KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,590
- 4,603
Ninakifahamu vizuri Chama Cha Mapinduzi na kila ninaposikia kinaelezwa tofauti na ninavyokifahamu hususani na wapinzani nawaza mengi sana lakini mwishowe nahitimisha mawazo yangu kwa kusema ni suala la muda kabla hawajaufahamu ukweli.
Ninatambua U CCM sio falsafa ya kila mtu na waliobahatika kuiishi wanaifurahia na wanaipenda sana. Na hapa takwimu za idadi ya wanachama wa jumuiya ya CCM na jumuiya za vyama vingine au wanachama wa CCM na WA vyama vingine zinatoa majibu ya Moja Kwa Moja Kwa Nini U CCM ni hitaji bora la nchi.
Nimemsikia Tundu Lissu akihimiza kukubali kukosolewa( hapa naamini anafikisha ujumbe Kwa Wana CHADEMA) ili kuepukana na U CCM. Bila shaka Kwa mtazamo wa Tundu Lissu U CCM haukubali kukosolewa. Huu ni upotoshaji mkubwa.
Msingi mkubwa wa CCM ni vikao na maamuzi yote yanafikiwa na vikao Ile ni vikao vya Kamati kuu, halmashauri kuu na mikutano mikuu Kwa ngazi zote na ndani ya vikao kuna kukubaliana na kutokukubaliana na mwishowe maamuzi kufikiwa. Hakuna hata uamuzi mmoja uliowahi kufikiwa na CCM bila kikao na hapa hoja ya Lissu ya kuhusanisha CCM na kutokukubali kukosolewa inakosa mashiko.
Ni CCM ndio inaendesha Serikali na maamuzi ya Serikali ni maamuzi ya wengi maana yake Kuna kukoselewa na kukosoa mambo mbalimbali lakini mwisho maamuzi ya wengi ndio yanafikiwa na yanaamriwa.
Kila kitu kinachofanywa na CCM ni Kwa kuzingatia sheria na kukosoa na kukosolewa pia. Ukosoaji unaohimizwa na CCM ni ule ukosoaji wa kuzingatia sheria, naamini hili hata Lissu analifahamu vizuri.
Lissu anachofanya ni danganya toto, kwamba CHADEMA kukosoana ni "pro max" kitu ambacho sio kweli. Inawezekana akawa amesahau lakini sio mbali sana. Uchaguzi mkuu wa CHADEMA uliomfanya kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hiko ,aliyetaka kugombea uenyekiti Frederick Sumaye aliambiwa sumu haionjwi kwa kulamba alipomkosoa Mwenyekiti Kwa kutaka kugombea uenyekiti.