Bunge letu ni Bunge la ovyo? Bunge linafanya Uhuni? Wabunge Wetu ni Wahuni? Tumshauri Spika naye aanze kuita Watu kwenye Kamati, au waachwe tu?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,499
113,608
Wanabodi,

Kama kawa kila nipatapo fursa, huja na makala zangu hizi za kwa maslahi ya taifa ambazo ziko kwa mfumo wa maswali, halafu majibu utayatoa mwenyewe wewe msomaji.

Maswali ya leo ni Bunge Letu ni Bunge la Hovyo? Bunge Letu Linafanya Uhuni? Wabunge Wetu ni Wahuni? Tumshauri Spika Aanze Kuita Watu Kwenye Kamati, au Waachwe Tuu?.

Maswali haya ni kufuatia mkutano wa jana na waandishi wa habari Bandari na DP World: Dkt. Slaa asema ni uuzaji wa Nchi. Adai Serikali iliyopo ina uhalali wa wasiwasi

Balozi Dkt. Willibrod Slaa anazungumza na Wanahabari katika Hoteli ya Regency Jijini Dar es Salaam, leo Juni 13 2023 kuhusu hati ya makubaliano yaliyoingiwa kati ya Tanzania na DP World.
.
Dkt: Slaa: Mbona hawalielezi hata bungeni hilo, kumbe kuna mambo mengi hata bunge limefichwa na bunge letu jinsi lilivyo la hovyo, naomba radhi sana na waniite kwa hilo, kilichofanyika juzi ni uhuni.

Baada ya kuzisoma hizo hoja, kabla sijaandika, nikatafuta kwanza clips ili kujiridhisha ni kweli maneno haya ameyamtaka kweli?, maana fani ya uandishi wa habari siku hizi imevamiwa, kuna waandishi wa habari wa kila aina kuanzia comedians, wasanii, na waandishi wengine wa hovyo sana, usipokuwa makini, sometimes waandishi hawa wa habari wa hovyo hovyo, hawachelewi kukulisha maneno!, hivyo nikamsikiliza mwanzo mwisho na kujirishisha kuwa ni kweli maneno hayo ameyasema, na sio tuu ameyasema, bali pia ameyaandika kwanza kisha akaja kutusomea sisi waandishi wa habari.



Kabla sijaendelea, naomba kuwakuwakumbusha wasomaji wangu, tujifunze kutofautisha definite statements na maswali. Hakuna statement kwenye bandiko hili, ni bandiko la swali! Natoa angalizo hili kwasababu mimi mwenzenu nimeisha wahi kuitwa all the way from Dar to Dodoma, kufika kule nikaulizwa kwanini umetoa hii statement? Nikajibu hiyo sio statement ni swali! Hivyo hapa nasisitiza hili ni bandiko la swali sio bandiko la statement!

Dr. Slaa ameliita Bunge Letu ni Bunge la Hovyo, na kilichofanyika kuridhia IGA ni uhuni? Ndio maana nauliza waungwana humu, hiki alichokisema Dr. Slaa kinaukweli kuhusu Bunge letu ni Bunge la hovyo?. Kilichofanywa na Bunge letu kuridhia IGA ya DPW ni uhuni?. Wanaofanya uhuni ni wahuni, jee Wabunge wetu ni Wahuni?.

Bunge letu Tukufu haliwezi kudhalilishwa hivi tukanyama! Je, tumshauri Madam Spika aanze ule utaratibu kama wa mtangulizi wake kuita watu kwenye Kamati, watu wowote watakao toa kauli za kulidhalilisha Bunge, au waachwe tuu kwasababu wanatoa maoni yao kwa mujibu wa ibara ya 18 ya katiba kuhusu uhuru wa kutoa maoni?

Nashauri Daktari aitwe mbele ya Kamati!. Mimi nilipouliza tu, hili swali Je, Bunge letu tukufu linajipendekeza kwa Serikali? niliitwa Bungeni kuhojiwa na kamati!, sasa leo Bunge linaitwa la hovyo! na kilichofanyika ni uhuni!, mtu huyu hawezi kuachwa hivi hivi tuu au aitwe mbele ya kamati kuthibitisha kauli yake?

Na ikitokea asipoitwa, jee hii haitaaminisha alichosema ni kweli?, ndio maana nawauliza waungwana humu, jee ni kweli Bunge letu ni Bunge la hovyo? Jee ni kweli kilichofanyika kwa Bunge kuridhia hii IGA ya serikali yetu na Mwarabu wa Dubai ni uhuni? Mtu anayefanya uhuni ni muhuni, jee waheshimiwa wabunge wetu ni wahuni?

Paskali
Rejea za mtoa mada kuhusu Bunge
- Baadhi ya Wabunge ni Stupid!, Tanzania haina Demokrasia!, Bunge ni Rubber Stamp!- TBC, Watch Now!
 
Nakujibu kuwa wabunge wa CCM Ni wahuni au niseme hivi wabunge walioko Bungeni Ni wahuni na hawajitambui hata kidogo!

Wanajadilije kitu ambacho kimeshaandikwa kwamba kikitiwa saini hakitavunjwa, au kubadilika?
Na wakaletewa mzigo ulishatiwa sahihi tayari na wamwpewa siku moja ya kuchakata!
Ni wahuni bwana P!

Ila pia nimesoma andiko la Thadeus Ole Mushi, mama asipoangalia anahujumiwa as per urais wa 2025
 
Mzee unaogopa kuitwa tena kwenda kujieleza? Hivi unataka kusema Tanzania tuna bunge la wananchi kweli? Walichaguliwa na wananchi gani?

Maana kilichotokea 2020 hata mtoto mdogo anajua kilikuwa ni kitendo cha kihuni. Hivyo hata hao walioko ndani ya yale majengo, watakuwa ni wahuni tu.
 
Wanabodi,

Kama kawa kila nipatapo fursa, huja na makala zangu hizi za kwa maslahi ya taifa ambazo ziko kwa mfumo wa maswali, halafu majibu utayatoa mwenyewe wewe msomaji.
 
Wale ni wahuni tu.Hata kuingia bungeni waliingia kihuni.Mambo mengi wanayosifia na kupongeza ndiyo ymefanya maisha yetu kuwa magumu. Sheria za hovyo kama zile za kutoa Kinga kwa viongozi wasiostahili Kinga,Sheria za Kodi na tozo zinazofanya maisha yetu kuwa magumu,sheria za mafao tofauti kwa wanasiasa na watumishi wa umma (kikotoo) haya yote ni mtu mbinafsi tu anaweza kupitisha.
 
Back
Top Bottom