voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,553
- 11,885
Angalieni pia hizo video clips!
Kwanza ieleweke kwamba watanzania hawapingi uwekezaji wenye tija,ambao ni Win- Win situation!
Uwekezaji wa miundombinu na teknolojia kwenye miradi kama bandari kuu.Ni suala muhimu sana!hasa katika Dunia ya sasa ambapo mambo yanaenda kwa kasi sana!
Tunachokipigia kelele watanzania ni
"Aina ya mkataba na vifungu vyake tata na vya kinyonyaji!"
Wabunge badala ya kuongelea vifungu vya mkataba, wao walijikita kuongelea teknolojia ya Bandari!
Watanzania jana tulishuhudia "Uhuni" wa wanaojiita "waheshimiwa" ndani ya Jengo la bunge letu.
Badala ya kujadili hoja iliyokuwa mezani, wao waliingia kuipigia upatu.Ni wazi maamuzi walikwisha yaamua huko kwenye vikao vya "Party caucus" vilivyofanyika mfululizo tangia siku ya Alhamisi/Ijumaa hadi usiku.
Ni kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii,ambapo spika amelazimika kumsimamisha mbunge ili afunguwe bahasha kuepuka tuhuma za rushwa ndani ya bunge!
Hii ni baada ya tukio la kuonekana wakipewa bahasha mfululizo huku mjadala ukiendelea ndani ya bunge la CCM.
Kituko kikuu:
Wabunge wote walijikita kuutolea sifa mkataba na faida zake, bila kutaja vielelezo vyake!
Kwa ujumla wabunge waligeuka makuwadi wa madalali wa Deep world
(DP- world).
Shame on all of waheshimiwa......nikianza na Mwita Waitara,Nape Nnauye,Jerry Slaa,Dk Mollel na wenzao woote waliotumia muda wa serikali kushambulia watu binafsi.
Ila waelewe jana sio leo,watanzania wanazidi kujitambua kila uchao!
My Take:
Ni wakati sahihi kuwaonyesha watawala na CCM yao kwamba wananchi wanapaswa kusikilizwa na kupewa kipaumbele!
Pale linapokuja suala nyeti kama hili la ubinafsishaji wa Bandari zetu.
Wabunge hata wameshindwa kututoa hofu WANANCHI ni kwa nini mkataba huu umeletwa kwa njia ya zimamoto,tena siku ambayo siyo ya kazi kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi hii.
Hao wanaoitwa wadau 76 waliofika Dodoma kutoa maoni kwenye kamati ya pamoja ni kina nani.
Na je!
Ni asilimia ngapi ya idadi ya watanzania milioni 60?
Ukweli ni kwamba bunge limetumika kama "Muhuri" tu!
Maamuzi yamekwishqfanyika siku nyingi.
Na hivyo nimeamini kwamba ninaishi Jaa-mihuri ya TANZANIA.
AHSANTENI na Jumapili njema!