuni zao wenyewe.

Migogoro ndani ya Chama na ile baina ya chama na chama pamoja na wanaharakati wanao waunga mkono rejea sababu za Chadema kutokushiriki mkutano wa vyama vya siasa. Hata wanaharakati wenyewe wamejitenga labda wamelaaniwa huwezi kumsema Rais Samia vibaya ukabaki salama.

Kuna tetesi za kisayansi au confidential information kuwa tayari vya upinzani wamejipanga kuwapa nafasi wanachama kutoka CCM tena watawapatia nafasi kubwa kuliko viongozi wa upinzani. Wapinzani wanawasubiria wanachama wa CCM wasio endana na kasi ya Rais Samia watakaotemwa ili kuwapokea na kuwapa nafasi.

Maandalizi ya kuunda timu za kampeni itakayoweza kugharamia chaguzi na logistics zao kuanzia ngazi ya kijiji hadi Urais vyama vya upinzani huu ni mlima kwao vyama vingi vipo hoi vinategemea ruzuku, Morali ya Wananchi kuchangia vyama vya upinzania imeshuka kwa sababu hawana hulka ya kuweka wazi mapato na matumizi. Sijaongelea Join the Chain.

Vyama vya Upinzani wameshagawana upande Chadema haijali Zanzibar na ACT haijali Bara. Tayari kuna watu wameshapangwa nani agombe wapi wengi itakuwa ni potelea Pwete muhimu wapate viti vichache vya uwakilishi bungeni.

Kukosekana kwa umoja kwa wanachama na wanaharakati kila mmoja anajiona ni bora zaidi ya mwingine ngumu sana mwanachama wa CUF kukaa meza moja na mwanachadema.

Vyama vingi vya upinzani hapa Tanzania vimejengwa kwa njia za hila, ubinafsi na ulaghai ni ngumu kuitoa CCM madarakani kwa njia hizi.

Mwaka 2025 Rais Samia atashinda kwa kishindo hakuna mgombea wa kupima naye ubavu ndani na nje katika uchaguzi mkuu ujao. Ameitenda kazi kwa uhakika! Viwango tulivyofika chini yake vilikuwa ndoto miaka mingi.

420Cousin
Madeira - Portugal
#MamaYukoKazini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom