Mimi ni Muumini wa Bunge kuwa na nguvu dhidi ya Serikali

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,875
Mimi ni muumini wa Bunge kuwa na nguvu (Parliamentary Supremacy) dhidi ya serikali (Executive Supremacy) au chama (Party Supremacy).

Bunge ndiyo chombo au muhimili mkubwa (Principal organ) wenye wajibu wa kuisimamia serikali (Executive) kwaniaba ya Wananchi kwa mujibu wa ibara ya 63(2) ya katiba yetu ya JMT ya 1977.

Ukubwa wa Bunge dhidi ya mihili mingine ni kwasababu Bunge ni Wananchi ,Bunge lina mamlaka ya wananchi (Popular sovereignty) hivyo ili serikali (Executive) iwajibike kwa Wananchi kikamilifu na kustawisha maisha yao kwa mujibu wa ibara ya 8(1) b , c , ni lazima serikali isimamiwe kikamilifu na Bunge.

Inavyopaswa kuwa siku zote (What ought to be),Mikataba yote au MoU inayosainiwa kati ya serikali na serikali nyingine au shirika inapaswa iwe wazi na ipate ridhaa ya Wananchi kupitia wabunge / wawakilishi wao waridhie (approve) au kutoridhia (disapprove) kwa mujibu wa ibara ya 63(3)e .Hii inafanywa katika nchi nyingi,sababu inasaidia kulinda maslahi ya nchi ,kuongeza uwajibikaji,uwazi ,nidhamu katika utendaji wa serikali na kupunguza kiwango cha Rushwa na ufisadi.

Hatimaye,Tanzania tunanza kuona utamaduni Mpya wa mikataba ya kimataifa na makubaliano ya serikali kupelekwa Bungeni kujadiliwa na kuridhiwa ni hatua nzuri ila yenye kasoro kuu mbili.

1.Mikataba mingine haijapelekwa Bungeni na haijawekwa wazi ,hivyo kama dhamira ni kuheshimu mamlaka ya wananchi na Bunge na kufuata katiba ni vyema pia mikataba mingine iwe wazi na kupelekwa Bungeni pia .

2. Kuna utata kidogo , namna mkataba huu unavyopelekwa Bungeni . Ni kana kwamba Bunge linapelekewa kupitisha tuu bila kuhoji au kuwa na mamlaka ya kuukataa . Mfano,

Ukisoma mkataba (IGA) ibara ya 25 (Entry into Force kuanza kwa mkataba) inasema mkataba utaanza tumika mara tuu baada ya kusainiwa, na baada ya kusainiwa tuu shughuli za awali (Early Project Activities) zitaanza fanyika kama kujenga Barabara,upembuzi yakinifu, mkataba huu tayari ulisasha sainiwa na huenda shughuli za awali zimeanza.

Jambo la kushangaza ibara hii hii ya 25 ya mkataba inasema siku 30 baada ya kusainiwa mkataba huu , mchakato wa kuridhia mkataba huu kupitia Bunge uanze .

Hoja yangu ambayo nilimuuliza mkurugenzi Mkuu wa Bandari ndugu,Plasduce Mbossa kupitia Clubhouse,na sikuridhishwa na jibu sababu yeye alijibu shughuli za awali zinanza mapema ili kuwahisha mradi na hakuna athari yeyote.

Nilihoji,
Kulikuwa na uharaka gani wa shughuli za awali (Early Project Activities) kuanza kabla ya mkataba kuridhiwa na Bunge ? , Je ina maana serikali inajua tuu Bunge linakwenda tuu kuupitisha bila tatizo lolote ndiyo maana wakaridhia shughuli za awali kuanza? ,Sababu muwekezaji yeyote hawezi kuanza shughuli za awali kama anajua mkataba unaweza usipite ,kwa tafsiri hii , hoja ya mkataba kupelekwa Bungeni kujadiliwa ili kuidhinishwa ni danganya toto ,it is just a semblance for political legitimacy.

