Mitihani mikuu mitano kwa gavana mpya wa BOT – Emmanuel Tutuba

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,603
Kwanza kabisa, Tanzania tumekuwa tukipata magavana wa benki kuu ambao walibarikiwa kuwa na taaluma nzuri kwenye masuala ya kiuchumi, na pia upande wa sheria kwa kumuangalia Prof Luoga ambaye amemaliza muda wake.

Hawa magavana ni watu walikuwa very intelligent, lakini pamoja na kuwa ‘very intelligent’ mara nyingi au mara zote, wamekuwa compromised na wanasiasa wa serikali kuu, na hata ikapelekea kusikia benki kuu ikitajwa kwenye skendo za ufisadi mkubwa wa mabilioni ya pesa kuanzia enzi za Balali, na mpaka ukija hii skendo ya Escrow kipindi cha Prof. Ndulu. Na haya matukio ya wanasiasa wa Tanzania ku compromise magavana wa benki kuu mpaka kujihusisha na skendo za upigaji, sio kitu cha mara ya kwanza na kigeni. Na hii, inatupa swali moja la msingi kuhusu uhuru wa benki kuu – ‘Je, benki kuu ya Tanzania ipo huru kiasi gani dhidi ya mikono ya serikali kuu?’

Msingi mkubwa wa hilo swali ni kwamba, inaonekana kabisa benki kuu ya Tanzania bado sio chombo ambacho kinafanya kazi zake kwa uhuru – kwamba kuna uwezekano mkubwa, sera za benki kuu kwenye masuala fulani fulani, bado yanaamuliwa na upande wa serikali, kitu ambacho kwangu mimi naona kabisa kinaweza kuwa na madhara kwa benki kuu katika kutekeleza majikumu yake ya msingi, hususani sera za kifedha, kulinda thamani ya shilingi, ufanisi wa vyombo vya kifedha na mikopo, na masuala mazima ya mfumuko wa bei.

1. Kwahiyo changamoto kubwa na ya kwanza kwa Emmanuel Tutuba ni kwamba, anaenda kufanya kazi kwenye chombo ambacho hakina uhuru dhidi ya serikali kuu, kwa maana hiyo kufanikiwa kwake pia kunahitaji utashi wa kiongozi aliyepo madarakani. Tumeona enzi za Balali na enzi za Prof Ndulu, namna viongozi wa wakati ule na utashi wao waliruhusu upigaji wa mabilioni ya fedha… kwahiyo bado na yeye (Tutuba) yupo 'prone to such scandals'. Hapa kwenye uhuru, nadhani Prof. Luoga kwa namna fulani ni kama alitaka kufanya mageuzi, ukiangalia zaidi kuhusiana na utoaji wa taarifa kuhusu deni la taifa ambalo naweza kusema ni mojawapo ya taarifa ambazo zimekuwa ni mwiba mkali sana kwa utawala uliopo. Na nina wasiwasi sana kama tutaendelea kupata taarifa kuhusu deni la taifa Kama ambavyo BOT wamekuwa wakizitoa kwenye kipindi cha Prof Luoga.

2. Ufanisi kwenye sekta ya mikopo kwa wananchi – hii ni moja ya mtihani ambao gavana Prof Luoga alishindwa kufanya chochote kwenye hili suala. Uhalisia ni kwamba, mabenki ya kibiashara yaliyopo Tanzania bado hawana ufanisi kwenye sekta nzima ya utoaji mikopo. Na hapa moja kwa moja nagusia mambo mawili ambayo ni mwiba mchungu sana kwa watanzania kutoka kwenye haya mabenki ya kibiashara, na nina amini kabisa, Gavana wa BOT ana mamlaka na wajibu mkubwa kurekebisha hii hali.

a) Riba kubwa kwenye mikopo – ukiangalia takwimu kwenye masuala ya riba kwa miaka karibu 17 iliyopita, watanzania wamekuwa wakikopeshwa kwa riba kubwa sana, kitu ambacho mimi naamini sio ‘fair’, kutokana na hoja moja kubwa sana kwamba, benki kuu ya Tanzania kwa nyakati tofauti wamekuwa wakileta sera za ‘accomodative monetary policy’, ambazo 'immediate impact' yake ni kushusha ‘cost of funds’ kwa mabenki. Lakini mabenki ya kibiashara ya Tanzania yamekuwa na ugumu wa kushusha viwango vya riba kwenye mikopo. Kwa tafsiri nyingine, kumekuwa na ‘a very weak transmission mechanism of our monetary policy’ – yaani sera za kifedha za BOT hazina manufaa ya haraka kwenye uchumi hususani ukiangalia viwango vya kukopa.

