BLACK MOVEMENT
JF-Expert Member
- Mar 11, 2020
- 2,712
- 6,511
Serikali ya CCM ni moja ya Serikali za Africa zinazo ishi kwa anasa kubwa sana, na katika vitu ambavyo Watawala wetu hawataki kusikiai ni kuishi ndani ya uwezo wa nchi.
Ruto kwa mwaka unao ishilia amesema waliamua kuchukua maamuzi magumu kupunguza matumizi ya Seriakli kwa Ksh Billion 400/ Hii alifanya ili kupunguza kukopa nje, kwa sababu some time wanakopa kuendesha Serikali.Hizi ni pesa mingi mno mno.
Bongo sio rahisi wapunguze matumizi ni kawaida kukuta msafara wa Waziri mkuu ukiwa na Magari zaidi ya 80 bado hapowa Makamo wa Rasi au Raisi mwenyewe, ni kawaida Watawala kuchomesha mafuta kutoka Dodoma hadi Dar, wao wako juu na V8 inafukuzia kwa chini. Kwa mwaka zinatumika Billion 500 na ziaidi kuagiza V8 pekee yake, maana yake kwa miaka 5 ni trilion 2 na billion 500 hizo ni za magari V8 bado mafuta na matengenezo yake sasa.
Kenya kwa sasa watawala wanahofia sana maandamano, wale raia sio wa kawaida ukiwaambia tutoke Barabarani kweli wanatoka, Tanzania watawala walisha soma raia wakajua ni mazezeta na hii wako sawa si walaumu kabisa na ndio maana wanatumia wanavyo taka na mwishi wa siku raia wanaongezewa Tozo ambazo Raisi hazimuhusu, Waziri mkuu hazimuhusu, Makamo wa Raisi hazimuhusu, mawaziri wote haziwahusu na kadhalika.
Ni Tanzania pekee kuna Ikulu 2 zenye hadhi sawa, elewa kwamba nchi nyingi Duniani zinaweza kuwa na ikulu ndogo ndogo ila ikulu kuu ni moja tu. Tanzania tuna ikulu ya Dodoma na Dar hizi ni ikulu 2 zenye hadhi sawa sawa kwa asilimia 100, only in Tanzania.Baadae tunaomba kujengewa matundu ya Vyoo na USAID.
Hapa sasa ndio unakuta V8 yanapishana Dodoma to Dar. Wiki hii wakuu wako Dodoma gari zinachomeshwa wese hadi Dodoma, wiki hii Dar gari zinachomeshwa mafuta hadi Dar.
Hizi cost za kuhudumia ikulu 2 zenye hadhi sawa mwisho wa siku tunazibeba sisi na ndio pale sasa unakuta huko vijijini wale ndugu zetu daily wanachangishwa michango ya kujenga Zahanati mara shule wakati kiuhalisia ni jukumu la Serikali make raia wanalipa kodi.
Binafisi nisha kataa kuchangia mchango wa iana yoyore kujenga Shule au Chochote kile ilihali Serikali ikiwa inaishi kwa anasa.
Ukiuliza leo utaambiwa Makandarasi hawajalipwa, kuna miradi imesimama pesa hakuna, ila hutakaa uone V8 zimepungua barabarani, Serikali haina pesa za maendeleo tu ila pesa za matumizi binafisi zipo za kutosha na si bure Bajeti huwa asilimia kubwa ni pesa za matumizi.