Lazima tuwe na Bunge ambalo serikali (Executive) haitakuwa na uwezo wa kutabiri kama jambo hili litapita au halitapita bila hivyo, suala la mikataba kwenda Bungeni kujadiliwa itakuwa haina maana yeyote.

Na ndiyo maana hoja ya kuwa na katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi inapaswa kupewa nguvu kwa sababu kama hizi ili kuvunja vunja Nguvu ya chama(Party Supremacy) dhidi ya nguvu ya Bunge (Parliamentary Supremacy), sababu inaonesha Party Caucus Bungeni ina nguvu kushinda Bunge lenyewe.

# Tuwe na Tume huru ya uchaguzi ili chaguzi zetu ziwe huru na haki ili Mbunge ashinde kwa kura za wananchi na sio wizi na figisu,hii italeta uwajibikaji Bungeni dhidi ya serikali.Pia kuwe na mgombea binafsi.

#Spika wa Bunge asiwe kiongozi wa chama ngazi yeyote,wala mjumbe wa vikao vya chama ngazi yeyote ile ,hili katika Rasimu ya pili ya Jaji warioba imekataza kabisa ibara ya 135 .

Mfano,
Spika wa Bunge Tulia Akson sasa ni mjumbe wa Kamati kuu ya chama,na kawaida maamuzi yeyote makubwa ya serikali huwa wanapeleka kwenye vikao vya chama kupata baraka ya chama.

Ikiwa chama kupitia Kamati kuu walibariki suala hili la Bandari ,ni wazi Spika wa Bunge Tulia Akson na yeye alibariki jambo hili (Unified Solidarity) .Je, Spika wa Bunge anaweza kuli-move Bunge lake kupinga mkataba huu hata kama una mapungufu?, Kuhoji kiasi cha kutaka mkataba huu ufanyiwe marekebisho?.

Hivyo , ni wajibu wetu sote kuiambia serikali na Bunge pia wasione aibu kufanya marekebisho katika maeneo ambayo mkataba huu una mapungufu na kama hauna Maslahi kwa Taifa letu tuachane nao na kama una Maslahi kwa Taifa letu ni wajibu wa serikali kutuambia ili tujue Maslahi hayo ni yapi ili sote tujue,pia serikali iwe tayari kuwajibika (Cabinet responsibility/Collective Ministerial responsibility )ikiwa mkataba huu utahatarisha Maslahi ya nchi hapo baadaye.


Abdul Nondo.
 
Hebu tusiongee mengi na kunukuu vifungu hovyo hovyo!

Hivi kweli Article namba 1 inasema Bandari zote kwenye Maziwa (lakes), bahari, dry Port na infrastructure zote anapewa muwekezaji nyie mnaona ni sawa kweli jamani
20230609_140823.jpg
 
Sasa udini wa kazi Gani ndugu yangu!
Udini upo, by necessary implications! Ndugu yangu Abdul watu sio wajinga , kuna watu wanaweza kufikiri sana tena sana na hilo kwa vile wewe ni msomi unalijua sana. Umeandika vema sana kwa kulemba lugha! Kwani huoni kuwa Samia ni mdini na mkabila wa kutupwa? Mbona Zito hajalikemea au kulizungumza kwa lugha anayoona yeye. (Zito is excellent katika kujenga hoja, anaona mbali, very vocal, intelligent as he has been ever, sasa ame mute Tangu samia awe rais).
Magufuli tulimchukia wote hata wakristo kwa vile alikuwa mkabila, upendeleo wa Chato, upendeleo wa kishenzi kabisa. Tulimkemea hapa hapa na Zito alimkemea kweli kweli.

Why is he keeping silent on this bandari saga? Zito tunayemjua asingelinyamaza katu! Ni wa dini yangu!

Kwanini bandari na ardhi ya zanzibar havipo kwenye unyanganyi wa bandari? What logical conclusion one can deduce from that?
 
Back
Top Bottom