policy rate.jpg


premium.jpg


Ukiangalia hizo grafu mbili, ni kwamba, kwa miaka ya hivi karibuni kuanzia mwaka 2017 mpaka 2022, benki kuu ya Tanzania waliweza kushusha ‘Discount rate – policy rate’ kutoka asilimia 16 kwa mwaka 2017 mpaka leo hii tupo kwenye policy rate ya asilimia 5, lakini hatujaona mabadiliko yoyote kwenye riba za mikopo, ambapo unaweza kuona, almost zipo flat kwa kipindi chote hicho ambacho BOT wamekuwa waki 'pursue accommodative monetary policy'.

Matokeo yake ni kwamba, sera za kifedha za BOT zimekuwa indirectly zikiwanufaisha Zaidi mabenki ya kibiashara, ambayo kwa sasa yanashindana kutengeneza mabilioni ya faida, kitu ambacho ni 'sufferings' kwa wananchi.

Kwahiyo kwa gavana mpya – Tutuba, hii ni issue ya msingi na ya kuisimamia, kwasababu riba kubwa ni mwiba mkali kwenye uchumi, wenzetu Kenya kwa kipindi fulani ilifika mahali walileta ‘interest rate cap’ ambapo mikopo mpaka bunge la Kenya waliweka sheria kudhibiti kiwango cha riba kuvuka asilimia 13. Na mpaka leo, japokuwa ile ‘interest cap iliondolewa, ila bado kiwango cha riba Kenya ni kidogo sana. Na matokeo tunayaona, namna uchumi wa Kenya umekuwa vibrant.

b) Maamuzi ya mikopo kufanywa nje ya mipaka ya Tanzania – na hili nalo ni suala ambalo ni mwiba kwenye sekta ya mikopo ya nchi hii, na ambayo pia BOT wana mamlaka nayo. Tanzania kuna benki za makaburu kama Stanbic, Absa, NBC, Bank ABC etc… Tanzania pia kuna benki za Wakenya kama Equity Bank na nyinginezo… sasa matokeo yake, maamuzi ya mikopo ya hizi benki unakuta mara nyingi yanaamuliwa kwenye ‘Golf course’ za Johanessburg na Nairobi… Unakuwa na watu ambao hawafahamu vizuri soko la Tanzania, nab ado watu hao hao wanakuwa wanaamua ni nani akopeshwe ni nani asikopeshwe. Matokeo yake, hawa wamiliki wa haya mabenki kuna maamuzi ambayo wamekuwa wakifanya makossa, just kwa kutoelewa soko la Tanzania lilivyo, nah ii imepelekea watanzania kuendelea ku ‘suffer’ pale inapokuja suala la kukopa kwenye hizo benki.

3. Gharama za kibenki kwa watumiaji wa benki – Makato katika miamala ya kibenki.. sio rafiki kwa watanzania na nafikiri kwamba BOT wana meno Zaidi kuweka regulation za kumlinda mtanzania.

Kwa miaka mitatu au minne iliyopita, kumeibuka wimbi la gharama kubwa za miamala ya kibenki, hususani baada ya benki nyingi kuja na hizi technolojia za mobile money transactions. Benki nyingi sasahivi zimeweka fees kubwa sana kwenye miamala ya kibenki kupitia hizi mobile money apps, kitu ambacho mimi binafsi sioni kama ni sahihi sana kwa ufanisi wa kiuchumi. Huwezi kuwa na makato karibu asilimia 2 kwa transaction moja ya kutuma pesa kutoka kwenye account yako, huo ni unyonyaji wa hali ya juu.

Na ninashangaa sana, na inazidi kunishangaza, fair fees inatakiwa iwe ni ‘fraction ndogo sana sana’, lakini unakuta unatuma laki nane (800,000) kupitia mobile money kutoka kwenye account yako ya benki, unashangaa kukuta makato ya shilingi 17,000, ambayo ni karibu asilimia 2.1%, kwa transaction ya kutuma. Huu ni uhuni wa hali ya juu.

