Hii inawezekana kabisa kuwa ni PR kutoka URT na serikali ya kichaka. Technically, that's exactly what happened, that is Ballali's visa being revoked. Lakini kitu ambacho hawasemi ni kuwa, hii inamaanisha kuwa ile immunity ambayo gavana alikuwa nayo kutokana na wadhifa wake (diplomatic), iliisha pale kibarua chake kilipoota mbawa. Lakini yeye binafsi bado anaweza akawa na hiyo visa.
Kuwa au kutokuwa na visa hicho si cha msingi. Naamini hii ni danganya toto ili wadanganyika watulie. Binafsi naona kuwa URT (Chenge, Mgonja, Mramba, BWM, etc) wamemtosa Ballali ambaye ni samaki mdogo tu. Kuna papa wakubwa wanaohusika katika soo hili ambao wanalindwa huku Ballali akifanywa kafara.
Mkuu,
Hata mimi niliamini hivyo lakini sasa baada ya kusoma statement ya ubalozi naona sio hivyo. Kwasababu serikali ya Tanzania imemwulizia (hiyo ni diplomatic term, maana yake ni kubwa zaidi ya hiyo) basi tayari amehusishwa na corruption na USA haiwapi visa watu wanaotuhumiwa kwa corruption.
Hivyo ndiovyo nilivyolielewa hili suala kwasasa. Kila saa habari mpya zinakuja kwahiyo labda baadaye inaweza kuwa tofauti.
Lakini mpaka sasa naona ngoma inamshinda Ballali, serikali wameamua kumvaa, inaelekea yeye hana majibu. Ni kibaka tu, anapiga kelele kwamba hajaiba huku kila mtu anaona ameiba, mafuta yanamwagwa, imebaki kiberiti kuwashwa.
Hili ni fundisho sana kwa wasomi mafisadi. Ballali hakuwa na sababu ya kutuibia maana kwa kufanya kazi IMF na BOT alikuwa na pesa za kuishi kama King mpaka anakufa. Lakini mataa yakizidi, Waafrika tunataka tushindane na Bill Gate kwa mapesa.