4. Huduma za kibenki jumuishi (Financial inclusion) - Gharama za miamala ya kwenye simu sio rafiki kwa sasa, na hii imedhoofisha huduma za kibenki jumuishi, ambayo marahemu Prof Ndulu alilipigania sana hili suala la huduma za kibenki juimuishi. Kwasababu Prof Ndulu, aliona ya kwamba, financial inclusion ni kitu kingeweza kusaidia ukuaji wa haraka wa uchumi hususani kwa watu masikini ambao wasingeweza kumudu huduma rasmi za kibenki.

Lakini kitu kimoja cha ajabu kilichotokea kwa upande wa serikali mpaka wakaamua kuja na hizi tozo, ni kwamba waliona sasa kwamba kuna fursa ya kutengeneza mapato ya kodi kwenye miamala ya simu kitu ambacho ni mojawapo ya sera ya hovyo sana. Kwasababu ile trend tulikuwa tunaona ya financial inclusion Tanzania, automatically imedumazwa na sera mbovu za kodi na tozo ambazo tumeziona kwa miaka 2 sasa.

Japo sina uhakika kama yeye mwenyewe ataweza kurekebisha hili suala la tozo au itabidi awashirikishe wizara ya fedha na TRA, lakini ambacho naamini ataweza kufanya, ni ku build a case ya kuweza kuangalia tena, kazi kubwa ya financial inclusion Tanzania na ikiwa ni haki kuendelea kuwa na ughali wa miamala kwenye simu.

Hapa nimekosa takwimu za ku support hoja yangu, ila kama kuna mtu anaweza kutafuta takwimu za miamala ya kifedha kwa miaka 5 basi ingependeza tupate ili tuweze kufanya trend analysis na kuangalia jinsi financial inclusion imekuwa affected na tozo za serikali.

5. Ufanisi kwenye sera za kifedha (Monetary policy) – nikizungumzia kwa upande wa credit growth (japo nimeshaainisha kwamba sekta ya mikopo inachangamoto) na kwa upande wa thamani ya shilingi dhidi ya dola, naweza kusema kwamba Prof. Luoga kuna namna fulani alijitahidi kuhakikisha kwamba thamani ya sarafu ya Tanzania inalindwa. Na kiukweli kabisa, ndani ya miaka 5 iliyopita shilingi ya Tanzania imekuwa fairly stable, na ni kipindi ambacho dunia imeshuhudia janga la Covid ambalo limekuwa ni mwiba mkali kwenye sarafu za baadhi ya nchi, hususani kama Kenya, ambapo sarafu zao zilipoteza thamani kubwa sana dhidi ya dola.

usdtzs.jpg



Kwahiyo tunategemea gavana mpya ataendeleza hili zuri lililofanywa na mtangulizi wake kuhakikisha kwamba, thamani ya shilingi dhidi ya dola inaendelea kuwa fairly stable, japo hiyo pia itategemea na namna uchumi wetu utavokuwa una perform, masuala ya deni la taifa, na pia namna benki kuu itakavokuwa inaunda sera zake za kifedha.

Pia kwenye issue ya ukuaji wa mikopo, kwa miezi 12 iliyopita Tanzania imeweza kuwa na ukuaji wa kasi sana wa utoaji wa mikopo ambao hatujaushuhudia kwa miaka mingi, nah ii inamaanisha pia kwamba, kwa kipindi hicho, kumekuwa na ukuaji wa shughuli za kiuchumi ambao ni mzuri kidogo, kwasababu hata ajira zimekuwa ni nyingi sana, kitu ambacho ni kizuri. Na ukuaji huu wa haraka wa mikopo umechochewa kwa kiasi kikubwa na sera ya BOT kwenye masuala ya sera za kifedha kwasababu hata ukiangalia Discout rate (BOT policy rate) ipo around 5% ambayo ni ndogo sana.


credit.jpg


Kwahiyo kwa kweli hapa Prof Luoga kwenye ufanisi wa monetary policy naweza kusema alifanikiwa kwa kiasi fulani, na nadhani kuna majarida kadhaa yalimsifia pia kwa hilo. Kuweza ku achieve accommodative monetary policy ambayo imekuza credit growth na at the same time kuwa na stable currency, hicho ni kitu cha kupigiwa makofi. Kwahiyo nadhani Gavana mpya ataiga hili jambo zuri.

Note: japo kama nilivyotoa angalizo kwamba, bado hatujafikia ufanisi kwenye hii mikopo kwasababu riba za kukupa bado sio rafiki kwa watanzania, na hichi ndo kitu ambacho nataka Gavana mpya aende akakishughulikie, ili basi mikopo itolewe kwa wingi Zaidi na kwa riba ambayo ni rafiki ili iwasaidie watanzania.

6. Uhuru kwenye miamala ya kutuma na kupokea fedha nje ya nchi i.e. paypal – hapa nadhani ni mahali gavana Prof Luoga alishindwa kabisa kushughulika na hiki kitu, na nadhani ni wasaa maalumu kwa gavana mpya kuweza kulifikiria hili suala na kulifanyia maamuzi upya. Hii ni sekta ambayo naweza kusema inaungana na ile ya financial inclusion kwenye urahisi wa kufanya e-commerce kwa wajasiriamali wa kitanzania. Na uzoefu hata kwa nchi jirani kama Kenya unatuonesha kwamba ili kusaidia wajasiriamali wadogo wadogo na watu masikini, hiyo inaweza kufanikiwa kwa kuweka mazingira rafiki kwenye sekta nzimo ya financial inclusion na kuondoa vile vikwazo vyote. Na mimi nashangaa sana ni kwanini mpaka sasa hakuna uamuzi juu ya hili suala? Kwasababu pamoja na serikali kuwazuia watanzania kutumia hizi technolojia, bado maelefu ya watanzania tumetumia njia nyingine kuweza kufanikisha hilo, na wengine wetu ilitubidi mpaka kutumia line za simu za mataifa ya nje. Kwahiyo naona ya kwamba, ni mambo ambayo gavana mpya anatakiwa kuona yana logic ya kufikiriwa tena kwa sababu ni mambo ambayo yana manufaa kwa wananchi walio wengi wenye kipato kidogo.

Kwahiyo kwa dhati namkaribisha ndugu Tutuba, na najua kabisa kwa mamlaka aliyonaye, hivi ni vitu ataweza ku take ownership na kuvisimamia, kwa sababu ni vitu ambavyo mimi binafsi naviona kwamba vinagusa taifa na wananchi wengi kwa ujumla.

Na endapo kama atashindwa kwenye haya masuala hapo juu, nadhani kabisa lazima tutaona matokeo kwenye namna mwenendo wa ukuaji na ufanisi kwenye uchumi, jinsi utavyokuwa mbovu. Kwahiyo atambue kwamba anaenda kuongoza taasisi ambayo ni sensitive kwenye uchumi wa nchi.

Wasalaaam!

N.Mushi
 
Analysis nzuri

Mi kilio changu ni gharama za kibenki ni kubwa sana.

Aishauri serikali iondoe VAT kwenye gharama za kibenki maana zinamuumiza mtumiaji wa mwisho.

Zamani makato ya ATM yalikuwa 800, ila kwa sasa ni 1300+

Ongezeko la 500 nzima
 
Dah, masta umeandika uchambuzi mmoja una madini sana.

Na umeandika katika namna mtu yeyote yule anaweza kuelewa na juu ya mada muhimu sana kwa maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Kudos!

Sent from my POCOPHONE F1 using JamiiForums mobile app
 
Analysis nzuri

Mi kilio changu ni gharama za kibenki ni kubwa sana....
Yaah hiyo pia ni hoja ya msingi... na hapo kwenye VAT nadhani ndo tunakuja kwenye upande wa fiscal policy.. na nadhani serikali anaweza akafanya jambo.

Ndiyo mana nikatoa angalizo mahali kwamba kuna baadhi ya points kwamba BOT itabidi ashirikiane na taasisi nyingine ili kurekebisha
 
Hapo kwenye paypal sijui wanakwama wapi? Sijui ni ushamba sijui na kutokua na exposure? Au ndio ile mtu kasoma chato akaenda shule ya kata akatoka hapo akaenda udsm yaani mtu wa hapa hapa with 0 exposure!

Wakenya wanatumia paypal vizuri sisi viongozi wetu wamelala fofo wanawaza tozo!!
 
Hapo kwenye paypal sijui wanakwama wapi? Sijui ni ushamba sijui na kutokua na exposure? Au ndio ile mtu kasoma chato akaenda shule ya kata akatoka hapo akaenda udsm yaani mtu wa hapa hapa with 0 exposure!

Wakenya wanatumia paypal vizuri sisi viongozi wetu wamelala fofo wanawaza tozo!!
Viongozi wetu wana kiburi
 
Back
Top Bottom